Miezi, ziki na siku za mingong'ingo, hatimaye vimefikia ukomo sasa baada ya klabu ya Chelsea kumthibitisha rasmi Jose Mourinho kuwa meneja wake mpya akichukua nafasi ya nafasi iliyoachwa wazi na Rafa Benitez.Kocha huyo ambaye anarejea klabuni hapo kwa ajili ya kuongoza jahazi la The Blues kwa mara ya pili, amekuwa akielezwa kuwa angejiunga na klabu hiyo kwa muda wa miezi kadhaa na mgogoro baina yake na wachezaji kadhaa wa Real Madrid alikokuwa akifundisha, ulitajwa kama chachu ya yeye kutaka kuondoka Uhispania. Alishinda mataji mawili mfululizo ya Ligi Kuu ya Uingereza katika awamu yake ya kwanza ya kuwa na Chelsea kabla ya......
kufungashiwa virago vyake kutokana na kile kilichokuwa kikielezwa kuwa ni mahusiano mabaya baina yake na mwekezaji wa Chelsea, Roman Abramovic
Akiongea muda mfupi baada ya kutambulishwa rasmi mchana wa leo, Mourinho amesema kuwa, katika maisha yake ya soka, amekuwa na nyakati za furaha zaidi wakati alipokuwa Chelsea na alipokuwa Inter Milan, lakini kumbukumbu nzuri zaidi a maisha yake ya soka ziko Chelsea.
Hata hivyo, mkutano rasmi na waandishi wa habari wa kumtambulisha mreno huyo unatarajiwa kuwa siku ya jumatatu ya Juni 10, na atakuwa akiungana na makocha wengine watatu kama wasaidizi wake. Makocha hao ni Rui Faria, Silvino Louro na Jose Morais.
0 comments: