Kikosi cha Young Africans kilichoanza dhidi ya Mgambo Shooting
Young
Africans mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu Tanzania bara leo wameendeleza
wimbi la ushindi baada ya kuichapa timu ya Mgambo Shooting kutoka mkoani
Tanga kwa mabao 3-0, mchezo uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Ikiwa na kumbukumbu ya ushindi katika
mchezo wake wa mwisho dhidi ya Rhino Rangers kwa mabao 3-0, kikosi cha
Young Africans kiliingia uwanjani kwa lengo la kuendeleza wimbi la
ushindi na ndivyo hali ilivyokuwa
Hamis Kiiza, Saimon Msuva na
Mrisho Ngasa walikosa mabao ya wazi dakika 15 za kipindi cha kwanza
kufuatia kutokua makini katika umaliziaji na kujikuta mipira yao ikitoka
pembeni mwa lango la Mgambo Shooting na mingine ikiokolewa na golikipa
wa Mgambo Shooting Tonny Kavishe.
Mbuyu Twite aliipatia Young
Africans bao la kwanza Young Africans dakika ya 31 ya mchezo kwa shuti
kali la mita 25 kwa mpira wa adhabu alioupiga na kujaa moja kwa moja
wavuni na kuamsha shangwe kwa washabiki wa Yanga.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 1 - 0 Mgambo Shooting.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo aliingia
nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' kuchukua nafasi ya Rajab Zahir
mabadiliko ambayo yaliongeza uwezo wa kumiliki mchezo na kulinda vyema
lango lao.
Dakika ya 50 ya mchezo, Hamis Kiiza 'Diego' aliipatia
Young Africans bao la pili kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinda mlango
wa Mgambo Shooting Tony Kavishe kumuangusha Didier Kavumbagu ndani ya
eneo la hatari na mwamuzi kuamuru ipigwe penati ambayo Kiiza hakufanya
makosa.
Didier Kavumbagu aliipatia Young Africans bao tatu la
mchezo dakika ya 67 ya mchezo baada ya mpira uliorushwa na mlinzi Mbuyu
Twite kumkuta Kavumbagu ambaye aliwazidi maarifa walinzi wa Mgambo
Shooting na kuukwamisha mpira wavuni.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 - 0 Mgambo Shooting.
Msimu
uliopita katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika
kati ya timu hizi Young Africans pia iliibuka na ushindi wa mabao 3-0,
mabao yaliyofungwa na Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na Nadir Haroub
'Cannavaro'
Young Africans: 1.Dida, 2.Twite 3.Oscar,
4.Rajab/Cannavaro 5.Yondani, 6.Chuji, 7.Msuva/Lusajo 8.Domayo,
9.Kavumbagu, 10.Ngassa, 11.Kiiza
0 comments: