WANAOTENGENEZA ACCOUNT ZA MASTAA FACEBOOK WAUMBUKA NI BAADA YA WENGI KUGUSHI AKAUNT ZA MASTAA
Hii ni baada ya watu wengi kugushi account na funny page za mastaa na watu maashuhuri ilikujipatia umaarufu pamoja na wafwasi (Followers) wengi,baada ya mastaa wengi kulalamikia mtandao huo kwa kutokuwepo kwa huakiki wa account pamoja na funny page za sasa Facebook imeamua kufuata mkondo wa Twitter kwa kuanzisha akaunti na kurasa zilizothibitishwa (verified pages/accounts) ili kuwawezesha watu mashughuli kuthibitisha akaunti akaunti na fan page zao. Facebook wamesema wamefanya hivyo ili ku...........
saidia watumiaji wa Facebook kuzitambua akaunti za kweli za mastaa na watu wengine mashughuli wanaotumia mtandao huo, pia ikiwemo biashara zenye majina makubwa.
Kurasa zilizothibitishwa zitakua na alama ya blue ya pata “check-mark” kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu. Watu wataoruhusiwa kutumia huduma hiyo ni, viongozi wa serikali, waandishi wa habari maarufu, makampuni au bidhaa maarufu. Hivyo kuanzia sasa, utaweza kufahamu akaunti/pages zipi ni za kweli na zipi ni feki.
Ili mtu mashughuli kupata akaunti iliyohakikishwa, mhusika atahitaji kuwasilisha kitambulisho halali kinachotambuliwa kiserikali.
About author: Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: