Rais Kagame afanya mabadiliko kwenye uongozi mkuu wa jeshi na kumteua Jenerali Patrick Nyamvumba kuwa mkuu mpya wa majeshi.
Jenerali Patrick Nyamvumba amechukua nafasi ya jenerali Charles Kayonga aliyeshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 2002.
Mkuu
mpya wa majeshi ya Rwanda,alikuwa kamanda wa kikosi cha umoja wa
mataifa cha kulinda amani UNAMID katika jimbo la..... Darfur nchini Sudan
tangu mwaka 2009.
Mabadiliko
hayo pia yameshuhudia wadhifa mpya katika uongozi wa jeshi la Rwanda,
ambao ni wadhifa wa mkaguzi mkuu wa jeshi uliopewa Brigedia jenerali
Jack Nziza baada ya kupandishwa cheo na kuwa meja jenerali.Jack Nziza
amekuwa akihudumu kama mkurugenzi mkuu katika wizara ya ulinzi.Pia mkuu
wa zamani wa idara ya upelelezi wa nje kanali Dany Munyuza ameteuliwa
kuwa naibu kamishna mkuu wa polisi ya Rwanda.Sababu za mabadiliko hayo
hazijawekwa wazi.
Chanzo - BBC Swahili
0 comments: