RAIS WA REAL MADRID AHAIDI KUMPA RONALDO CHOCHOTE ATAKACHO

Power-brokers: Perez (above) and Zidane (below) want to unite Ronaldo and Bale at the Bernabeu
Bumper deal: Perez is prepared to break the bank to keep Ronaldo at Real 
 RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez anajiandaa kumfanya Cristiano Ronaldo awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani katika jithada za kumshawishi abaki Bernabeu, baada ya kuondoka kwa Jose Mourinho.
Perez amesema: "Ningependa Cristiano Ronaldo awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani. Tunakwenda kufanya kila kitu katika mikono yetu kumfanya awe na furaha.Nyota huyo wa zamani wa Manchester United amekuwa akihusishwa na uvumi wa kurejea Old Trafford msimu ujao au kwenda kujiunga na Matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain - lakini Perez anapambana kumzuia Madrid kwa muda zaidi.......
Ronaldo amekuwa mchezaji mkubwa duniani tangu anunuliwe kwa Pauni Milioni 80 kutua Hispania mwaka 2009, akifunga mabao 146 katika mechi 135.
Rais wa Madrid pia amesema kwamba licha ya matatizo yote yaliyotokea na Special One msimu huu, wachezaji bao wanamzungumzia vizuri Mourinho.
Alisema: "Wachezaji wanamzungumzia vizuri tu Mourinho. Wameniambia alikuwa bora. Hatujui nani atakuwa kocha mpya. Tutazungumzia hilo wiki ijayo. Lakini tunataka Zinedine Zidane awe kiongozi wa mpango huu,"alisema.
Kazi ya kwanza ya Zidane ni kuhakikisha anamsajili nyota wa Tottenham, Gareth Bale kwa Pauni Milioni 65.
Share on Google Plus

0 comments: