Makamu wa kwanza wa serikali ya Zanzibar Maal Self Sharifu Amadi amevitaka vyama vya siasa nchini kutoleta uhasama wala chuki miongoni mwa jamii ya kitanzania. Ameyasema hayo jana wakati akihutubia katika mkutano ulioandaliwa na....... chama cha wananchi CUF uliofanyika katika ukumbi wa Goldern Rose jijini arusha wenye lengo la kupanua wigo wa kidemokrasia.
Mh,MaalSelf amesema kuwa vyama vya siasa nchini visiwe sababu ya kuwagombanisha Watanzania bali vishirikiane katika kuwatumikia watanzania ikiwa ni pamoja na kuwashawishi kwa hoja na wala sio kwa fedha.
Ameendelea kwa kusema kuwa Endapo vyama hivyo viatafanya kampeni zisizo sahihi vitasababisha kuvurungika kwa amani ndani ya nchi hatimaye kusababisha sifa mbaya ya jiji la Arusha kuchafuka.
Vilevile amaongeza kuwa vyama vya siasa havikuja kuleta ugomvi bali vilikuwepo ili viweze kuleta amani nchini watu wasiogombane na wakaanza kupigana wao kwa wao hatimae kupoteza amani nchini.
0 comments: