Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
anayetarajiwa kuzuru Goma wiki hii alisema ataharakisha mpango wa
kupelekwa kwa wanajeshi wa Umoja wa mataifa katika eneo hilo kujaribu
kusitisha uasi .
Kikosi cha UN kitakachokwenda DRC kupambana na waasi, kitajumuisha wanajeshi kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.
Taarifa zinasema kuwa watu 19 wameuawa na
wengine 27 kujeruhiwa katika mapigano kati ya waasi na wanajeshi wa
serikali mjini Goma DRC.
Mapambano yalikuwa makali kwa siku ya pili huku
katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akitarajiwa kuwasili mjini
humo hapo kesho, kama sehemu ya ziara yake ya eneo hilo.
0 comments: