Na Mwandishi Wetu, Rombo
SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwepo kwa ugonjwa
wa homa ya nguruwe wilayani Rombo, baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo
wameiomba Serikali kuhakikisha inatoa elimu zaidi juu ya maambukizi ya
ugonjwa huo ili kudhibiti maambukizi zaidi.
Kauli hiyo imetolewa mjini hapa kwa nyakati tofauti na....
wananchi huku
wakisisitiza kuwa ipo haja kwa Serikali kupitia wataalamu wake kutoa
elimu kutokana na ukweli kwamba wananchi wengi hawana uelewa kuhusu
namna ugonjwa huo unavyoambukizwa na athari zake kwa binadamu.
“Kuna watu hapa wanachinja mizoga ya nguruwe wanakula na hata
kuwauzia watu, hii ni dhahiri kuwa hawajui madhara yake,” alisema
Hermani Massawe Mkazi wa Usseri.
Hata hivyo wananchi pia wameitupia lawama serikali kwa kitendo cha
kushindwa kupeleka wataalamu wa mifugo maeneo ya vijijini ili watoe
chanjo ya ugonjwa huo. Mmoja wa wakazi wa Usseri, Daria Pius aliongeza
kuwa wanashangaa kuona wataalamu wa mifugo wakiishia maeneo ya mijini tu
huku maeneo ya vijijini kusahaulika wakati ndio wahitaji wakubwa wa
huduma hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: