Mwigizaji mwenye asili ya Zimbabwe, ambaye aliigiza kwenye filamu ya Walking Dead, ameteuliwa kuigiza mamake mwanamuziki mashuhuri Tupac Shakur.
Danai Gurira ambaye alizaliwa 1978 eneo la Grinnell, jimbo la Iowa wazazi wake walipokuwa wanaishi Marekani.
Gurira huigiza kama Michonne katika filamu ya Walking Dead.
Kwa mujibu wa tovuti ya habari za burudani Deadline, Gurira ndiye aliyeteuliwa kumuigiza Afeni Shakur kwenye filamu kuhusu maisha yake ambayo imepewa jina All Eyez on Me.
Mwelekezi wa filamu hiyo ni Benny Boom.
Mwanagenzi Demetrius Shipp Jr ataigiza kama 2Pac.
Afeni Shakur halisi, ambaye ni mwanaharakati wa zamani wa kisiasa na mfuasi wa chama cha Black Panther, ndiye mwandalizi mkuu wa filamu hiyo.
Tupac aliuawa kwa kupigwa risasi 1996, akiwa na umri wa miaka 25.
Wazazi wa Gurira, Josephine Gurira na Roger Gurira, walihamia Marekani 1964 lakini wakarejea Zimbabwe baada ya uhuru Desemba 1983.
Baada ya kumaliza masomo ya shule ya upili, Danai Gurira alirejea Marekani na kusomea shahada ya kwanza katika saikolojia chuo cha Macalester, na baadaye akapata shahada ya pili katika sanaa kutoka kitivo cha Tisch, chuo kikuu cha New York.
0 comments: