KAULI YA POLISI JUU YA ULIPUAJI MABOMU WAZUA BALAA KWA WANANCHI YADAIWA KUCHOCHEA JAMII


Advera-Senso
Inasikitisha kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai. Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika kinga ya kutetea watu wanaote........nda uhalifu - Advera Senso (pichani) Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania.

Kauli hii ya polisi imekuja baada ya kusikia kauli aliyoitoa  Mke wa  Henry Kilewo (Joyce Kiria) ambaye pia ni Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na kituo cha television cha EATV  kuwa hadi sasa hajui mumuwe alipo. Inasemekana mbele ya waandishi alioongea nao mtaa wa samora jijini - Dar es salaam leo, Joyce Kiria alipaza sauti na  kuomba msaada kwa Rais Jakaya Kikwete na watanzania  ili asaidiwe na kujua mahali aliko mume 

3

1a
Joyce Kiria (Mrs  Henry Kilewo   akiwa amebeba watoto wake wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini, Joyce amedai hajui mumewe ambaye ni  Kaimu Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa  Dar es Salaam, Henry Kilewo hajui alipo hadi sasa

Joyce Kiria siku ya jumamosi aliweza kuwajulisha marafiki kupitia ukurasa wake wa facebook habari za kuchukuliwa kwa mumewe   kutoka Central police na kupelekwa kusikojulikana kama inavyoonekana hapa chini
Share on Google Plus

0 comments: