1) Jose Mourinho, OK,
Special One hakusajiliwa kwa namna ya kawaida kama wachezaji na
alimgharimu Roman kiasi kidogo tofauti na wachezaji wengi waliomfuatia
kuja Stamford
Bridge, lakini Chelsea isingekuwa hivi ilivyo bila Mourinho.
The Blues walifanikiwa kuutetea ubingwa wao msimu uliofuata na mreno
huyo akaiongoza timu hiyo kushinda League Cup na FA Cup bkabla ya
kuondoka September 2007 kwa makubaliano na Chelsea.Mapema mwezi uliopita Jose Mourinho alirudi rasmi kuifundisha Chelsea akitokea Real Madrid.
2) Didier Drogba
Alisajiliwa na Chelsea July 2004 kwa ada ya uhamisho wa £24m, Drogba alichukua muda kidogo kuanza kufunga pamoja na kufunga goli lake la kwanza katika mechi ya 3 ya kimashindano kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace.Mwanzoni, wachambuzi wa soka hasa wale wapenzi wa Chelsea hawakuwa wakimpa nafasi ya kufanya vizuri darajani, lakini Muafrika magharibi huyo baadae aliwaonyesha vitu vya hatari mpaka wakaanza kumtukuza kuliko baadhi ya wachezaji wengi wa timu hiyo.
Mshambuliaji alithibitisha ukali wake kwa kuwa mmoja wa wachezaji wa kuogopwa hasa kwenye mechi kubwa.
Akiwa ameshashinda makombe matatu ya Premier League, manne ya FA Cup, mawili yaLeague Cup ana ngao za hisani mbili, Drogba akajihakikishia nafasi katika historia ya Chelsea kwa kufunga bao la kusawazisha kwenye fainali ya UCL dhidi ya Bayern Munich kabla ya kufunga penati ya ushindi na kuipa ubingwa wa kwanza wa ulaya Chelsea.
Juan Mata aliwasili akitokea Valencia kwa ada ya uhamisho wa £23.5m August 2011 na alipewa tuzo ya mchezaji wa mwaka wa klabu baada ya kuisadia timu ya Roberto Di Matteo iliyoshinda ubingwa wa FA Cup na Kombe la mabingwa wa ulaya.
Kijana huyu anatajwa kuwa Gianfranco Zola, msimu uliopita aliiongoza Chelsea kushinda ubingwa wao wa kwanza Europa League. Japokuwa anatajwa kuwa anaweza kuuzwa za Mourinho darajani.
0 comments: