Choo kinachojisafisha chenyewe pamoja namtumiaji pia.

Kinaitwa CHOO chenye akili kinachofunguka chenyewe unapokikaribia na kujisafisha chenyewe, kimeonyeshwa kwenye maonyesho ya bidhaa za kielectroniki Mjini Las Vegas, Marekani. Kwa mujibu Wa msemaji wa kampuni ya Toto, choo hicho pia kina uwezo Wa kumsafisha mtumiaji kwa kutumia kifaa maalumu kinachotoa maji ya vuguvugu na hewa ya moto anapokuwa amekikalia.
Licha ya kuwa bei yake ni dola 9,800, zaidi ya vyoo milioni 40 tayari vimeuzwa. Mchakato wa choo hicho kujisafisha kutumia mchanganyiko wa dawa za Kusafisha pamoja na kioo maalumu kilichotengenezwa na madini ya Zirconium na Titanium oxide.

Share on Google Plus

0 comments: