Charles Mwijage ( Muleba Kaskazini-CCM) Mwenyekiti. Wengine ni Said Arfi (Mpanda Mjini-Chadema), Dk. Dalaly Kafumu (Igunga-CCM), Said Nkumba (Sikonge-CCM), Cynthia Ngoye (Viti Malum-CCM), Hamad Rashid Mohamed ( Wawi-CUF), Ramo Makani ( Tunduru Kaskazini-CCM) na Muhammad Amour Chomboh (Magomen-CCM).
Wajumbe
wengine ni Cecilia Paresso (Viti Maalum-Chadema), Rukia Kassimu Ahmed
(Viti Maalum-CUF), Mariam Kisangi ( Viti Maalum-CCM), Agripina Buyogera
(Kasulu Vijijini –NCCR-Mageuzi) na Suleimani Jafo (Kisarawe-CCM).
Alisema
hadidu za rejea ni kuchunguza chimbuko la mgogoro, kufuatilia hatua
zilizochukuliwa na serikali kutafuta ufumbuzi, kukutana na wadau
mbalimbali ili kupata maoni yao kuhusu mradi ya gesi asilia na kuangalia
mambo mengine yenye uhusiano na mgogoro huo.
Spika
alisema kuundwa kwa kamati hiyo kunatokana na kikao cha Kamati ya
Uongozi ya Bunge, ambayo ilipendekeza Bunge liende kuwasikiliza wananchi
kuhusu hofu ya kujengwa bomba hilo.
“Kamati ya
Uongozi iliagiza kuwa katika mazingira ya utulivu na amani, kamati
ikutane na wananchi mbalimbali na kuwasikiliza hoja zao. Nawasihi
wananchi, kamati itakapokuja wawe watulivu, wawazi, na huru kutoa mawazo
yao bila wasiwasi na mashaka,”alisema.
Alisema kamati itapata nafasi ya kutosha ya kukutana na wananchi, vikundi, taasisi na watu binafsi.
Kwa mara ya
kwanza vurugu hizo zilijitokeza Januari 31 mwaka huu, kupinga ujenzi
huo, lakini hali ya usalama ilikuwa mbaya wiki hii baada ya Wizara ya
Nishati na Madini kuwasilisha bajeti ambayo pamoja na mambo mengine
iliyozungumzia ujenzi wa bomba hilo.
Kutoka na machafuko Bunge liliahirisha shughuli zake Ijumaa na kuipa nafasi serikali itoe taarifa ya usalama mkoani Mtwara.
BY SHARON SAUWA
SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 comments: