Kiasi ya watu 12 wameuawa baada ya treni la abiria kuligonga basi
lililokuwa likivuka reli jijini Nairobi, Kenya. Shirika la Msalaba
Mwekundu la Kenya limesema watu wengine wamejeruhiwa kufuatia ajali hiyo
mbaya
Mabaki ya basi la abiria lililogongwa na treni jijini Nairobi
Ajali za barabarani zinazosababisha idadi kubwa ya vifo hutokea kila
mara nchini Kenya. Kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za barabara na mabasi
yanayojaa abiria kupinduka, kila mara huendeshwa kwa mwendo wa kasi na
kuyapita magari mengine ili kupata faida ya haraka.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, gari hilo lilikokotwa kwa takribani mita 500 kutoka eneo la ajali. Mkuu wa polisi jijini Nairobi Benson Kibui amesema basi hilo la abiria lilivuka reli wakati treni hilo lilipofika kwa mwendo wa kasi. Ajali hiyo ilitokea wakati wakaazi wengi wa jiji walipokuwa wamejaa barabarani wakielekea makazini saa za asubuhi.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri:Josephat Charo

0 comments: