MZUMBE SECONDARY YAFUNGWA...WANAFUNZI WAPEWA SIKU MBILI WAPOTEE KATIKA MAZINGIRA YA SHULE

Hii ndiyo kazi ya kuwazuia wanafunzi wenye vipaji wa shule ya sekondari Mzumbe iliyopo wilaya ya Mvomero baada ya wanafunzi hao kuandamana usiku wa manane kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro
Wananfunzi wakidato cha kwanza hadi cha sita katika shule ya sekondari Mzumbe Morogoro wamelazimika kuandamana kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa huo wakishinikiza kuboreshewa huduma muhimu.Maboresha wanayodai kuboreshewa shuleni hapo ni pamoja na miundombinu, kuondoa ubadhirifu, uongozi mbovu na kukomeshwa vitendo vya lugha chafu zinazo tolewa na baadhi ya walimu.Maandamano hayo yalizimwa mapema asubuhi baada ya jeshi la polisi kulazimika kufika katika eneo lasangasanga barabara kuu ya Iringa Morogoro ambapo maandamano hayo yalikuwa yamefika kuelekea.......
katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro.
Wananfunzi hawa wa shule ya sekondari Mzumbe Morogoro ya wenye vipaji maalum wanadai kuwa maandamano hayo yanatokea baada ya kuvumilia kwa muda mrefu na hivyo wameamua kupaza sauti zao wakibainisha matatizo lukuki yanayo wasibu ambayo yanaweza kushusha kiwango cha taaluma yao.
Share on Google Plus

0 comments: