KUMEKUWAPO na taarifa za kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Simba uliopangwa kufanyika Kesho (Machi 17, 2013) jijini Dar es Salaam kujadili mustakabali wa klabu.
Ikumbukwe kwamba Mkutano Mkuu wa Wanachama ndiyo chombo cha juu kabisa cha maamuzi kwa klabu yetu. Katiba ya Simba SC imeupa Mkutano Mkuu hadhi ya juu mno na ndiyo maana ime.....
weka utaratibu wa kufanyika kwake.
Miongoni mwa utaratibu ni kwamba ni lazima uitishwe na Mwenyekiti aliye madarakani wa klabu. Kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji, ndiye atakayepanga ajenda, mahali na wakati wa kufanyika kwa mkutano wenyewe.
Katika miaka ya nyuma, zilikuwepo nyakati ambapo klabu ilikaa hadi miaka mitatu pasipo kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wowote wa wanachama. Hakuna mwanachama au kikundi chochote
0 comments: