Raia wawili wa Iran wamehukumiwa kifungo cha maisha katika mahakama moja ya Kenya kuhusiana na mashtaka ya ugaidi.Raia hao ni Ahmad Mohammed na Sayed Mousavi
ambao walishtakiwa wiki iliyopita kwa kumiliki..... vilipuzi, ambavyo inaaminika vilikuwa vitumiwe kwa kufanya mashambulizi."mwili unanisisimka nikifikiria hasara ambayo ingesababishwa na
shambulizi hilo la kigaidi," amesema jaji Kiarie Waweru Kiarie, kama
linavyoripoti shirika la habari la AFP.Hata hivyo, serikali ya Iran imekana kuhusika na mpango huyo wa kuishambulia nchi ya Kenya. Siku ya Jumapili, balozi wa Iran nchini Kenya,
Malik Hussein Givzad, amesema ubalozi utasaidia familia za washtakiwa
hao ku......kata rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa. "kama ubalozi, tunachoweza kufanya ni kuzisaidia
familia za washtakiwa kukata rufaa, iwapo mawakili wanahisi kwamba
hakuna ushahidi wa kutosha," amenukuliwa balozi Givzad na gazeti la
Kenya Daily Nation. "nchi ya Iran ina uhusiano mzuri wa kibiashara na Kenya. Huu ulikuwa ni mchakato wa kisheria, tunauheshimu." ameongeza kusema. Mahakama ilibaini kwamba Mohammed na Mousavi
ambao wanahusishwa na mtandao ambao unapanga njama ya kulipua mji wa Nairobi na sehemu ya pwani ya nchi hiyo Mombasa. Jaji Kiarie amesema ameamua kuwafunga maisha kwa
sababu ya vilio vya waathirika wa milipuko iliyopita vilisikika zaidi
kuliko kujitetea kwao, imeripoti AFP. Mawakili kutoka upande wa utetezi wanadai
kwamba, Mohammed na Mousavi walihojiwa na maafisa wa usalama wa Israel
pindi walipokuwa wanashikiliwa. Hata hivyo, upande wa mashtaka umekana tuhuma hizo.
0 comments: