
Mwanaharakati wa Ethiopia Bogaletch Gebre, ameshinda
tuzo ya kimataifa, kwa kampeini yake ya kupambana dhidi ya ukeketaji au
tohara kwa wasichana na wanawake.
Bi Gebre alituzwa tuzo yaMfalme Baudouin nchini
Ubelgiji kwa kuhamasisha dhidi ya tamaduni au mila ambazo ni haramu
kuzungumziwa , kulingana na kamati iliyomteua kuwa mshindi.
Alisaidia
katika kupunguza visa vya ukeketaji kutoka 100% ya watoto wasichana hadi
kufika 3% katika baadhi ya maeneo ya Ethiopia.
Ukeketaji hufanywa zaidi katika jamii za kiafrika na Mashariki ya kati.
Pia inajulikana kama tohara kwa wasichana ambacho ni kitendo cha kitamaduni kinachiaminiwa kuwafanya wasichana kuendelea kuwa bikira na kisha kumwezesha mwanamke kuoleka.
Katika ukeketejaji sehemu ya siri ya mwanamke
hukatwa hali inayomweka mwanamke au msichana yule katika hatari ya
kupata magonjwa na hata kupata matatizo wakati wa.... kujifungua.
Bi Bogaletch aliambia BBC kuwa ujumbe wake kwa
viongozi wa kijamii wanaopigia debe ukeketaji, alikuwa na kauli mbiu hii
kwao'' Baba wewe uliishi wakati wako, huu ni wakati wetu, wakati wa
watoto wetu. Hatutaki kuwaua watoto wetu. Natumai una busara ya kutosha
kukubali hilo.''
Wakfu wa Mfalme Baudouin ulimpa Bi Gebre dola
580,000 kama tuzo yake kwa kampeini yake ya kipekee kuhamasisha jamii
kuondokana na ukeketaji.
Shirika analofanyia kazi Bi Gebre alisema
lilianza kufanya mikutano na wanawake katika maeneo ambayo viwango vya
elimu ni vya chini mno na ambako ukeketaji ulikuwa unafanywa kwa sana.
Kwa kutumia kauli mbinu hii kote nchini Ethiopia, ilipeleekea kupunguza visa vya ukeketaji.
Bi Bogaletch aliambia BBC kuwa wanaounga mkono ukeketaji, wanaamini kuwa wanawake wanapswa kudhalilishwa.
"haina uhusiano na utamaduni , hatujui hata jambo hili lilitoka wapi,'' alisema Gebre
"vipi kitu ambacho kinawaua wanawake , kuwadhuru wanawake na watoto kukubalika?''
Mwezi Februari, Umoja wa Mataifa ulisema kuwa
takwimu zinaonyesha kuwa wasichana wachache barani Afrika na Mashariki
ya kati, wanakeketwa kwa lazima .
Nchini Kenya visa vya ukeketaji miongoni mwa watoto wadogo vinaendelea kupunguka.
0 comments: