Hatimaye,
baada ya kile kilichoonekana kuwa ni muda mrefu wa kusubiri, dakika takriban 60
zilizoonekana kama masaa mia moja, Kardinali Jorge Mario
Bergoglio kutoka Argentina ndiye kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani.
Kardinali huyo aliyezaliwa.....
Buenos Aires mwaka 1936 anakuwa kiongozi wa 266 wa kanisa hilo ulimwenguni, akichukua mikoba kutoka kwa Papa Benedict XVI aliyestaafu rasmi tarehe 28 Februari, na jina lake la upapa atakuwa Papa Francis wa kwanza. (Francis I)
Buenos Aires mwaka 1936 anakuwa kiongozi wa 266 wa kanisa hilo ulimwenguni, akichukua mikoba kutoka kwa Papa Benedict XVI aliyestaafu rasmi tarehe 28 Februari, na jina lake la upapa atakuwa Papa Francis wa kwanza. (Francis I)
Taarifa kutoka Argentina, zinasema kuwa mpaka hivi sasa wananchi
wameduwaa kwa furaha ya ajabu kwani hawakutegemea kusikia taarifa kama hizi, ni
ajabu na pia ni furaha kwa Amerika yote. GK imefahamu hili kupitia kituo cha TV
cha Al Jazeera.
"Kama mnavyojua,
jukumu la mkutano huu wa Makardinali ilikuwa ni kuwapatia Roma Askofu, na
inavyoonekana kaka na dada zangu wameamua kumchagua mtu kutoka upande
mwingine."
Ni sehemu ya maneno ya kwanza ya Papa Francis, na kisha akaendela kusema.
Na tuanze hii safari ya watu na kanisa la Roma katika undugu, upendo, kuaminiana na kujiamini, tuombe, kwa ajili ya wote, kwa ajili ya dunia nzima, naombea hii safari ya kanisa ambayo inaanza leo na makardinali wangu hapa, iwe ya matunda kwa jiji hili zuri.
Sasa naomba kuwabariki, lakini kabla ya kubariki watu, naomba mniombee kwa Mungu ili anipe baraka zake, naomba tuombe baraka kwa ajili yangu kimoyo moyo (kimyakimya
0 comments: