EOTF WANAWAKE WAKIWEZESHWA KIUCHUMI NA WAKIPEWA ELIMU YA UJASILIAMALI WANAWEZA KUTOKOMEZA UMASIKINI

Mama Anna Mkapa akizungumza katika semina hiyo
Washiriki mbalimbali katika semina hiyo
Picha ya pamoja kati ya Washiriki mbalimbali katika semina hiyo na mgeni rasmi.
WANAWAKE wakiwezeshwa kiuchumi na ikiwa ni pamoja na kupatiwa elimu ya ujasiriamali, kuepuka maradhi hatarishi na kufahamu haki zao katika jamii hali ya umaskini itapungua kwa kile kipato kuongezeka katika kundi hili kubwa la Watanzania.
Kauli hiyo imetolewa leo Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani.
Mama Anna Mkapa ambaye pia ni Mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii wajasiriamali hao kutoka
mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani, ambapo jumla ya wanawake wapatao 264 wanashiriki.
“Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote umekusudia kwa nguvu zake zote kuendeleza vita ya hii ya kuwawezesha wanawake  nchini kujikwamua katika wimbi la umasikini, maradhi na ujinga,” alisisitiza Mama Mkapa.
Aidha ameiomba Serikali, asasi za kiraia, taasisi za dini na wahisani binfasi ndani na nje ya nchi, kusaidia wanawke haswa wa vijijini kujikwamua na umaskini. Mama Mkapa aliongeza kuwa mfuko huo, kwa kipindi cha miaka 16 zaidi ya wanawake 6,820 wamepata mafunzo ya stadi za biashara na wengine 4,500 wamepata fursa ya kushiriki maonyesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa kupitia EOTF ili kutangaza na kuuza bidhaa zao.
Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Abdallah Kigoda akifungua mafunzo hayo alisema Serikali imeanzisha utaratibu wa kuweka kumbukumbu za mkopo katika mabenki kwa kupitia ‘Credit Reference Bureau’ ili kuweza kusaidia kuwafahamu wateja, na kuwaasa wajasiriamali wanapokopa wakumbuke kulipa kwani uaminifu ni kitu muhimu katika biashara.
“Suala lingine la kulipa kipaumbele ni lile la kuongeza thamani ya mazao wanayoyazalisha na tuache kuwazalishia watu wengine bidhaa wakaenda  kuongezea thamani kidogo tu kama vile kwa kufunga na kuweka nembo ya kibiashara na kuuza kwa bei kubwa,” alisema Dk. Kigoda.
Aliahidi kuwa Wizara yake iko makini kufanya linalowezekana kushirikiana na wajasiliamali hao kutatua tatizo hilo la kuuza malighafi badala ya bidhaa iliyoongezwa thamani ili kuongeza ajira na kupunguza umaskini.
Share on Google Plus

0 comments: