KASHFA YA KIGOGO IKULU BADO INALINDIMA



Dar es Salaam. Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka ku......
jua hatima ya kigogo huyo jana.
Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.HABARI NA MWANANCHI
Share on Google Plus

0 comments: