KIKOSI cha timu ya Yanga leo kiliendelea kujifua katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiwinda na mechi yao ya Klabu Bingwa Afrika inayotarajiwa kupigwa Jumamosi ijayo dhidi ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Katika mazoezi hayo kocha mkuu wa kikosi hicho, Hans Der Pluijm, alianza na kuwafundisha wachezaji hao jinsi ya kupiga mashuti makali wawapo karibu na lango la adui. Sambamba na kupiga mashuti ya kumpoteza kipa wa timu pinzani, kocha huyo aliwafundisha wachezaji hao jinsi ya kuwahadaa mabeki wa timu pinzani.
Katika mazoezi hayo mshambuliaji tishio kwa magoli ya vichwa, Mrundi Hamisi Tambwe aliendelea kuwafurahisha mashabiki waliohudhuria mazoezi hayo kwa kupiga mabao safi kwa kutumia kichwa chake.
NA RICHARD BUKOS / GPL
0 comments: