WANAWAKE wakiwezeshwa kiuchumi na ikiwa ni pamoja na
kupatiwa elimu ya ujasiriamali, kuepuka maradhi hatarishi na kufahamu
haki zao katika jamii hali ya umaskini itapungua kwa kile kipato
kuongezeka katika kundi hili kubwa la Watanzania.
Kauli hiyo imetolewa leo Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Mfuko wa
Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa wakati wa ufunguzi wa
mafunzo ya siku tatu ya wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye
Ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani.
Mama Anna Mkapa ambaye pia ni Mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu,
Benjamin Mkapa alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa
kiuchumi na kijamii wajasiriamali hao kutoka
mikoa yote Tanzania Bara na
Visiwani, ambapo jumla ya wanawake wapatao 264 wanashiriki.
“Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote umekusudia kwa nguvu zake zote
kuendeleza vita ya hii ya kuwawezesha wanawake nchini kujikwamua katika
wimbi la umasikini, maradhi na ujinga,” alisisitiza Mama Mkapa.
Aidha ameiomba Serikali, asasi za kiraia, taasisi za dini na wahisani
binfasi ndani na nje ya nchi, kusaidia wanawke haswa wa
vijijini kujikwamua na umaskini. Mama Mkapa aliongeza kuwa mfuko huo,
kwa kipindi cha miaka 16 zaidi ya wanawake 6,820 wamepata mafunzo ya
stadi za biashara na wengine 4,500 wamepata fursa ya kushiriki maonyesho
mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa kupitia EOTF ili kutangaza na
kuuza bidhaa zao.
Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Abdallah
Kigoda akifungua mafunzo hayo alisema Serikali imeanzisha utaratibu wa
kuweka kumbukumbu za mkopo katika mabenki kwa kupitia ‘Credit Reference
Bureau’ ili kuweza kusaidia kuwafahamu wateja, na kuwaasa wajasiriamali
wanapokopa wakumbuke kulipa kwani uaminifu ni kitu muhimu katika
biashara.
“Suala lingine la kulipa kipaumbele ni lile la kuongeza thamani ya
mazao wanayoyazalisha na tuache kuwazalishia watu wengine bidhaa
wakaenda kuongezea thamani kidogo tu kama vile kwa kufunga na kuweka
nembo ya kibiashara na kuuza kwa bei kubwa,” alisema Dk. Kigoda.
Aliahidi kuwa Wizara yake iko makini kufanya linalowezekana
kushirikiana na wajasiliamali hao kutatua tatizo hilo la kuuza malighafi
badala ya bidhaa iliyoongezwa thamani ili kuongeza ajira na kupunguza
umaskini.
EOTF WANAWAKE WAKIWEZESHWA KIUCHUMI NA WAKIPEWA ELIMU YA UJASILIAMALI WANAWEZA KUTOKOMEZA UMASIKINI
About author: Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: