ULIMWENGU APIGA MBILI, SAMATTA MOJA NA PASI YA BAO TP MAZEMBE IKIUA 4-2 NA KUTINGA NUSU FAINALI AFRIKA

WASHAMBULIAJI wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu jana kwa pamoja walifunga mabao matatu wakati TP Mazembe ikiifunga Entente Setif ya Algeria 4-2 mjini Lubumbashi na kutinga Nusu Fainail ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Thomas Ulimwengu alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na Samatta moja, wakati linguine lilifungwa na Tressor Mputu Mabi.
Ulimwengu aliifungia Mazembe bao la kwanza dakika ya nne kwa kichwa, ambalo halikudumu sana baada ya beki Mohamed Ziti kusawazisha dakika nne baadaye.
Watau hatari; Kutoka kulia ulimwengu, Mputu na Samatta jana


Mazembe ikazinduka na kupata bao la pili dakika ya 16 lililofungwa na Tessor Mputu, ambaye aliipangua safu ya ulinzi ya Setif na kumtungua kipa Sofiane Khedairia.
Ulimwengu akaifungia Mazembe la tatu dakika ya 27, akimalizia krosi maridadi ya Mbwana Samatta, ambaye alimtoka Abdelghani Demmou.
Jinsi Mbwana Samatta anavyopendwa Mazembe
Mazembe ilipata bao la nne dakika ya nne baada ya kutimia saa moja mchezoni kupitia kwa Samatta, ambaye alitumia vizuri udhaifu wa beki Demmou.
Samatta akimiliki mpira mbele ya beki wa Setif
Ulimwengu akitafuta njia ya kuchomokea
Tressor Mputu akitafuta mbinu za kumtoka mtu
Mputu alipata nafasi nzuri ya kufunga dakika tatu baadaye, lakini Khedaria akaokoa na Setif ikapata bao linguine dakika ya 71 kupitia kwa mshambuliaji wake, Kaled Gourmi, aliyemtungua vizuri kipa Robert Kidiaba.
Mazembe ilipewa penalti dakika za majeruhi, lakini kiungo Ngasanya Ilongo akapaisha.

Samatta akipambana katika mchezo wa jana
Samatta akivizia mpira udondoke afanye mambo
Stopila Sunzu anakaba
Robert Kidiaba akiwa amedaka
Timu hiyo ya DRC sasa imetinga Nusu Fainali ikiwa bado ina mchezo mmoja mkononi, baada ya kutimiza pointi 10 kutokana na mechi tano.
FUS Rabat, ambayo itamaliza na Mazembe katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo B, inaweza kuungana na akina Samatta na Ulimwengu ikiwa itawafunga wenyeji CA Bizertin ugenini Tunisia leo. Bizertin na FUS zimefungana kwa pointi tano kikla moja.
Share on Google Plus

0 comments: