Papa Francis aliyechaguliwa hivi karibuni, amekutana na waandishi wa
habari mjini Rome akisema kuwa atapenda kanisa maskini lenye lengo la
kuwasaidia maskini.Katika hatua ambayo Vatikani imesema inaonesha uwazi zaidi, Papa mpya
alizungumza na mamia ya waandishi wa habari na alisema alichagua jina la
Mtakatifu Francis wa Assisi kwa sababu aliku...... wa mtakatifu wa amani,
matumizi haba na kutumikia maskini
"Wakati wa uchaguzi wa papa mpya kando yangu alikuwa Askofu wa Sao Paulo, Claudio Hummes. Ukweli ulipokuwa unakaraibia alinipoza. Na kura zilipotimia thuluthi mbili alinikumbatia na kunibusu. Aliniambia "usiwasahau masikini". Na hilo limebaki nami...masikini, masikini"
0 comments: