MAFUNDISHO YA MUNGU NA MTUMISHI WA MUNGU JOSEPHAT .E. MWINGIRA

Photo: Naibariki Jumatano yangu...
DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

(Darasa linaendelea lilipoishia jana...)
Ndivyo ilivyo katika maisha ya mtu, Mafanikio yake na Baraka zake; zina “Parasites” wadudu wanaokula hayo maisha yake. Sasa mdudu mkubwa anayekula maisha ya mtu ni laana, maana ndiye mdudu wa kwanza MUNGU alimtangaza. Tangazo la kwanza mdudu wa kuharibu maisha ya mtu ni laana, akasema maadamu umefanya kosa hili, nchi imelaaniwa.

Mnafahamu nchi ni udongo hivyo ardhi ikilaaniwa na ufahamu asili ya mwanadamu ni udongo. Sasa kimelaaniwa kile ambacho ni asili yako mwanadamu. Mti ukikata mizizi unanyauka na kukauka; tangazo la kwanza la kujua mateso ya mwanadamu tunajua kwamba asili yake imetokana na udongo kwa hiyo ardhi ambayo kwayo tumetoka. Na asili ya Baraka zote tunazoziona zinatokana na ardhi, fedha zinatoka kwenye ardhi, magari, miti, chakula, afya yako, nguo, wanyama, n.k. Sasa kipi ambacho hakikulaaniwa? Maana asili ya kile kitu ndicho kilicholaaniwa; hivyo hapa tunachotakiwa kuangalia kinachokutesa ni kuangalia laana gani inakutafuna wewe, maana laana ndiyo iliyotangazwa kwanza baada ya mwanadamu kukosa.
Share on Google Plus

0 comments: