
Meneja
wa bia ya Serengeti Allan Chonjo (wa pili kulia) akiongea kwa njia ya
simu na mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde Mwl.Michael
Valerian Mbuya katika mkutano na wana habari uliofanyika jana katika
ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam, kushoto kwake
ni Meneja mauzo wa Push Mobile Rugambo Rodney, kulia kwake ni Afisa
mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko na Mkaguzi
kutoka Bodi ya Michezo ya
Bahati Humudi Abdul Hussen(wa kwanza kushoto).25 Juni 2013, kampuni ya bia ya Serengeti imetangaza mshindi wa pili wa kampeni ya Winda na Ushinde ambae amejinyakulia kitita cha milioni moja baada ya kuchezesha droo yake ya pili. Droo hiyo ilichezeshwa katika ofisi za kiwanda hicho jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mhakiki kutoka katika bodi ya uchezeshaji promosheni bwana Humud Abdul Hussein.
Baada ya kupokea Michael Varelian Mbuya (29) ambae ni mwalimu wa sekondari kutoka Tabata Dar es salaam alionesha furaha yake na kubaki bumbuwazi kwa furaha. “Nina furaha isiyokifani kuwa mshindi wa promosheni hii ya Winda na Ushinde kutoka katika kampuni ya bia Serengeti na ntaitumia kufungua duka kwani ni ndoto yangu kubwa. Na najivunia kuitumia bia ya serengeti kwani ndio bia niipendayo na nawapongeza sana kampuni ya Serengeti kwa kuanzisha mashindayo haya na mpaka sasa nimeshajishindia bia nyingi pamoja na bia taslimu” alisema mshindi huyo.

Wakihakiki
namba za simu za mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde
iliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti, wa kwanza
kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo, Afisa mwandamizi
kutoka PWC Daniel Nnko(katikati) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya
Bahati Nasibu Humudi Abdul Hussen(kushoto)
Lengo la kampuni yetu ni kuendeleza umoja na mshikamano na wateja wetu kwa kuutambua na kuuthamini mchango wa wateja wetu kwani wao ni muhimili mkubwa katika kukuza na kuendeleza bai yetu ya Serengeti. Na sasa kampuni ya Serengeti inachezesha promosheni hii kutimiza azma yake ya kuinua uchumi wa wateja wao kama sehemu ya shukrani kwa wateja wake. Ni wakati wako ndugu mteja kushiriki mara nyingi uwezavyo na kuhakikisha unajishindia zaidi ya milioni saba. Ili kushiriki unatakiwa kufungua chini ya kizibo cha bia ya Serengeti na utakuta namba maalumu na unatakiwa kuituma kwenda namba 15317 na utapokea majibu.
Tafadhari kunywa kistaarabu na ni maalum kwa 18+
0 comments: