Mzozo wa
kisiasa umeibuka nchini Zimbabwe baada ya rais Robert Mugabe kutoa agizo
kuwa uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika tarehe Thelathini na Moja
Julai mwaka huu. Waziri
mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, ametoa taarifa muda mfupi tu baada
ya agizo hilo la rais, akisema kuwa rais Mugabe amekiuka sheria kwa
kutoshirikisha bunge na ameapa kupinga uamuzi huo.Katika
kikao na waandishi wa habari, Tsvangirai, amemshutumu Bwana Mugabe kwa
ku.......kiuka mkataba wa ugavi wa mamlaka uliosainiwa miaka mitano iliyopita,
baada ya mzozo kuhusu matokeo ya kura kusababisha ghasia nchini humo.
Tsvangirai
ametaka uchaguzi huo kuhairishwa hadi mageuzi ya kikatiba yafanyike ili
kuhakikisha zoezi hilo la uchaguzi linafanyika kwa njia huru na haki.
Bunge la
nchi hiyo bado linajadili mswada wa sheria ambao utaruhusu vyama vyote
vya kisiasa kupewa nafasi sawa katika shirika la habari la serikali
wakati wa kampeini.
Lakini wiki
mbili zilizopita mahakama ya kikatiba nchini humo iliagiza kuwa uchaguzi
huo ni sharti ufanyike kabla ya mwisho wa Julai.
Chanzo - BBC Swahili
0 comments: