Mkuu wa
jeshi la polisi nchini ameahidi kutoa zawadi nono ya fedha taslim za kitanzania
sh.milioni50 kwa yeyote atakae toa taarifa za kuwafichua wahalifu wengine wa
tukio la mlipuko ulio tokea katika kanisa la Roma lililopo Olasiti.
hayo
yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Liberatus Sabas aliopokua
akiongea na waandishi wa habari juu ya taarifa za kukukamatwa kwa wahalifu
walio......
fikia 13 ambapo wahalifu wa nne wakiwa ni raia wa falme za kiarabu.
Kamanda
Sabas amesema kuwa watuhumiwa 10 kati yao tayari washaojiwa na wanatarajiwa
kufikishwa mahakani mda wowote huku watatu kati yao bsdo wanaojiwa naendapo
upelelezi utakamililka watafikishwa pia mahakamani
Hata hivyo
taarifa zinasema kuwa kabla ya uzinduzi wa kanisa la Romani Katoriki parokia
mpya ya Olasiti ambapo mgeni rasmi alikuwa barozi wa Vatican nchini Askofu
Francisco Padilla alipokuwa anataka kukata utepe wa uzinduzi ndipo mtu mmoja
aliekuwa amejificha kwenye choo kilicho jirani na kanisa hilo umbali wa mita 20
alirusha bomu hilo
Aidha
Kamanda Sabas amefafanua kuwa bomu hilo lilileta madhara kwa watu wapatao 66
ambapo watatu kati yao warifaliki wakiwa kwenye taratibu za matibabu na hivyo
wanatarajiwa kuzikwa kesho May 10 katika kanisa hilo la Olasiti Pamoja na hayo
kamanda amewahakikishia wakazi wa jiji Arusha kuwa ulinzi umeimarishwa
vyakutosha hasa kwenye zile sehemu zenye mikusanyiko mikubwa kama huo
unaotarajiwa kesho kwenye mazishi.
STORI NA
HAZLA QUIRE
0 comments: