MWENYEKITI WA MAKAMPUNI YA IPP MEDIA, DK REGINALD MENGI AWAKABIDHI ZA WADI WASHINDI WA TWITTI WAZO JIPYA LA KUONDOA UMASIKINI


 Mshindi wa pili, Peter George akipokea kitita cha sh. laki 5
  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi kitita cha sh. milioni 1 mshindi wa kwanza wa shindano la  Twiti Wazo Jipya Kuondoa Umaskini, Jilly Gaudence Kyomo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute Of Management and Enterprenuership, Dk. Donath Olomi. Kulia ni mshindi wa pili, Peter George na mwanafunzi wa chuo cha CBE, Ludovick Angelino.
  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi shindano la Twiti Wazo Jipya Kuondoa Umaskini jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute Of Management and Enterprenuership, Dk. Donath Olomi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
---
Na Mwandishi Wetu

VIJANA watatu wa jijini Dar es Salaam, wameibuka washindi katika shindano la Dk. Reginald Mengi la ‘Kutwit’ kuondoa umasikini nchini.

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo lililopewa jina la Twiti Wazo Jipya Kuondoa Umasikini ni Jilly …. ambaye aliibuka na kitita cha sh milioni moja, Peter George (sh 500,000) na Ludovick Angelino (300,000).

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya IPP, Dk. Mengi alisema shindano hilo lina lengo la kuibua mawazo mapya jinsi ya kupambana na umasikini.

Alisema washiriki wa shindano hilo lililozinduliwa Mei 13 na washiriki wengi walijitokeza kuibua mawazo mapya na washiriki watatu ndio walioshinda.

Dk. Mengi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, alisema mchakato wa kupata washindi, ulisimamiwa na Kiongozi wa Taasisi ya Chuo cha Uongozi na Ujasiliamali (IMED), Donath Olomi na jopo lake.

Akizungumza jinsi washindi hao walivyopatikana, Dk. Olomi alisema jumla ya Twits 481 zimepokelewa kati ya Mei 13 hadi 31.

Alisema vigezo vilivyotumika katika mchakato huo ni wazo lililoeleweka  na kuelezeka kirahisi,  lisiwe wazo ambalo limeshasikika mara nyingi na liwe linaweza kutekelezeka.

Alisema mshindi wa kwanza Jilly alitoa wazo lililosema ‘Tuwe na utamaduni wa kupenda kile tukifanyacho, tukifanya kwa moyo, uadilif, heshima na kujali muda hata kama it’s self employed.
Share on Google Plus

0 comments: