MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara, hatimaye imetoa dhamana kwa Mbunge wa
Mtwara Mjini, Hasnein Murji (CCM). Akisoma dhamana hiyo, Hakimu wa
mahakama hiyo, Dynes Lyimo, alisema mtuhumiwa huyo atatakiwa kufika
mahakamani hapo Julai 4, mwaka huu. Alisema mtuhumiwa alitakiwa
kudhaminiwa Juni 10, mwaka huu, lakini alishindwa kutimiza masharti.
Alisema mshitakiwa akiwa nje kwa dhamana, hatakiwi kufanya mkutano wowote bila kibali cha.... Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara.
Alisema mali zilizowekwa dhamana, zitatunzwa na mahakama kwa mujibu wa sheria.
Mbunge huyo, alifikishwa mahakamani saa 2:10 asubuhi, akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Katika hatua nyingine, kesi inayowakabili viongozi wa vyama vinne vya siasa, inatarajiwa kutajwa leo.
Awali viongozi hao, walikosa dhamana baada ya wakili wao kuwa safarini.
Viongozi hao ni Hassan Uledi (NCCR), Hamza Licheta (TLP), Said Kulaga CUF na Katani Ahmed Katani (CUF).
Kwa pamoja viongozi wote, wanakabiliwa na kesi ya uchochezi, kula njama
na kuamsha hisia mbaya kwa wakazi wa Mtwara na Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
0 comments: