SIRI YA ZIARA YA OBAMA SASA YAJULIKANA SHUGHULI NZIMA YA MAANDARIZI YAKE KUFANYWA NA MAAFISA WA MAREKANI





 MAANDALIZI ya ziara ya Rais wa Marekani hapa nchini, Barack Obama yamezidi kushamiri na sasa Wamarekani ndio wanaoongoza karibu kila idara wakitumia vifaa vyaoEneo ambalo linaonekana kumilikiwa na Wamarekani kwa asilimia karibu zote ni lile la mawasiliano, ambapo inaelezwa kuwa maofisa wao ndio watakaoongoza kila kitu ikiwemo kufanya ukaguzi wa watu watakaoingia uwanjani hapo kesho kwa ajili ya kumlaki Obama. Habari
zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa kikao maalumu kimefanyika juzi, kikiwahusisha maafisa wa juu wa Marekani na Tanzania kwa ajili ya kutengeneza programu itakayofanikisha ziara ya rais huyo wakati atakapotua kesho na kuondoka Julai 2.
 Kwa mujibu wa habari hizo ambazo pia zilithibitishwa na Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Moses Malaki zinaeleza kuwa maandalizi makubwa hadi kufikia jana yalikuwa tayari, ingawa kuna vifaa ambavyo Tanzania haikuwa navyo hivyo kuwaomba Wamarekani.

Katika kikao hicho, inaelezwa kuwa maofisa wa Marekani ambao sasa wameteka karibu idara zote muhimu ambazo zitafanikisha usalama wa kiongozi wao, walihoji kuhusu huduma mbalimbali nchini na kutaka ipate orodha ya vitu vilivyopo na ambavyo havikuwepo.

Miongoni mwa vitu ambavyo vilikosekana au havikuwa katika hali nzuri ni pamoja na ngazi ya kushukia Obama kwenye ndege.

Akizungumzia hilo, Mkurugenzi huyo wa uwanja wa ndege Malaki, alisema ngazi hiyo haikuwepo jambo ambalo liliilazimisha Marekani kuleta ya kwao.
Share on Google Plus

0 comments: