Beki
wa Yanga, David Luhende ameongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa
ajili ya mechi dhidi ya Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza
Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zitakazofanyika
mwakani nchini Afrika Kusini.
Kocha
Kim Poulsen amesema kutokana na uamuzi huo wa kumuongeza beki huyo wa
kushoto amemuondoa mchezaji mmoja kwenye kikosi chake. Mchezaji huyo ni
mshambuliaji Zahoro Pazi wa JKT Ruvu.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager sasa itaingia kambini
kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam, Julai 3 mwaka huu badala
ya Julai 4 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Mechi
ya Uganda itachezwa Julai 13 mwaka huu, saa 9 kamili alasiri kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati ile ya marudiano itachezwa wiki
mbili baadaye jijini Kampala, Uganda.
Wachezaji
wanaotakiwa kambini ni Aggrey Morris (Azam), Aishi Manula (Azam), Ally
Mustafa (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo
(Yanga), Haruni Chanongo (Simba), John Bocco (Azam), Juma Kaseja
(Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar) na Kelvin Yondani (Yanga).
Wengine
ni Khamis Mcha (Azam), Mrisho Ngasa (Simba), Mudathiri Yahya (Azam),
Mwadini Ali (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Salum
Abubakar (Azam), Shomari Kapombe (Simba), Simon Msuva (Yanga) na
Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar).
0 comments: