JINSI KDF ILIVYOTIBUA UOKOAJI WESTGATE



Hadi sasa, Serikali haina habari yoyote ya ukweli kuhusu yaliyofanyika Westgate. Kamera za hivi punde zaonyesha baadhi ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) wakipora bidhaa kutoka katika maduka na benki ndani ya jengo la Westgate badala ya kuokoa watu.
Matarajio makubwa ya Wakenya yalikuwa kwamba jeshi lao litapambana na magaidi na kuwaokoa wananchi na mali zao, lakini matokeo yakawa kinyume.
Nairobi. Ni zaidi ya mwezi mmoja tangu Kenya ishambuliwe na magaidi wa Al-Shabaab.
Baada ya moshi kutokomea na waliouawa kuzikwa huku majeruhi wakiendelea kuuguza majeraha yao, maswali mengi bado hayajapata majibu.
Oktoba 18, runinga moja ya hapa nchini iliweka bayana kwenye habari zake jinsi mambo yalivyofanyika ndani ya jengo la Westgate tangu wavamizikuwasilia wakiwa wanaendesha gari ambalo walilinunua Septemba 6, mwaka kutoka kwa Mkenya mmoja ambaye hakujua kwamba alikuwa anawauzia watu wenye mpango mbaya.
Mpango ulivyosukwa
Kamera za usalama kwenye Benki ya Barclays iliyoko kwenye Barabara ya Mama Ngina, jijini Nairobi, zilinasa wavamizi wawili wakiingia kwenye benki hiyo na kutoa Sh365,000 (Sh6,840,000 za Tanzania) kutoka katika akaunti zao za kumlipa aliyekuwa amewauzia gari hilo.
Ndani la gari hilo siku ya tukio kulikuwa na wavamizi wanne ambao sasa majina yao yamejulikana baada ya uchunguzi wa kina wa ushirikiano wa Marekani, Israel na Uingereza kuwa ni Abu Baraa Al Sudani, Khatab Alakene, Umir Al Mogadish  na Omar Abdulraham Nabhan.
Wavamizi hao walikuwa wamepanga shambulizi hilo kwa umakini na wakafanikiwa kutekeleza kitendo chao cha kinyama bila kunaswa.
Si ajabu kwamba huenda walisaidiana na adui zetu kuvamia nchi ya mama yao. Tangu mwaka 2006 Kenya imekuwa ngome ya waasi ya al-Shabaab na mitandao yao ilikuwa imekita mizizi hasa katika eneo la Pwani, Kaskazini mwa nchi na Nairobi.
Jijini Nairobi, katika eneo la Eastleigh, asilimia 98 ya wakazi ni wenyeji wenye asili ya Somalia na ni kitovu cha Al-Shabaab nchini Kenya. Hapa ndipo ramani ya Westgate ilisomwa kwa makini na wavamizi walipokuwa wakijitayarisha kutekeleza maovu yao.
Inaaminika walipiga kambi kwenye nyumba mbili za wageni katika barabara za Eastleigh.  
Uvamizi huo ulifanyika peupe hivyo Polisi na Jeshi hawawezi kujitetea kwamba hawakuwa wanajua yote yanayopangwa na waasi wa al-Shabaab.
Share on Google Plus

0 comments: