Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,” alisema Makalla.
Kauli hiyo
inaifanya timu za Yanga kupoteza ubingwa wake, huku Simba na Super
Falcon kuachana na mashindano hayo kutokana na sababu hiyo muhimu. Timu
hizo pamoja na Shirikisho la Soka nchini, TFF lilikuwa linasubiri
taarifa rasmi kutoka serikalini.
Awali, Rais
wa Shirikisho la Kandanda nchini, TFF, Leodegar Tenga alisema kuwa wao
hawana taarifa zozote kuhusiana na uamuzi wa Serikali zaidi ya kauli
yao ya kwanza.
“Sina taarifa, labda wewe una taarifa rasmi kuhusiana na uamuzi wowote kuhusiana na hatima ya timu za Tanzania katika mashindano hayo,” alisema Tenga ambaye pia ni Rais wa Cecafa.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alisema kuwa hali
ya usalama wa Darfur si nzuri na kuiomba TFF ifikirie upya uamuzi wa
upeleka timu Darfur kwani kuna ushahidi kuwa hali ya usalama si nzuri.
“Tuna
ushahidi kuwa hali ya Darfur siyo nzuri kiusalama, tumewaandikia TFF
kuwaeleza hayo na kuwaomba wafikirie upya ushiriki wa Tanzania katika
mashindano hayo,” alisema Membe.
Habari na Majuto Omary, Mwananchi
Chanzo - Mwananchi
0 comments: