wanamuona kama baba wa taifa lao.
Mandela , rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini, anaugua maradhi ya Mapafu. Mamia ya wananchi walikesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika.
Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu.
Awali mwanawe wa kike,
Makaziwe alisema afya ya babake inaendelea kuwa njema.
Aidha Makaziwe amevikashifu
vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa shujaa huyo
akisema wanahabari wanapaswa kumheshimu babaake.
Rais Jacob Zuma alisema
Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali
mahututi.
"leo angalau yuko sawa
kidogo kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais Zuma baada ya kuongea na
madakatari wanaomtibu Mandela.
Bwana Zuma alifutilia mbali
safari yake ya Msumbiji ili kumtembelea Mandela hospitalini.
Wakati huohuo mwanawe
Mandela Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa anaweza kuhisi mtu
akimgusa.
Chanzo - BBC
Swahili
0 comments: