Mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika unaanza leo katika
mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, ukihudhuriwa na wakuu wa nchi na
serikali wapatao 70 kutoka Ulaya na Afrika.
Makao Makuu ya Umoja wa Afrika

Kuitishwa kwa mkutano huu wa nne kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika
kuligubikwa na miito ya kuususia kutokana na kutoalikwa baadhi ya nchi,
kama vile Sudan ambayo rais wake Omar al-Bashir anakabiliwa na mashitaka
ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, na Zimbabwe, ambako mke wa rais Robert
Mugabe amewekewa vikwazo vya usafiri. Hata hivyo inatarajiwa kwamba
viongozi wa mataifa 40 ya kiafrika watahudhuria mkutano huo ambao
unafunguliwa rasmi mchana wa leo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye ni mmoja wa viongozi watakaoshiriki, amesema ushirikiano kati ya Ulaya na Afrika ni muhimu kwa maendeleo ya pande hizo mbili.
Mwanzo mpya wa uhusiano

Akizungumza leo kabla ya kuanza mkutano huo, rais wa Halmashauri kuu ya Ulaya Jose Manuel Barroso amesema mnamo miaka mitatu ijayo, Umoja wa Ulaya utatoa kiasi cha Euro milioni 800, kusaidia mradi wa pamoja baina ya Umoja huo na Afrika katika kuzuia mizozo.
Hata hivyo, rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf amesema hatua bora ambayo Ulaya yaweza kuichukua kusaidia bara la Afrika ni kusaidia kukua kwa uchumi wake.

Haki za binadamu kuangaziwa
Masuala mengine muhumu yanayotarajiwa kuwepo kwenye meza ya mkutano huo kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika ni yale yahusuyo mabadiliko ya tabia nchi, umasikini, uhamiaji na haki za binadamu, hususan kufuatia hatua ya Uganda kupitisha sheria dhidi ya ushoga, ambayo imekosolewa sana na washirika wake wa nchi za magharibi. Edmundo Matos kutoka chama tawala nchini Msumbiji, FRELIMO, amesema itabidi Ulaya ikubali ukweli kwambaAfrika inavyo vigezo vyake vya maadili ya jamii.

Jana, Umoja wa Ulaya ulitangaza kuwa unaanzisha ujumbe wake wa amani katika nchi hiyo, ambao umekuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu. Ujumbe huo utawashirikisha wanajeshi 1000, ambao watakwenda kuwaunga mkono wanajeshi wa Ufaransa na wa Umoja wa Afrika ambao tayari wanajaribu kutuliza mgogoro wa umwagaji damu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mwandishi: Daniel Gakuba/DPAE/AFPE
0 comments: