SHILOLE AFUNGUKA KUHUSU MAVAZI YAKE



Na Imelda Mtema
NI siku nyingine tena tunakutana katika safu yetu maridhawa ya Staa na Mwana, kama kawa hapa tunakutana na mastaa ambao wamejaliwa kupata watoto. Nisikuchoshe, leo tunaye staa wa muziki na filamu Bongo,  Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambaye nilimtembelea nyumbani kwake....

Kinondoni, Dar. Shilole amejaliwa kupata watoto wa kike wawili ambao ni Joyce (10)  na  Rahma (6) ambapo anasema kuwa watoto wake ndiyo marafiki zake wakubwa na pia anafanya kazi kwa nguvu sana kwa sababu yao.

Mahojiano kati yake na mimi yalikuwa kama ifuatavyo.
:

Amani: Mambo Shilole?
Shilole: Mambo safi tu, karibu sana.
Amani: Mbona nyumba imepoa wanao wako wapi?
Shilole: Watoto wangu wako shule wanasoma ‘boding’.
Amani: Sasa wanavyokuwa mbali na wewe, huwakumbuki?
Shilole: Nawakumbuka sana lakini kwa sababu wana
itafuta elimu, sina jinsi.
Amani: Watoto wako wanachuliaje muziki wako haswa unapovaa viguo vya nusu utupu?
Shilole: Wanatambua kuwa mimi ni mama yao, muziki ndiyo kazi yangu hivyo heshima yangu iko palepale. Nguo zangu mbaya haziwezi kuchangia malezi mabaya kwa wanangu.
Amani: Huwa unawachalaza viboko wakikosea?
Shilole: Kwa kweli wanaponikosea lazima nivae uso wa kazi, wanakula mboko za uhakika kabisa lazima nibadilike kidogo maana bila kufanya hivyo huwezi kumfunza mtoto.
Amani: Kwa hiyo watoto wako unawaangalia mwenyewe?
Shilole: Ndiyo, mimi ndiyo baba na ndiyo mama. Tumetengana na baba yao siku nyingi.
Amani: Unapenda watoto wako wakikua wafuate nyayo zako?
Shilole: Yaani mimi hata siwapangii, chochote watakachopenda wenyewe.
Amani: Haya nashukuru Shilole.
Shilole: Haya karibu tena.
Share on Google Plus

0 comments: