Duru kutoka
kwa ofisi ya rais Jacob Zuma, zinasema kuwa Mandela mwenye umri wa miaka
94, yuko katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa.
Jamaa zake pamoja na aliyekuwa mkewe Winnie Madikizela-Mandela, walimtembelea hospitalini Jumatatu
Mwanawe Mandela Zenani (Mandela-Dlamini), pia alirejea kutoka nchini Argentina, ambako yeye ni balozi.
Serikali imekuwa ikisema kuwa hali ya Mandela inatia wasiwasi ingawa madaktari wameweza kuidhibiti.
Amekuwa katika chumba ya wagonjwa mahututi tangu kulazwa hospitalini Jumamosi kwa mara ya tatu mwaka huu.
Mwezi Disemba , bwana Mandela alilazwa hospitalini kwa siku 18 baada ya kupata maradhi ya mapafu,
Kumekuwa na
taarifa za simanzi kwa mara ya kwanza huku familia yake ikikusanyika
kando yake, baadhi ya watu wakisema kuwa ni muda wamwache Mandela aende
zake.
Bwana
Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi
, ikiwa ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.
Kwa mujibu
wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg
baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu. Msemaji wa serikali Mac
Maharaj amesema kuwa maafisa katika hospitali wanataka kudhibiti idadi
ya watu wanaozuru hospitali hiyo ili wampunguzie bwana Mandela usumbufu.
Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.
Kwa mujibu
wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa
watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu anapougua.
Lakini
mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna
matumaini madogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa
ubaguzi wa rangi, huenda akapona.
Anasema kuwa
wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa
babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.
Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.
Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.
Alifungwa
jela miaka 27 na anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa
akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa jela.
Chanzo - BBC Swahili
0 comments: