KUMBE OBAMA ALIMTEUA MSAIDIZI WAKE WA IKULU AKIWA NAHIBU MKUU KUWA BALOZI WA ILI AJE TANZANIA

.
.mwananchi.co.tz wameripoti kwamba Rais wa Marekani Barrack Obama amemteua msaidizi wake wa karibu ambae ni Mark Childress kuwa balozi wa nchi hiyo Tanzania.
Childress ni msaidizi wa Obama katika Ikulu ya Marekani (White House) akiwa Naibu Mkuu wa Utumishi anayeshughulikia mipango katika Serikali ya nchi hiyo na aliwahi kufanya kazi katika Bunge la Seneti.
Obama amefanya uteuzi huo ikiwa ni wiki moja tangu alipohitimisha
ziara yake katika nchi tatu za Bara la Afrika, ikiwemo Tanzania.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani ilisema nafasi hiyo inahitaji kuidhinishwa na Bunge la Seneti la nchi hiyo kwa sababu uteuzi wake unaweza kuwa na maana kubwa katika kutekeleza sera za nje za Marekani.
Kuteuliwa kwa Childress kunaashiria kwamba Balozi wa sasa wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt anakaribia kumaliza muda wake, awali Childress ambaye aliwahi kuwa msaidizi na msiri wa muda mrefu wa Seneta wa zamani Tom Daschle, alitarajiwa kushika moja ya nyadhifa mbili katika utawala wa Rais Obama ambazo ni Mkuu wa Utumishi katika Idara ya Huduma ya Afya ya Jamii (HHS) au Naibu Mkurugenzi katika Ofisi ya Maboresho ya Afya katika Ikulu ya Marekani.
Share on Google Plus

0 comments: