Bweni moja
la wanafunzi wa kiume katika Shule ya Sekondari Lupata inayomilikiwa na
Jumuiya ya Wazazi Wilayani Rungwe limeteketea kwa kuchomwa moto na
baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakipinga kitendo cha uongozi wa shule
hiyo kuwasimamisha masomo wenzao watatu kwa utovu wa nidhamu. Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman (pichani), jana alisema tukio
hilo lilitokea juzi saa 2:00 usiku, baada ya wanafunzi waliosimamishwa
masomo ku.....wahamasisha wenzao kupinga adhabu hiyo na kufanya vurugu.
Alisema
tukio hilo limesababisha uharibifu mkubwa wa mali za shule hiyo ingawa
moto huo haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu.
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Diwani alisema chanzo ni wanafunzi watatu
wa shule hiyo kusimamishwa masomo utokana na utovu wa nidhamu.
Alisema wanafunzi hao baada ya kusimamishwa masomo walianza
kuwahamasisha wenzao kuwaunga mkono katika kupinga adhabu hiyo, jambo
lililopelekea kufanyika kwa vurugu kubwa shuleni hapo.
Alisema bweni lilichomwa moto lilikuwa ni la wanafunzi zaidi ya 50 ambao
hawakuwa tayari kuwaunga mkono wanafunzi hao, hali iliyosababisha
wenzao kulichoma bweni walilokuwa wakilala.
Kamanda Diwani alisema jumla ya wanafunzi 15 wakiwemo waliokuwa
wamesimamishwa masomo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Rungwe
kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na vurugu hizo.
Alisema tathimini ya uharibifu wa mali bado inaendelea kufanywa ili kujua thamani ya mali iliyoharibiwa na moto huo.
habari NA EMMANUEL LENGWA
CHANZO: NIPASHE
0 comments: