Askari wa kikosi cha ulinzi wa Rais wa
Marekani, wakiwa juu ya paa la Uwanja wa Ndege wa Zamani, wakiangalia
usalama kabla na baada ya kuwasili kwa Rais wao, Barack Obama, uwanjani
hapo, ambapo aliagwa rasmi na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete na
mkewe mama Salma, waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mkuu wa Mkoa Said Sadiki,
Wakuu wa Wilaya za Temeke, Sofia Mjema na wa Ilala, Raymond Mushi, Meya
wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula
na Ushirika, Adam Malima pamoja na viongozi wengine. (Picha zote na
Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Hapa Askari hao, wakirekebisha vifaa vya mawasiliano wakiwa juu ya paa la Uwanja huo, wa Zamani.
Hapa Askari hao, wakifunga vizuri vifaa vyao hivyo vya mawasiliano uwanjani hapo.
Wananchi waliojitokeza kumuaga Rais Barack Obama wa Marekani wakipunga bendera za Tanzania na marekani, uwanjani hapo leo.
Moja ya ndege inayofuatana na ndege ya
Rais wa Marekani, Barack Obama, Airforce One, ikiwa uwanjani hapo
ikisubiri kuondoka pamoja na Airforce One.
Hapa baadhi ya Makamanda na Maofisa wa
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi wakiwa uwanjani hapo
kumsubiri Rais Obama awasili kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza
ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said
Sadiki (kulia), akiwa na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa,
uwanjani hapo kusubiri kumuaga Rais Barack Obama wa Marekani.
Hapa anaonekana mmoja wa mbwa
anayetumika katika ulinzi na walinzi hao wa Rais Barack Obama, akiwa
katika kuangalia usalama uwanjani hapo leo.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na mgeni
wake, Rais Barack Obama wa Marekani baada ya kuwasili uwanjani hapo
tayari kuagwa kwa safari yake ya kurejea nyumbani nchini Marekani baada
ya kuamaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Rais Barack Obama wa Marekani,
akisalimiana na kuagana na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu,
Salva Rwemamu, katiakti yao akionekana Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond
Mushi na kushoto, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema.
Rais Barack Obama wa Marekani,
akisalimiana na kuagana baadhi ya viongozi, uwanjani hapo. Kushoto ni
mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete na mkewe, Mama
Salima wakiwa na wageni wao, Rais Barack Obama na mkewe, Michelle
wakiangalia ngoma za utamaduni pamoja na kuwaaga wasanii wa vikundi
hivyo vya burudani, vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa kuwaaga uwanjani
hapo leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimuongoza mgeni
wake, Rais Barack Obama wa Marekani kuelekea kwenye uwanja wa ndege kwa
ajili ya kupigwa nyimbo za Taifa za Tanzania na Marekani ili kuagwa
rasmi.
Rais Barack Obama, akiwapungia wananchi
pamoja na viongozi waliofika uwanjani hapo kumuaga wakati akielekea
kwenye ndege yake tayari kwa safai ya kurudi nyumbani nchini Marekani
leo.
Rais Barack Obama, akizungumza na watoto
wa Rais Jakaya Kikwete, waliofika uwanjani hapo kumuaga wakati
akielekea kwenye ndege yake, tayari kwa safari ya kurejea nyumbani leo.
Wake wa Marais Jakaya Kikwete, Mama
Salma (kushoto) na Barack Obama, Michelle (kulia), wakiagana kwa
kukumbatiana huku waume zao wakiwaangalia.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (kushoto) na Balozi wa Afrika Kusini
nchini Tanzania, Thanduyise Chiliza.
Airforce One ikiruka uwanjani hapo baada ya Rais Barack Obama kuagwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete.
Airforce One ikianza kupaa baada ya kuruka uwanjani hapo.
Rais Jakaya Kikwete na Balozi wa
Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, wakipungia ndege iliyomchukua Rais
Barack Obama, wakati ikiruka uwanjani hapo leo.
Rais Jakaya Kikwete akifuta machozi huku
akiangaliwa na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, wakati
ndege iliyombeba mgeni wake, Rais Barack Obama wa Marekani ikiruka
angani.
Hapa Balozi wa Marekani nchini, Alfonso
Lenhardt na Rais Jakaya Kikwete, wote wakionekana kufinya macho
yaliyokuwa yakilengwa lengwa na machozi baada ya ndege iliyokuwa
imembeba mgeni wake, Rais Barack Obama wa Marekani kuruka angani.
Hapa Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Mkuu
wa Mkoa, Said Sadiki (kulia), wakifuatilia ndege hiyo, iliyokuwa tayari
angani. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernad Membe na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam
Malima.
Hapa Balozi wa Marekani nchini, Alfonso
Lenhardt akionekana bado akiendelea kufuta machozi huku Rais Jakaya
Kikwete (kulia), akimcheka pamoja na waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anayeshikwa mkono na Rais
Kikwete pamoja na Waziri Mkuu mizengo Pinda.
Hapa Rais Jakaya Kikwete, anaonekana bado akibana macho yake.
Hapa Rais Jakaya Kikwete sasa akiwa
ameweka vizuri mawani yake na kulia Mkuu wa Mkoa, Said Sadiki
wakiangalia kwa vizuri ndege hiyo iliyokuwa ikipaa mawinguni. Hapa Rais Jakaya Kikwete
(kushoto), Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt (kulia) na Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), wakiwa na nyuso za
tabasamu baada ya mgeni wao, kuondoka salama nchini.
0 comments: