MSHAMBULIAJI wa Wigan, Arouna Kone
amekwenda kufanyiwa vipimo vya afya Everton leo huku The Toffees
wakijiandaa kuipiga bao Newcastle kumnunua mchezaji huyo anayeuzwa Pauni
Milioni 5.
Kocha mpya wa Everton, Roberto Martinez
anatarajia kuungana tena na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29,
ambaye alimfundisha akiwa Uwanja wa DW.
Mwanasoka huyo wa Ivory Coast amefunga
mabao 11 katika Ligi Kuu ya England katika msimu wake wa kwanza England
na aliiwezesha Wigan kutwaa Kombe la FA, lakini hajafanya siri juu ya
kutaka kwake kuondoka katika klabu hiyo baada ya kushuka Mei.
Kone alikataa kuhamia Tyneside mapema wiki hii kwa Pauni Milioni 6.
Klabu zote zimepewa ruhusa kuzungumza na Kone aliyesaini Mkataba wa miaka mitatu na Wigan msimu uliopita.
0 comments: