SOMA HABARI HII YA KUSHANGAZA ALIEBAKA MPAKA KUUWA AZIKWA KABURI MOJA NA MAREHEMU AKIWA HAI NA MAREHEU

ufukuaji wa makaburi ni tabia ambayo zamani ilikuwa ikifanywa kwa minajili ya kuiba vitu vya thamani wanavyozikwa navyo marehemu, siku hizi ni kwa ajili ya kukata viungo vya marehemu hao
Kijana mmoja ambaye alikuwa akituhumiwa kumbaka mwanamke mmoja huko nchini Bolivia, amezikwa akiwa hai katika kaburi ambalo amezikwa mwanamke ambaye alituhumiwa kumbaka.Taarifa ya awali ya Polisi, imeelezea kuwa upelelezi wa awali umeonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 17, alishiriki katika tukio la kubakwa na kuuawa kwa mwanamke mwenye miaka 35 katika manispaa ya Colquechaca.Mkuu wa Polisi wa eneo hilo ameeleza kuwa, zaidi ya....
wananchi 200, walimkamata kijana huyo anayetajwa kwa jina la Santos Ramos na kumzika akiwa hai katika kaburi ambalo mwanamke huyo muathirika wa tukio hilo alikuwa anazikwa.
"Walizuia barabara, waliweka vizuizi vya kuingia na kutoka katika eneo la mji huo ili kuzuia poliei kuweza kuwaingilia katika zoezi lao hilo" ameongeza msemaji huyo.
Mwandishi mmoja wa habari ambaye hakupenda kutambulika kwa hofu ya kukumbana na hasira za wananchi hao, ameeleza kuwa, Ramos alikamatwa na kufungwa kamba kabla ya kutumbukizwa katika kaburi ambalo mwili wa mwanamke aliyeuawa ulikuwa umetumbukizwa kwa ajili ya maziko.
Imetafsiriwa toka BBC
Share on Google Plus

1 comment: