Ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama
Sucrose, Fructose na Glucose na vile vile ina kiasi kingi cha ufumwele
(fibre) ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.
Ndizi
ina uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza
kupata nishati ya kufanyakazi ya muda wa dakika 90 kwa....
kula ndizi mbili
tu.
MFADHAIKO WA AKILI (DEPRESSION)
Kwa mujibu wa utafiti
uliofanywa na Chama Cha Afya ya Akili cha Taifa (MIND) cha nchini
Uingereza, kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili, watu
wengi waliondokana na tatizo hilo na kujisikia vizuri baada ya kula
ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli kwamba ndizi ina kirutubisho
kinachojulikana kama tryptophan, ambacho ni aina fulani ya protini
inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.
MATATIZO WAKATI WA HEDHI (PMS)
Kama
wewe ni miongoni mwa wale akina mama wanaopatwa na matatizo mbalimbali
ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu na unaweza
kuponywa. Vitamin B6 iliyomo kwenye ndizi, hurekebisha kiwango cha
sukari ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.
UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA)
Ndizi
ikiwa ni chanzo kizuri cha madini aina ya chuma (iron), inaweza kuwa ni
dawa ya kuzuia na kuponya upungufu wa damu kwa sababu madini ya chuma
huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.
SHINIKIZO LA DAMU
Tunda
hili ni la aina ya kipekee, lina kiwango kikubwa cha madini ya
potasiamu (potassium) na wakati huo huo lina kiasi kidogo sana cha
chumvi (sodium) hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na
tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.
Ukweli huo, hivi
karibuni umeifanya Mamlaka ya Dawa na Chakula ya nchini Marekani,
iwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza
rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya shinikizo la damu na
kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.
NGUVU YA AKILI
Hivi
karibuni, wanafunzi wapatao 200 wa Shule ya Twickenham nchini
Uingereza, walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi mbivu wakati
wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa mapumziko na wakati wa chakula
cha mchana, ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao. Utafiti unaonesha kuwa
potasiamu iliyojazana kwenye ndizi, ina uwezo wa kumsaidia mwanafunzi
kuamsha uwezo wake wa kujisomea.
MZIO (HANGOVER)
Moja ya dawa
ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangover)
ni kunywa ‘Milkshake’ iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali. Ndizi
hutuliza tumbo, ikisaidiwa na asali, hurejesha kiwango cha sukari
kilichopungua kwenye damu wakati maziwa hutuliza na kurejesha maji
kwenye mfumo wake.
Ndizi pia husaidia katika matatizo mengine kama
vile kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kutuliza vidonda vya
tumbo, kuondoa asidi tumboni, kushusha joto mwilini, kurekebisha mapigo
ya moyo, n.k.
Hivyo ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni bora.
Ukiilinganisha na epo (apple) ndizi ina protini mara nne zaidi, wanga
mara mbili, vitamini A na chuma mara tano, na madini mengine mara mbili
zaidi ya epo.
Mwisho; USIWEKE NDIZI KWENYE JOKOFU!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: