FLAVIANA MATATA MAMBO YAMNYOKEA SOUTH AFRICA

MAMBO yamezidi kumnyookea mwanamitindo nyota wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata, baada ya kuingia mkataba wa kutangaza nguo za kampuni inayoongoza nchini Afika Kusini na Mashariki ya Kati, Truworths.Truworths inaongoza kwa kuuza nguo za jumla na rejareja siyo Afrika Kusini tu, ambako kuna maduka ya kuuza na kusambaza zaidi ya 400 na kuwapa kibali cha kufanya biashara hiyo katika nchi 14 za Mashariki ya Kati na Afrika. Hatua ya Flaviana kupata nafasi hiyo, imetokana na jina lake katika masuala ya maonesho mbalimbali ya mitindo katika nchi hiyo, Uingereza na Marekani ambako ndiko anafanyia kazi kwa sasa.
Share on Google Plus

0 comments: