KATIKA hali isiyo ya kawaida Jeshi la Polisi
wilayani Rombo,limelazimika kusimamia shughuli ya mazishi baada ya kundi
la watu wanne kuzuia mwili wa marehemu Gaspar Evarist (18) aliyefariki
kwa ajali ya pikipiki usizikwe shambani kwake kijiji cha Muriae,
wilayani Rombo.
Mkuu wa Polisi wilayani hapa, Ralph Meela alisema kuwa vurugu hizo
zilisababishwa na mama wa marehemu huyo na watoto wake wakitaka mwili
huo usizikwe kwenye shamba la baba yake mzazi bali wakauzike sehemu
nyingine.
Akifafanua zaidi Meela alisema chanzo cha mzozo huo ni baba wa
marehemu kufariki miaka mingi iliyopita na hivyo waliokuwa wakizuia
mwili huo walidhani kuwa endapo marehemu atazikwa hapo shamba hilo
litakua la kwake na hivyo watakosa urithi.
Alisema katika vurugu hizo zilisababisha uharibifu wa mali, kwani
wahusika walivunja msalaba wa jumuiya pamoja na kumzuia padre kuendesha
ibada ambaye ndugu walimtishia na hivyo kuondoka kuepuka vurugu hizo.
Baada ya polisi kufika waliwakamata watuhumiwa na kisha kusimamia mazishi hayo.
Wakati huo huo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la
Lewanga Kimario
(23) mkazi wa kijiji cha Mrere Mashati wilayani Rombo amefariki dunia
baada ya kujinyonga. Mkuu wa Polisi Wilaya ya Rombo,Ralph Meela
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Meela alisema kuwa tukio hilo
lilitokea Juni 25, mwaka huu majira ya saa 9:00 alasiri katika Kijiji
cha Mrere Mashati.
Meela alisema kuwa mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa umening’inia juu ya paa la nyumba yake.
Aidha alisema kuwa chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana. Kwa mujibu
wa baba mzazi wa marehemu, Thomas Kimario alisema kabla ya tukio
marehemu alikua akisumbuliwa na malaria kali na hivyo inaweza ikawa ndio
sababu ya kifo chake.
ROMBO KIMENUKA POLISI WAAMUA KUSIMAMIA MAZISHI BAADA YA VURUGU KUTOKEA MSIBANI
About author: Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: