MAFUNDISHO YA MUNGU NA MTUMISHI WA MUNGU JOSEPHAT .E. MWINGIRA

Photo: Naibariki Jumanne yangu...


DARASA/CHUMBA CHA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
(Darasa linaendelea lilipoishia...)

"KUTAMBUA ADUI ANAYEKUTAFUNA.

Adui mkubwa wa mtu ni yeye mwenyewe.

Mathayo 7:3 “Basi mbona wakitazama kibanzi kilichoko ndani ya jicho la nduguyo, na boriti iliyoko ndani ya jicho lako mwenyewe huliangalii”.

Yer. 1:11 “Tena Neno la Bwana likanijia kusema Yeremia waona nini, nikasema naona ufito wa mlozi (maana yake ni mateso)”. Sasa mtesi mkubwa ni wewe mwenyewe! YESU anasema liangalie hilo boriti jichoni mwako; yakupasa kufahamu kwamba unatakiwa kuyatatua yale yanayokuhusu kabla hujaanza kuyatatua ya mwingine. Tusiwe watu wa kuangalia huku na huku na kusema, “Yule ana dhambi sana, yule ana shida sana”, hebu uwe mtu wa kuangalia ya kwako halafu uone unaweza kutoka mahali kwenda mahali."

(Usikose Darasa Mwana wa MUNGU huu ni Wakati wako, ni Wakati wako wa kupata Furaha na Amani na Ushindi, ni WAKATI WAKO SASA, Usikose, Ni Neema hii imekujilia, Mshukuru BWANA.)

0 comments:

UN YAKANA KUWA NA HATI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

bunge1


WAKATI serikali ikidai kuwa hati halali za Muungano zipo Umoja wa Mataifa (UN), umoja huo umeikana kwa kuweka wazi kuwa hakuna ushahidi wa jambo hilo.
Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima Jumapili kutoka kwa Ofisa wa Masuala ya Sheria na Mikataba wa UN, Andrei Kolomoets, zilibainisha kuwa hakuna ushahidi wa sekretarieti ya umoja huo kuzisajili hati hizo.
Kolomoets alibainisha kuwa kama hati hizo zingekuwa zimesajiliwa na Umoja wa Mataifa kungekuwa na kumbukumbu zake.
Sakata la hati za Muungano liliibuka bungeni wiki iliyopita ambapo wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walionyeshwa hati ya sheria ya kuridhia mkataba wa Muungano zilizokuwa na saini walizodai zimeghushiwa.
Saini za Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Julius Nyerere na aliyekuwa Katibu wa Bunge, Pius Msekwa, zilionekana zina utofauti mkubwa, jambo lililozusha mtafaruku miongoni mwa wajumbe.
Baadhi ya wajumbe walizipinga sheria hizo za hati za Muungano wakidai saini za Nyerere na Msekwa zimeghushiwa, kwa sababu zinatofautiana
zikionekana kufanyiwa utaalamu wa kompyuta.
Mathalani katika hati ya Tanganyika No. 22 ya 1964, herufi mbili za jina la Julius (us) zinatofautiana na herufi nne za mwanzo (Juli) wakati kwenye hati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania No. 18 ya 1965 herufi zote
zimeandikwa kwa ufanano.
Utata mwingine upo kwenye herufi ‘K’ ya jina la katikati la Kambarage, ambapo hati ya mwaka 1964 herufi hiyo inatofautiana na ile ya mwaka 1965.
Hata saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri wakati huo, Pius Msekwa, zinatofautiana kwenye hati hizo, hivyo wajumbe kadhaa kutaka iletwe halisi (original) badala ya nyaraka za sheria zilizoidhinisha Muungano.
Nyaraka hizo za sheria za kuridhia hati za Muungano zimepingwa na wajumbe wengi wa Bunge wakidai zina shaka kutokana na kuridhiwa na upande mmoja wa Bunge la Tanganyika bila Baraza la Mapinduzi kuridhia.
Mkorogano huo ulizidi baada ya Mwenyekiti wa kamati namba mbili inayoongozwa na Shamsi Vuai Nahodha, kudai kuwa aliambiwa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kuwa hati halali za Muungano zipo Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar aliiambia kamati namba mbili kuwa hajawahi kuiona hati ya kisheria ya Zanzibar kuridhia mkataba wa Muungano, ila kwa nafasi yake anaamini ipo.
Nahodha alisema mwanasheria huyo hakuwahi kuitafuta kwakuwa hakukuwa na matatizo ya kimuungano yenye kuhitaji azionyeshe hati hizo.
Vuai alisema hati hizo zilipelekwa Umoja wa Mataifa, kwakuwa kabla ya Muungano uliofanyika Aprili 26, 1964 Tanganyika na Zanzibar kila mmoja alikuwa na kiti cha uwakilishi katika umoja huo.
Alisema kutokana na Muungano huo kulilazimika Tanzania kuwa na kiti kimoja, hivyo hati hizo zilipelekwa Umoja wa Mataifa kuthibitisha Muungano huo.
Maelezo hayo yanaonekana kukinzana na yaliyotolewa na Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Hamis Hamad, aliyesema kuwa hati halali ya Muungano ipo na wanaangalia uwezekano wa kutoa nakala (kopi).
Alisema kopi hiyo itapelekwa mahakamani kwa ajili ya kuidhinishwa kisheria ili ipelekwe kwa wajumbe wa Bunge Maalumu.
Hamad hata hivyo alisema jambo hilo ni lazima walifanye kwa umakini mkubwa, kwakuwa hati hiyo inaweza kupotea.
Msekwa aitwa
Katibu wa zamani Bunge la Jamhuri ya Muungano aliyekuwa mmoja wa watu waliosaini nyaraka za sheria ya kuridhia hati hizo, Pius Msekwa, wiki iliyopita aliitwa kwenye kamati kutoa ufafanuzi ambao hata hivyo ulipingwa na baadhi ya wajumbe.
Pia saini za Msekwa na Rais wa Kwanza wa Tanganyika, Julius Nyerere, kwenye nyaraka hizo zinatofautiana kati ya mwaka 1964 na 1965, hatua iliyowafanya wajumbe kuomba ziletwe hati halisi za Muungano.
Katika ufafanuzi wake kwa wajumbe wa Bunge Maalumu, Msekwa alisema hati ile inasema kutakuwa na serikali ya Tanganyika na Zanzibar pamoja na Bunge la Jamhuri na Baraza la Mapinduzi, hivyo ni serikali mbili.
Kuhusu nyaraka za kisheria za Baraza la Mapinduzi kuridhia hati ya Muungano, Msekwa alisema hajawahi kuziona, bali aliona picha za kikao cha kuridhia suala hilo.
Pia Msekwa alikiri kuwa saini yake na ile ya Nyerere kwenye nyaraka za mwaka 1964 na 1965 ni sahihi, na kwamba hazijaghushiwa kama inavyodaiwa.

0 comments:

KAMATI 10 BUNGE MAALUMU ZAITOA JASHO CCM


Dodoma. Kura za awali katika Kamati 10 kati ya 12 za Bunge Maalumu la Katiba, zinakipa wakati mgumu Chama Cha Mapinduzi,(CCM) kutekeleza azma yake inayotajwa kuwa ni kufumua Rasimu ya Katiba, ili kuondoa mapendekezo ya Muundo wa serikali tatu, baada ya wajumbe wa Zanzibar kukwamisha upatikanaji theluthi mbili.
Kwa mujibu wa taarifa za kamati, ambazo tangu juzi zimeanza kutolewa katika sura ya kwanza na sita zinazungumzia Muundo wa Muungano, wajumbe kutoka Zanzibar kwa sasa ndiyo kikwazo kikubwa kwa CCM.
Hata hivyo, uamuzi ya mwisho kuhusu Muundo wa Serikali, kati ya mbili au tatu, unatarajiwa kujulikana Alhamisi wiki ijayo, wakati kamati zote zitakapowasilisha taarifa zao na kupigwa tena kura kwa wajumbe Tanzania Bara peke yao na Zanzibar peke yao.
Iwapo wajumbe wa Zanzibar wakiitetea kwa theluthi mbili kama sasa, mapendekezo ya muundo wa serikali tatu ndiyo yatakayopelekwa kwa wananchi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wenyeviti wa kamati hizo, Stephen Wassira, Ummy Mwalimu, Anna Abdalah na Paul Kimili, walitaja moja ya vifungu ambavyo vimeshindwa kupata theluthi mbili kuwa ni ibara ya kwanza kifungu cha kwanza.
Akizungumza jana Wassira ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Namba Sita alisema kwamba katika kamati yake ibara hiyo imeshindwa kupata theluthi mbili, ili kuweza kufanyiwa marekebisho.
“Lakini huu siyo mwisho kama nilivyosema awali, tukirudi bungeni tutapiga kura kwa wajumbe wote na ndiyo itakuwa na uamuzi wa mwisho kama muundo wa Muungano utakuwa na Serikali tatu ama mbili, ambao utapelekwa kwa wananchi,” alisema Wassira.
Jussa, Lissu- tumeibana CCM
Jussa alisema: “Kwa taarifa za matokeo tulizonazo katika Kamati Namba 1, 2, 3, 4, 6, 10, 11 na 12 mapendekezo ya kubadilisha Rasimu katika ibara hizo mbili yamekwama. Kama CCM wakichakachua sura ya kwanza na sita, maana yake ni kwamba hapa hakuna Katiba, hakuna kura ya maoni na hakuna mwafaka.”
Vifungu hivi pia kwa mujibu wa wenyeviti wa kamati nyingine, isipokuwa kamati ya Tano, ambayo inaongozwa na Hamad Rashid, havikupata kura theluthi mbili na hivyo kubaki kama vilivyo kwenye rasimu.
Naye Lissu alisema kwa sasa CCM ndiyo inaweza kuanza mkakati wa kuvuruga Bunge kwani tayari wamejua hawana theluthi mbili ya Zanzibar ili kubadili Rasimu kama wanavyotaka.

0 comments:

MATUMAINI YA KATIBA MPYA SASA YAWA NDOTO KWA TAIFA


Ikulu imeeleza kuwa imeshindwa kutimiza ahadi yake kwa taifa ya kulipatia Katiba Mpya ifikapo Aprili 26, 2014.
Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue alilieleza gazeti hili kuwa kwa hali ya mchakato huo ilivyo sasa, wameshindwa kufikia lengo hilo, lakini hawajakata tamaa kuhusu kupatikana Katiba Mpya ndani ya mwaka huu.
“Kweli matarajio ya awali yalikuwa hayo, lakini kama unavyoona hali ilivyo, ni vigumu kusema matarajio mengine, ingawa majadiliano yaliyofanywa mwaka huu ni lazima Katiba inayopendekezwa iwasilishwe kwa wananchi na mwakani tutakuwa na Katiba Mpya,” alieleza Balozi Sefue.
Katika hali isiyoeleweka Balozi Sefue alisisitiza msimamo wa awali wa Serikali kwamba Katiba itakayopatikana itatumika kwenye Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.
Dk Slaa
Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), Dk. Willbroad Slaa, alisema hilo ni fundisho kwa Serikali kwamba kiburi na jeuri havitakiwi katika masuala yanayohusu umma.
Alisema muda huo wa kupatikana Katiba Mpya ulipotangazwa, walioanzisha kilio cha kudai Katiba Mpya nchini ambao aliwataja kuwa ni vyama vya upinzani vya siasa, taasisi mbalimbali za kijamii walipinga na kutoa ushauri kwa Serikali, lakini walipuuzwa.
Dk. Slaa alisema walipendekeza kwamba badala ya kupeleka mchakato wa Katiba mchakamchaka, warekebishe kwa mara ya 15 Katiba inayotumika, ili iende na wakati wa sasa ikiwamo Uchaguzi Mkuu ujao kwa lengo la kutoa muda wa kutosha kwa mchakato wa taifa kupata Katiba Mpya.
“Lakini walitukebehi na kututukana sana, sasa kiko wapi Aprili 26 hiyo hapo na Katiba haijapatikana na kusema itapatikana mwaka huu na kutumika kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani ni ndoto za mchana,” alieleza Dk. Slaa.
Dk. Slaa alisema tukio hilo liwe fundisho kwa Serikali, wawe wakweli, wanyoofu na wafahamu kuwa nje ya Serikali kuna watu makini na wanaojua vilivyo mchakato wa Katiba.
Alisema ana taarifa za Bunge Maalumu kuahirishwa Mei 9, 2014 ili kupisha Bunge la Bajeti. Hivyo mategemeo ya Katiba Mpya kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, yanatia shaka.
“Kwa akili ya kawaida tu isiyohitaji elimu ya chuo chochote, kutumia Katiba Mpya kwenye Uchaguzi Mkuu ujao ni jambo lisilowezekana kwa hiyo waache kutuletea matumaini yasiyokuwapo, sisi siyo watoto wadogo,” alieleza Dk. Slaa.

0 comments:

CHELSEA, MANCITY NA LIVERPOOL ZAWANIA UBINGWA WA ENGLAND.

Fußball Premier League Chelsea Arsenal


Manchester City watajaribu kuwauwa ndege wawili kwa kutumia jiwe moja, wakati watakapojaribu wikendi hii kuwaongezea joto viongozi wa ligi Chelsea na pia kuyauwa matumaini ya Arsenal kutwaa ubingwa.
Ushindi wa City wa magoli matatu kwa sifuri dhidi ya Manchester United uliwaongeza karibu na Chelsea kwa pengo la points tatu huku wakiwa na mechi mbili za kucheza. Arsenal wako nyuma ya vijana wa Pelkegrini wakiwa na pengo la points tatu, lakini wamecheza mechi mbili zaidi na hawatataka kushindwa wakati timu hizo mbili zitakapokutana leo uwanjani Emirates.
Huku Liverpool wakisubiri hadi kesho Jumapili, wakati watakapowaalika nambari sita Tottenham Hotspurs, Cheslea watakuwa na fursa ya kupanua uongozi wao na points nne wakati watakapocheza ugenini dhidi ya Crystal Palace leo Jumamosi.
La liga
Nchini Uhispania ambapo pia kinyang‘anyiro cha taji kimepamba moto..Atletico Madrid wanakabiliwa na kibarua kigumu ugenini dhidi ya Athletic Bilbao leo Jumamosi katika juhudi zao za kutaka kusalia juu ya miamba Barcelona na Real Madrid.
Mara ya mwisho ambapo timu ambayo siyo Barcelona au Real Madrid imewahi kushinda La liga ni mwaka wa 2004 wakati Rafa Benitez aliwaongoza Valencia kutwaa uchampion. Na ni mwaka wa 2008 ambapo timu tofauti iliweza kumaliza msimu katika nafasi ya pili, na timu hiyo ilikuwa Villareal yake Manuel Pellegrini kwa wakati huo. Atletico wako mbele ya Barca na faida ya point moja na tatu mbele ya Real, wakati kukisalia mechi nane msimu kukamilika.
Barcelona pia watakuwa leo na mchuano mkali wa ugenini dhidi ya Espanyol. Real Madrid wanacheza leo dhidi ya mahasimu wao wa nyumbani Rayo Vallecano.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters

0 comments:

NYOTA WAKIKIE ANAETIKISA ULIMWENGU WA SOKA

 Doreen Nabwire Omondi


Ni wachezaji wanaume tu kutoka barani Afrika wanaopata nafasi nyingi katika ligi za Ulaya. Lakini kwake Doreen Nabwire Omondi, mpira wa miguu siyo tu mchezo wa wanaume pekee, bali pia wanawake wanaweza kutamba
Bruce Amani alimtembelea Doreen Nabwire katika uwanja wa Geißbockheim, viungani mwa mji wa Cologne, ambako alikutuna naye wakati akifanya mazoezi na wenzake, na kutokana na hadithi yake, Doreen siyo tu nyota ndani na nje ya uwanja wa michezo, bali ni kielelezo kwa wasichana wengi nchini Kenya.
Ni mwendo wa saa moja jioni, katika uwanja wa Geißbockheim, viungani mwa mji wa Köln Ujerumani, ambako ndio makao ya timu za vijana na za wanawake za FC Köln. Doreen Nabwire Omondi pamoja na wachezaji wenzake wanamalizia mazoezi yao ya leo kabla ya mchuano wa kirafiki mwishoni mwa wiki na timu ya Duisburg.
Baada ya kocha wake kupuliza kipyenga cha kukamilisha mazoezi, nilipata fursa ya kukutana na mshambuliaji huyo ambaye ndiye mchezaji pekee mweusi kutoka barani Afrika anayechezea klabu hiyo ya ligi ya daraja ya pili ya Bundesliga. Doreen Nabwire Omondi, mwenye umri wa miaka 26 anasema safari yake kwa hakika imekuwa na panda shuka nyingi tangu alipoanza kuichezea klabu ya Mathare Youths nchini Kenya.
Mwandishi wa habari wa DW Bruce Amani akimzungumza na Doreen Nabwire Mwandishi wa habari wa DW Bruce Amani akimzungumza na Doreen Nabwire
Doreen ambaye ni mama wa mtoto mmoja, alizaliwa katika mtaa wa mabanda wa Korogocho, eneo la Mathare jijini Nairobi, ambako ukimtajia yeyote neno mtaa wa mabanda, kitu kinachomjia akilini kwanza ni masuala kama vile ukosefu wa usalama, kiwango kikubwa cha uhalifu, vijana kujihusisha na dawa za kulevya, miongoni mwa mengine mengi. Hivi vyote Doreen anasema havikuweza kumfanya kushindwa kuendelea kuota ndoto yake ya kuimarisha taaluma yake ya kuwa mwanasoka shupavu.
kando na kuwa nyota ndani ya uwanja, pia ni kielelezo nje ya uwanja. Changamoto zinazowakabili wasichana katika jamii, na hasa wanaoishi katika mitaa ya mabanda, zilimwezesha kuanzisha kikundi kinachofahamika kama GirlsUnlimited, ambacho kinawahamasisha vijana kuhusu namna ya kukuza vipaji vyao na kupitia michezo.
Doreen anahoji kwamba bado hawahi kupata jibu la ni kwa nini soka la wanawake halina umaarufu namna ilivyo michezo mingine ambayo inawapa wanaume na wanawake nafasi sawa za kutamba viwanjani na kuuonesha mashabiki na ulimwengu mzima vipaji walivyo navyo.
Wakati akiwa nchini Uholanzi, kando na kuwa alikuwa anaichezea klabu ya Zwolle, pia alipewa mafunzo ya kuwa mkufunzi wa soka, na akahitimu na shahada ya Diploma. Na sasa anasema kitu ambacho anataka kukifanya wakati atakapozitundika njumu, ni kurudi nchini Kenya, na kuanzisha shule ya kutoa mafunzo ya soka la wanawake, ili kuwapa nao wasichana wengine fursa ya kujiimarisha kama wachezaji nyota, ambao watakuwa maarufu hata kumliko.
Kando na kuwa mchezaji wa FC Köln, yeye pia hufanya kazi na Shirika moja la kijamii mjini Köln linalofahamika kama RheineFlanke, katika kitengo cha kuwahamasisha vijana kuhusu michezo na mabadiliko ya kijamii na maendeleo, kupitia warsha mbalimbali.
Mwandishi: Bruce Amani

0 comments:

JUHUDI ZA AMANI YA MASHARIKI YA KATI ZA SHIKA KAZI

 


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry amemaliza ziara ya masaa karibu 16 mashariki ya kati bila ya kukutana na kiongozi wa mamlaka ya utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry amekutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa mara ya pili hii leo baada ya kupita masaa 12-ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuyanusuru mazungumzo kati ya Israel na Palastina yasivunjike.
Jana John Kerry alisitisha ziara yake ya Ulaya na kwenda Jerusalem ambako alikutana kwa muda mrefu kwanza na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na baadae na mkuu wa tume ya Palastina katika mazungumzo ya amani Saeb Erakat baada ya mazungumzo pamoja na Mahmoud Abbas kuakhirishwa jana usiku.
Baada ya duru ya pili ya mazungumzo leo asubuhi pamoja na Netanyahu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ameondoka na kwenda Brussels kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa jumuia ya kujihami ya NATO kuhusu Ukraine na Afghanistan.
Maafisa wa kipalastina wanasema hata hivyo waziri Kerry huenda akarejea katika eneo hilo kesho ili kukutana na kiongozi wa utawala wa ndani Mahmoud Abbas.
Kila upande unataka hakikisho
Wakuu wa tume za Israel na Palastina katika mazungumzo ya amani:Tzipi Livni (kushoto) na Saeb Erakat
Jana wapalastina wameitaka Marekani iwape hakikisho la kuachiliwa huru kundi la tatu na la mwisho la wafungwa wa kipalastina waliokuwa waachiwe huru Marchi 29 iliyopita.Israel inapinga kuwaachia huru ikitaka ipatiwe hakikisho na wapalastina kwamba hawataondoka katika meza ya mazungumzo wafungwa hao wakiachiwa huru.
Duru za kuaminika zinasema Marekani inafikiria uwezekano wa kumuachia huru jasusi Jonathan Pollard anaeshikiliwa Marekani ili kuyanusuru mazungumzo ya amani.
Jana usiku uongozi wa wapalastina ulikutana Ramallah,akihudhuria pia Mahmoud Abbas na kutishia kuendelea na juhudi za kujiunga na mashirika ya Umoja wa mataifa ikiwa hawatapatiwa hakikisho la kuachiwa huru wapalastina hao katika kipindi cha masaa 24 yanayokuja.Wamepinga pia fikra ya kurefushwa mazungumzo ya amani,baada ya Aprili 29 bila ya kwanza Israel kusitisha ujenzi wa makaazi ya wahamiaji wa kiyahudi katika ukingo wa magharibi wa mto Jordan na katika sehemu ya mashariki ya Jerusalem.Zaidi ya hayo wapalastina wanataka wafungwa elfu moja ziada wa kipalastina akiwemo Marwan Barghouti na Ahmad Saadat waachiwe huru.Israel lakini inasemekana inapendekeza kuwaachia huru wafungwa 420, kufungua njia ya mpakani kati ya Ukingo wa magharibi na Jordan na kuruhusu kuishi pamoja familia.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir:Reuters/DPA/AFP

0 comments:

ISRAEL YAGOMA KUWAACHIA HURU WAFUNGWA WA KIPALESTINA

 


Israel imeufuta mpango wa kuawachia wafungwa wa kipalestina na kudidimiza zaidi matumaini ya kufanikiwa kwa mchakato wa kutafuta amani Mashariki ya kati huku Israel na Palestina zikichukua misimamo mikali
Waziri wa sheria wa Israel ambaye pia ndiye mpatanishi mkuu wa nchi yake Tzipi Livni, hapo jana amewaambia wajumbe wa Palestina wa mchakato wa kutafuta amani kuwa Israel haiwezi kuwaachia huru wafungwa 26 kwa sababu Palesetina imeamua kuanza harakati za kutambulika zaidi kimataifa.
Duru zinasema Israel inaichukulia hatua hiyo ya Palestina kama kinyume na makubaliano ya awali ambapo Palestina ilikuwa imeahidi haitaendeleza kampeini zake za kutaka kutambulika kama taifa huru na kujiunga na mashirika na mikataba ya kimataifa inayotambulika na Umoja wa Mataifa.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha pande hizo mbili zinasalia katika meza ya mazungumzo, amewataka wanasiasa wa Israel na Palestina kuonyesha ukomavu na muelekeo wa uongozi katika kushughulikia mchakato huo wa kutafuta amani.
Israel na Palestina zavutana
Mazungumzo hayo yalikwama mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Israel kukataa kuwaachia huru wafungwa wa kipalestina siku ya Jumamosi kama ilivyokuwa imetarajiwa na kuighadhabisha Palestina ambayo Rais wake Mahmoud Abbas aliwasilisha maombi ya kutaka nchi hiyo kujiunga na mashirika ya kimataifa takriban 15 yanayotambuliwa na Umoja wa Mataifa.
Rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahmoud Abbas Rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahmoud Abbas
Livni ameitaka Palestina kufutilia mbali uwasilishwaji huo wa kutambulika kimataifa na kurejea mara moja katika meza ya mazungumzo lakini Palestina imesisitiza kuwa haitafanya hivyo hadi kuwe na marekebisho katika makubaliano yaliyofikiwa awali na Israel ambayo inaishutumu kwa kugeuka na kutoheshimu mikataba.
Msemaji wa ikulu ya Rais wa Marekani Jay Carney amesema uamuzi wa Israel wa kutowaachia huru wafungwa wa kipalestina unaibua changamoto na kuzorotesha juhudi za kupatikana ufumbuzi katika mzozo huo wa muda mrefu wa mashariki ya kati:
Hata hivyo Carney amesema Kerry na kundi la wajumbe wa Marekani wanaoshiriki katika mchakato huo hawatakatishwa tamaa na changamoto hizo na watajaribu kuhakikisha pande zote mbili zinaendelea kushiriki katika mazungumzo.
Marekani yasikitishwa na hatua za pande zote mbili
Kerry ambaye amekua katika pilika pilika za juu chini kwa takriban mwaka mzima kushughulikia mchakato huo wa kupatikana amani amewapigia simu waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Palestina Abbas lakini yaliyojadiliwa hayajawekwa wazi.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry
Huku hayo yakijiri,wapalestina katika ukanda wa Gaza wamefyatua makombora manne kusini mwa Israel na kujibiwa mara moja kwa mashambulizi ya angani kutoka Israel.
Msemaji wa jeshi la Israel amesema hakuna aliyejeruhiwa katika majibizano hayo ya leo.Maafisa wa usalama wa Palestina wamethibitisha kuwa Israel imelishambulia eneo la Gaza leo ikilenga vituo sita vya kundi la Hamas tawi la kijeshi katika mji wa Gaza.
Mwandishi:Caro Robi/AFP

0 comments:

VIONGOZI WA KUNDI LA M23 KUFIKISHWA ICC

  Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uganda Henry Okello Oryem
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje ,wa Uganda Henry Okello Oryem, amesema huenda baadhi ya viongozi wa waasi wa M23, wakafikishwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu dhidi ya binaadamu.
Grace Kabogo amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Uganda, Ali Mutasa, ambapo kwanza alitaka kujua iwapo hatua hiyo inatokana na shinikizo lolote kutoka nje, hasa ikizingatiwa kuwa waasi wa M23 walikimbilia Uganda kwa usalama wao, nchi ambayo imekuwa ikidaiwa kuwasaidia waasi hao.
Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Grace Patricia Kabogo
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

0 comments:

MPIGA PICHA ANJA NIEDRINGHAUS AUAWA AFIGHANISTAN

Mpiga picha raia wa Ujerumani aliyeuwawa Afghanistan, Anja Niedringhaus Niedringhaus


Polisi nchini Afghanistan imesema mwandishi habari wa kike kutoka nchi za Magharibi ameuwawa kwa kupigwa risasi mkoani Khost huku mwengine akijeruhiwa vibaya siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo.
Mpiga picha raia wa Ujerumani aliyeuwawa Afghanistan, Anja Niedringhaus
Msemaji wa polisi katika mkoa wa Khost,Mobarez Mohammad Zadran aliliambia shirika la habari la AFP kwamba waandishi hao wawili Mpiga picha Anja Niedringhaus na muandishi Kathy Gannon walipigwa risasi leo asubuhi ndani ya makao makuu ya polisi ya wilaya na kwamba mmoja amejeruhiwa vibaya.
Zadran pamoja na naibu mkuu wa polisi wa eneo hilo Yaqub Mandozai wamesema waliofanya shambulizi hilo walikuwa wamevalia sare za polisi.
Huyu ni mwandishi habari wa pili kutoka nchi za Magharibi kuuwawa nchini Afghanistan wakati wa kampeni za uchaguzi baada ya mwandishi mwengine kutoka Sweden; Nils Horner kuuwawa kwa kupigwa risasi mjini Kabul mnamo Machi 11.
Rais wa Afghanistan anayeondoka Hamid Karzai Rais wa Afghanistan anayeondoka Hamid Karzai
Mauaji mengine nchini Afghanistan ni ya mwandishi mkuu wa chombo cha habari cha AFP raia wa Afghanistan Sardar Ahmad, Mke wake na watoto wake wawili waliouwawa tarehe 20 mwezi Machi wakati watu waliokuwa na bunduki walipovamia hoteli ya Serena, kuwapiga risasi na kuwauwa watu tisa wakiwemo raia wanne wa kigeni.
Mkoa wa Khost unaopakana na eneo lililo na utata la Kaskazini mwa Waziristan linadhibitiwa na wapiganaji wa Haqqani wanaoshutumia kwa mashambulizi mengi makubwa nchini Afghanistan.
Mtandao wa wapiganaji hao umekuwa ukiwalenga raia wa kigeni. Kabul imetikiswa na mashambulizi makubwa wakati huu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo kesho. Uchaguzi huu ni wa kihistoria kwa kuwa ni wa kwanza utakaobadilisha madaraka kwa njia ya kidemokrasia.
Ulinzi wazidi kuimarishwa Afghanistan siku moja kabla ya uchaguzi
Aidha ulinzi umezidi kuimarishwa nchini Afghanistan kufuatia uchaguzi huo wa urais kumchagua atakayechukua kiti cha uongozi kutoka kwa rais anayeondoka Hamid Karzai, anayebanwa na katiba ya nchi hiyo kugombea tenawadhifa huo.
Kulingana na waziri wa mambo ya ndani nchini humo Omar Daudzai zaidi ya maafisa wa usalama takriban 400,000 wakiwemo polisi, majeshi, na majasusi wamewekwa kote nchini humo kuimarisha ulinzi.
Hata hivyo waasi wa Taliban wameapa kuvuruga uchaguzi huo kwa ghasia na kuwahimiza wapiganaji wao kuwalenga maafisa wa uchaguzi, wapiga kura na maafisa wa usalama.
Maafisa wa Usalama Afghanistan Maafisa wa Usalama Afghanistan
Licha ya hayo hapo jana rais Hamid Karzai amewahimiza wapiga kura kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa kesho.
Mchumi na mfanyakazi wa zamani wa benki ya dunia Ashraf Ghani, Abdullah Abdullah aliyejitosa katika uchaguzi wa mwaka wa 2009 pamoja na aliyekuwa waziri wa nchi za kigeni Zalmai Rassoul ni miongoni mwa wagombea 9 wanaowania kukalia kiti cha urais nchini Afghanistan.
Atakayeshinda uchaguzi na kuchukua nafasi ya Karzai atakabiliwa na kipindi kigumu cha kuiweka nchi hiyo dhabiti wakati wanajeshi wa Afghanistan wakipambana na wapiganaji wa Taliban bila ya usaidizi wa wanajeshi wa Jumuiya ya kujihami NATO. Muungano huo unaoongozwa na Marekani unatarajiwa kuondoa wanajeshi wake 53,000 nchini Afghanistan mwishoni mwa mwaka huu.
Mwandishi:Amina Abubakar/AFP

0 comments:

WALIOTUMWA KUILIPUA URUSI WAKAMATWA



Kitengo cha kimataifa cha upelelezi Nchini Urusi FSB, kinasema kuwa kimewazuilia raia 25 wa Ukraine, kikiwalaumu kwa kupanga mashambulio ya kigaidi mwezi uliopita wakati jimbo la
Crimea lililoko Ukraine lilipokuwa likiandaa kura ya maoni.

0 comments:

WATATU WAHUKUMIWA KIFO KWA UBAKAJI NCHINI INDIA

 
Wanaume watatu wamehukumiwa kifo Mjini Mumbai, India baada ya kupatikana na hatia katika visa tofauti vya ubakaji walioufanya kwa pamoja.
Moja ya visa hivyo kilitokea dhidi ya mwandishi mpiga picha aliyekuwa kazini alipobakwa.
Uamuzi huo umefanywa chini ya sheria mpya iliyopitishwa ya kuwaadhibibu wanaoendeleza uhalifu huo wa ubakaji. Sheria hiyo ilipitishwa baada ya kile kisa Delhi kilichoughadhabisha umma cha msichana aliyebakwa na ngege basini na kujeruhiwa vibaya sana.
Wanaume hao walikuwa wameshitakiwa kwa kesi ya kumbaka msichana huyo mwandishi aliyekuwa ameenda kupiga picha kiwanda cha nguo kilichotelekezwa, lakini pia mwanamke mwengine akajitokeza na kutoa ushahidi wa jinsi wanaume hao walivyombaka maeneo hayo hayo mwezi mmoja kabla.
Wahukumiwa hao wanaweza kukata rufaa kwa mahakama ya juu zaidi.
Kuongezaka kwa visa vya ubakaji vimepelekea maaandamano ya mara kwa mara nchini humo na sasa mahakama zinaharakisha kusikilizwa kwa kesi hizo.
Pia limekuwa swala la mijadala mikali katika kampeni za uchaguzi unatajariwa hivi karibuni nchini humo.

0 comments:

BIG RESULTS NOW' KUFANIKISHA UBIA KATI YA SEKTA BINAFSI NA ZA UMMA

  Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, hivi karibuni. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now). Picha na Sufianimafoto.com
******************************
 Na Mwandishi Wetu
Serikali inalenga kushirikiana na sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya kimkakati yenye thamani ya shilingi trioni 6 hadi kufikia mwaka 2015/16 ikiwa ni sehemu ya ukamilishwaji wa mkakati wa “Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa” yaani Big Results Now (BRN), utaratibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo makubwa kwa muda mfupi. 

Katika mkuitano wake na wamiliki wa magazeti tando, msemaji mkuu wa wizara ya Fedha, Bi Ingiahedi Mduma alibainisha kuwa kuna vyanzo vingi vya fedha ambavyo wizara yake imedhamiria kuvitumia lakini kwa hii ambayo wanatarajia kushirikisha sekta binafsi ipo miradi mitatu mikuu ambayo inatarajiwa kutoa muongozo.


Bi mduma aliitaja miradi hiyo ya awali kuanza kutekelezwa kwa ubia ni ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam hadi Chalinze, uendeshaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, na ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi III. 



Amesema ukiachana na miradi hii, Wizara ya Fedha inaendelea kutekeleza jukumu la kutafuta na kutoa fedha za kugharamia shughuli za BRN zilizoibuliwa katika maabara zote sita za Elimu, Maji, Kilimo, Uchukuzi, Nishati na utafutaji na mapato ya serikali.


Bi Mduma ameelezea pia kwamba katika kipindi cha Julai hadi Disemba, 2013 Wizara ya Fedha imefanikiwa kutekeleza kiashiria hiki kwa kutoa fedha za maendeleo za ndani kwenye Wizara zinazotekeleza shughuli za BRN.

Amesema jumla ya shilingi Bilioni 590.5 zimetolewa katika kuhakikisha kwamba maabara hizi zinaweza kujitegemea katika miradi yake.

Akitaja viwango nvya fedha ambavyo wizara imetoa, Bi Mduma alisema miradi ya Elimu imepewa jumla ya shilingi bilioni 8.3, Miradi ya Maji imepewa shilingi bilioni 86.0, Miradi ya Kilimo shilingi bilioni 10.2, Miradi ya Uchukuzi shilingi bilioni 146.6 na Miradi ya Nishati imepewa jumla ya shilingi bilioni 339.4.

0 comments:

WANAOKUBALI SERIKALI TATU WANAKWEPA UNAFIKI, KANGI LUGOLA



Mjumbe wa Bunge la Katiba Kangi Lugola, ametaja msimamo wake wa kuunga mkono serikali tatu kwamba ni kukwepa unafiki.
Lugola, ambaye alisema kwenye kikao cha Bunge la Katiba kuwa atakuwa wa mwisho kuisaliti Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema kinachowasumbua wanasiasa wengi ni suala la unafiki ambalo ameapa hatakuwa tayari kulisujudia.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu msimamo wake unaopingana na chama chake cha CCM, alisema wanaounga mkono miongozo ya vyama kwenye Bunge la Katiba, wanafanya hivyo kwa unafiki na hofu ya kisiasa.
 Alisema kitendo cha kupinga Rasimu ya Pili ya Katiba ambayo iliwasilishwa na  mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba, ni sawa na kupinga mawazo ya wananchi.
“Tumetumia fedha nyingi kwa ajili ya Tume ya Jaji Warioba kukusanya maoni ya wananchi na alichokileta bungeni ni matakwa ya Watanzania. Leo hii tunaanza kuchakachua kile ambacho alikifanyia kazi kwa uaminifu mkubwa?” alihoji Lugola.
Alisema hawezi kukubaliana na dhambi ya unafiki. “Nawataka wana-CCM wenzangu muweze kupima mambo badala ya kuburutwa,” alisema.
Kuhusu muundo wa Muungano, alisema hata sasa hakuna Muungano kwani Zanzibar imeshajitangazia mamlaka yake.
“Kama wanataka kurudisha Muungano, Serikali ya Zanzibar inatakiwa ivunjwe ili ieleweke kuwa hakuna Tanganyika na hakuna Zanzibar. Sasa hakuna lolote ambalo linaweza kunishawishi kuwa kuna Muungano,” alisema Lugola.
“Muundo wa be huyo alisema kuwa serikali tatu unawezekana na tayari upo unafanya kazi, lakini ukiwa katika kivuli cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema ambaye wiki iliyopita aliwatahadharisha wajumbe wenzake dhidi ya hatari kwa wengi kuwaburuza wachache.

0 comments:

LORI LA MAFUTA LALIPUKA DAR WAWILI WAJERUHIWA


Taharuki ya aina yake ilitokea jana eneo la Tabata Relini kwenye yadi ya malori ya Kampuni ya Oilcom baada ya kutokea kishindo kikubwa kilichotokana na kupasuka kwa tanki la mafuta.
Tukio hilo lililotokea saa 11 jioni, lilizua hofu miongoni mwa wakazi na wafanyakazi wa eneo hilo, na lilitokana na hitilafu ya kiufundi wakati wa kulitengeneza tanki hilo.
Mashuhuda wa tukio hilo lililojeruhi watu watatu waliliambia Mwananchi kuwa mlipuko huo ulitokea wakati fundi akichomea sehemu ya tanki katika karakana ya magari ya kampuni hiyo.
“Kuna fundi alikuwa juu ya lori akipima mifuniko na chini alikuwepo dereva wa lori hilo na fundi mwingine wa kuchomea vyuma akichomea, wote walikuwa wakiendelea na kazi.
“Dereva wa lori hilo alikuwa akimuelekeza fundi sehemu ya kuchomea na ghafla ukatokea mlipuko mkubwa,” alisema Omari Wenge, fundi katika karakana hiyo.
Alisema mlipuko huo ulimtupa chini fundi aliyekuwa juu ya tanki na kulikosababisha aumie usoni na sehemu za kifuani.
Shuhuda huyo alisema dereva na fundi wa kuchomea, waliumizwa sehemu mbalimbali za mwili kwa kupigwa na vipande vya mabati ya tanki na kichwa cha gari hilo.
Majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu zaidi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Camillus Wambura alisema kuwa hakuwa amepata taarifa zozote za ajali hiyo hivyo angetujulisha pindi angezipata.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa karakana hiyo wakipewa huduma ya kwanza baada ya kuzimia kwa mshtuko huku wengine wakiweweseka kwa hofu.
Kichwa cha lori hilo kilichakazwa na mlipuko huo ambao moja ya mabati yanayoligawa tanki hilo yalitupwa upande wa pili wa Barabara ya Mandela.
Sehemu ya juu ya mbele ya lori hilo, ilitupwa juu ya paa la moja ya majengo ya karakana hiyo huku chini zikiwa zimetapakaa nyaraka na mabaki mengine ya sehemu ya mbele ya lori hilo.
Naye mmoja wa mashuhuda, Boniface Msisi aliyekuwemo ndani ya karakana hiyo, alisema hali ndani ya eneo hilo ilibadilika ghafla huku kila mfanyakazi akitafuta mlango wa kutokea.

0 comments:

TIMU YA JAJI WARIOBA YATUPIWA VIRAGO NJEE

 

Tumeisoma kwa umakini mkubwa taarifa iliyotolewa juzi na Ikulu, ikikanusha madai ya mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kwamba Ikulu imeitupia virago Tume hiyo. Tumejaribu kuisoma taarifa hiyo ya Ikulu tena na tena, aya kwa aya, mstari kwa mstari na neno kwa neno. Lakini kadiri tulivyozidi kufanya hivyo ndivyo tulivyozidi kugundua kuwa ni dhahiri Tume hiyo, siyo tu ilitupiwa virago, bali pia ilidhalilishwa na kufadhaishwa kutokana na lugha ya kejeli na masimango iliyokuwa katika taarifa hiyo ya Ikulu.
Jaji Warioba alikaririwa akilalamikia jinsi yeye na makamishna wa Tume walivyoondolewa ofisini na kunyang’anywa magari kwa namna ambayo iliwadhalilisha, kwani licha ya hatua hiyo kuchukuliwa kwa haraka bila kusubiri siku ambayo Tume ilikuwa imepanga kufanya makabidhiano, Serikali haikutaka kujipa muda wa kufanya maandalizi ya kuwarudisha wajumbe makwao.
Katika kuhalalisha hatua hiyo ya Serikali, taarifa ya Ikulu ilijikita zaidi katika kifungu cha 31(1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kinachoelekeza kwamba shughuli za Tume zingekoma rasmi baada ya mwenyekiti wake kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge la Katiba. Ikulu ilisema katika taarifa hiyo kwamba Jaji Warioba aliwasilisha Rasimu hiyo bungeni Machi 18 na siku iliyofuata Rais alitia saini tangazo la kuvunja Tume hiyo kwa mujibu wa sheria, hivyo ilishangazwa na kitendo cha mtu “kujitia amesahau siku hiyo kwani hicho ni kiwango cha juu sana cha unafiki”.
Hata hivyo, jambo linalomtatiza Jaji Warioba na wenzake ni uharaka wa Serikali kuivunja Tume hiyo wakati ikijua kwamba Tume ilikuwa haijamaliza kazi yake wakati ilipokabidhi Rasimu hiyo kwa Rais. Jaji Warioba anasema Serikali ilikuwa ikijua kwamba Tume ilikuwa ikiendelea na kazi ya kuandaa Randama ya Rasimu, Bango Kitita la Rasimu pamoja na maelezo aliyoyatoa wakati wa kuwasilisha Rasimu kwenye Bunge la Katiba.
Lakini pia Jaji Warioba anasema kuwa hata kama sheria ilitaja muda wa kuvunja Tume hiyo, bado Serikali ilikuwa na wajibu wa kuhakikisha inavunjwa katika mazingira yanayokubalika kama zilivyovunjwa tume zote zilizotangulia, kwani sheria hiyo haikuzuia kufanya hivyo.
Sisi tunadhani kuwa kwa kuzingatia utamaduni uliozoeleka, Tume ingevunjwa rasmi katika mazingira ya kistaarabu na heshima kama tulivyoshuhudia ikizinduliwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete katika viwanja vya Ikulu, Aprili 13, 2012.
Tunashindwa kuelewa kiini cha udhalilishaji huo mkubwa kwa Tume hiyo, pamoja na Rais Kikwete kuimiminia sifa na pongezi nyingi kwa kuweka utaifa mbele. Akipokea Rasimu hiyo Desemba 31, 2013 katika viwanja vya Ikulu, Rais Kikwete alisema Tume hiyo imefanya kazi iliyotukuka na ya kihistoria na kuwataka wajumbe wa Bunge Maalumu waige mfano wake pindi Bunge hilo litakapoanza kazi ya kujadili Rasimu na hatimaye kuandika Katiba mpya. Sasa nini kimetokea kiasi cha Tume hiyo kuonekana kama imefanya uhaini ni kitendawili ambacho hakijateguliwa.
Sisi tunadhani kwamba haikuwa sahihi kwa Serikali kuwadhalilisha Jaji Warioba na makamishna wa Tume hiyo, hata kama pengine haikufurahishwa na baadhi ya mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba waliyoiwasilisha.
Kwa kuzingatia kwamba Tume hiyo iliundwa na watu ambao uzalendo wao hauwezi kutiliwa chembe ya shaka, Serikali ilipaswa kuienzi kazi waliyofanya hata kama kwa shingo upande.

0 comments:

CCM WACHEMKA KWENYE MAPENDEKEZO YA KAMATI BUNGENI

1


Mapendekezo ya CCM ya kutaka kufanya marekebisho katika baadhi ya vifungu katika Ibara ya 1 ya Rasimu ya Katiba yamegonga mwamba baada ya kukosa theluthi mbili ya kura kutoka Zanzibar.
Hali hiyo imejitokeza katika kamati tatu kati ya 12 ambazo zimeanza kutoa matokeo ya kura baada ya mjadala.
Wakitoa taarifa kwa waandishi wa habari, mwenyeviti wa Kamati Namba 1, Ummy Mwalimu na Namba 10, Anna Abdallah, walisema kuwa theluthi mbili imekosekana katika baadhi ya vifungu kwenye ibara hiyo.
Walisema kwamba vipengele vilivyokosa theluthi mbili ya kura zilizopigwa, vitapelekwa bungeni pamoja na hoja zilizotolewa na wengi na wachache. Abdallah alisema ibara nyingi walizozipigia kura katika kamati yake hazikupata theluthi mbili ya kura.
“Kwa mfano muundo wa serikali kwa vyovyote vile hatupati theluthi mbili, ila tunapata walio wengi wanataka nini. Walio wengi wanataka mfumo wa serikali mbili, kwa hiyo taarifa yetu itakuwa na maoni ya wajumbe wengi, na ile wachache,” alisema Anna.
Alikiri kuna wajumbe wachache ambao wanataka muundo wa shirikisho la serikali tatu, lakini hawawezi kusema hao ndio wameshinda.
Alitolea mfano wa ibara ya pili ya sura ya kwanza ambayo inazungumzia mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo waliafikiana kuongeza milima na anga.
Alisema kuwa ibara hiyo ilikubaliwa na wajumbe wote baada ya kuongezwa maeneo hayo mawili.
“Maeneo yenye utata ikiwamo kwenye muundo wa serikali ndio tumeshindwa kupata theluthi mbili ya kura zilizopigwa na wajumbe kutoka pande mbili za Muungano,” alisema.
Naye  Mwalimu alisema ibara ya 1 katika sura ya kwanza hawakupata theluthi mbili pande zote mbili.
Alisema uamuzi huo si wa mwisho, bado watakwenda katika Bunge la Katiba kupigiwa kura za jumla.
Pamoja na kamati nyingine kuendelea kupiga kura, habari za ndani zinasema upatikanaji wa theluthi mbili katika ibara hiyo ya kwanza umekuwa mgumu.

0 comments:

MAFUNDISHO YA MUNGU NA MTUMISHI WA MUNGU JOSEPHAT .E. MWINGIRA


DARASA/CHUMBA CHA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Efatha Ministry.
(Darasa linaendelea lilipoishia...)

"Usifurahi unakula tu ugali na kushiba wakati wengine wanasaza, wana nyumba nzuri, magari mazuri na maisha yao ni mazuri na yenye baraka; watoto wao wanasoma shule nzuri na wanapendeka maana wanafaulu vizuri; ukoo wao unatukuka! Lakini wewe hata ujitahidi, mbele huendi, kulikoni? Mwenye haki ana mateso mengi lakini BWANA humponya nayo yote.

Leo BWANA Atajifunua kwako kubali kufungua moyo wako."

(Usikose Darasa, Huu ni wakati wa USHINDI wako, Ni Neema hii kwako)

0 comments:

The founder of Match.com lost his girlfriend to a man she met on Match.com


The founder of
Match.com
lost his girlfriend
to a man she met
on Match.com

0 comments:

SITTA AFUNGUKA KUHUSU KUCHEZEWA KWA SAINI YA NYERERE NA MSEKWA

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,Samuel Sitta amekiri “kuchezewa” kwa saini ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na sehemu ya saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa zilizopo kwenye hati ya sheria ya kuridhia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema ni kweli kuna maneno katika hati hiyo ya sheria namba 22 ya 1964, iliyosainiwa na Nyerere na Msekwa, Aprili 25, 1964, yameongezwa.
Alisema katika saini ya Nyerere kumeongezwa herufi “us” kwa kompyuta na katika sehemu ya saini ya Msekwa kumeandikwa neno “Msekwa” kwa kompyuta, jambo ambalo ni makosa. Sitta alisema walioongeza maneno hayo ni wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuona sehemu ya maandishi kwenye saini hizo hayasomeki, lakini walifanya makosa.
“Wale vijana walipoona document (nyaraka) haisomeki waliongeza “us” mwisho kwa kompyuta kwenye saini ya Nyerere, ila walifanya makosa maana bora kitu kionekane kufifia hivyo hivyo lakini kibaki na maana yake,” alisema.
Hata hivyo, Sitta alisema kwa waliofanya kazi na hayati Baba wa Taifa wanatambua saini iliyopo kwenye hati ya sheria hiyo ipo sawa ukiondoa makosa ya kuwekwa herufi hizo.
Kuhusu saini ya Msekwa, alisema pia kulifanyika makosa katika sehemu ya saini hiyo, kuandikwa kwa kompyuta “Msekwa”.
“Ni saini ya Msekwa, lakini vijana wa chamber kwa AG waliongeza neno “Msekwa” kwa kompyuta. Ni mtu asiyejua thamani na uhalisia wa saini ni kubaki ilivyo hata kama kwa miaka 100 hata mtu aje kuisoma kwa darubini,” alisema.
Hata hivyo, alisema maudhui ya hati ya sheria hiyo, iliyosainiwa rasmi Aprili 25, 1964 ni sahihi kama ambavyo walikubaliana waasisi wa Muungano, Nyerere na Karume.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema alisema kwamba hafahamu kama ofisi yake inahusika na kuchezewa kwa saini hizo, tofauti na madai ya Sitta.
Sheria iliyopitishwa Z’bar
Sitta alisema ili kuondoa utata, ameagiza kupatiwa hati ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume (Presidential Decree) aliyotoa kusaini makubaliano kwani wakati huo, hakukuwa na Bunge.
“Karume alitumia Baraza la Mapinduzi akatumia amri ya Rais akasaini. Tunatarajia kuipata hiyo, sasa tutakuwa tumepata nyaraka za Bara na Zanzibar,” alisema Sitta.
Hata hivyo, alisema kisheria kilichopitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la MapinduziZanzibar ni yaleyale yaliyopo kwenye mkataba wa Muungano.
“Unajua kuhoji sasa mambo haya ni kupoteza muda, ni kama kuulizana na mke wako cheti cha ndoa baada ya kuishi pamoja miaka mingi, jana (juzi) nilikuwa nawaomba wajumbe kujua tunachotakiwa ni kutengeneza Katiba ambayo, inajibu matatizo yetu,” alisema Sitta.
Hati ipo UN - Akizungumzia hati ya Muungano, alisema kuwa ni kweli kupata hati hiyo kuna umuhimu, lakini mambo yote muhimu yanayohusu Muungano yamewekwa katika sheria hizo mbili zilizoridhiwa na pande zote.
Alisema kwa muda walionao wajumbe wa bunge hilo, lazima wautumie vizuri kuliko kwenda hadi Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya kuchukua hati hizo.
“Bunge la Tanganyika lililetewa muswada unaoonyesha mambo waliyokubaliana Nyerere na Karume, na Baraza la Mapinduzi likapelekewa hivyohivyo,” alisema na kuongeza: “Sasa ubishi wa hiyo hati ya kwanza kabisa ambayo wengi wanasema ipo Umoja wa Mataifa ilikopelekwa kuthibitisha nchi imebadili jina, hiyo ni ya nini? Ni ubishi wa bure tu.”
Sitta alisema kisheria kilichopitishwa na Bunge kinatambua yaliyomo katika hati hiyo na hali ndivyo ilivyo pia kwa Baraza la Mapinduzi.
Kwa takriban siku tatu, kamati kadhaa za Bunge zinazojadili Rasimu ya Katiba, zimekuwa na mgongano juu ya hati za muungano na uhalali wa saini za Nyerere na Msekwa.
Kanuni kutenguliwa - Alisema pia, Bunge la Katiba itabidi kubadili kanuni na ratiba yake katika kikao cha leo.
Sitta alisema kwa utaratibu uliokuwapo, leo kamati ndio zilipaswa kuanza kuwasilisha taarifa zake, lakini imeonekana haiwezekani.
“Ni kamati moja tu Namba 5, kati ya kamati 12 ndio ambayo ilikuwa imekamilisha kujadili na kupiga kura walau Sura ya Kwanza tu ya Rasimu, hivyo kwa hali ilivyo lazima tupitie upya kanuni zetu,” alisema Sitta.
“Tuliweka siku moja kwa ajili ya uandishi na kuandika ripoti, lakini haiwezekani, imebidi tuongeze siku nyingine moja ili wajumbe waweze kuipitia tena taarifa ya kamati ambayo itasomwa bungeni, vinginevyo itasababisha ubishi,” alisema.
Alisema marekebisho yote ya kanuni, yatafanyika leo bungeni na baadaye ndio itatolewa Ratiba ya Bunge katika siku zijazo.
Hata hivyo, alisema katika ratiba hiyo, kutakuwa na mapumziko ya Bunge Aprili 7, kupisha maadhimisho ya Siku ya Karume, baadaye Ijumaa Kuu, Sherehe za Pasaka na pia maadhimisho ya Sokoine na Muungano.
Chanzo - Mwananchi

0 comments:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 4 APRILI 2014

0 comments:

NINI KINASUMBUA VIWANGO VYA ELIMU TANZANIA

 
Baadhi ya watafiti wa masuala ya kielimu nchini Tanzania wamesema mgawanyo mbaya wa walimu katika ajira mpya ni moja ya mambo yanayokwamisha maendeleo ya kielimu ikiwemo kushuka viwango vya ufaulu kwa wanafunzi katika shule za msingi nchini humo.
Shirika lisilo la kiserikali la haki elimu limesema utafiti wake umebaini kuwa mikoa ya kanda ya magharibi nchini humo na ile iliyopo ziwa Victoria haijafikia malengo ya kitaifa ya idadi ya walimu katika kila shule
Katika ripoti hiyo ya utafiti wa shirika la Hakielimu, imeeleza kwamba mgawanyo wa walimu wapya haujalenga uhaba wa walimu uliopo.
Shirika hilo linasema kuwa baadhi ya mikoa iliyopokea mwalimu mmoja kwa kila wanafunzi 37, imeongezwa walimu jambo ambalo sio sawa kwa sababu baadhi ya mikoa haina walimu wa kutosha na hilo linapaswa kuzingatiwa.
Haki elimu wanasema sababu hizo ni baadhi ya mambo yanayochangia ufaulu duni , ambapo kwa kipindi cha miaka minne iliyopita ufaulu kwa shule za msingi umekuwa ni wastan wa asilimia 60 hadi 40 tu.
Limeongeza kwamba walimu wanataka kuishi katika mikoa ya karibu na hivyo kufanya kila wawezali kuwashawshi wadau kutowapeleka mikoa ya mbali.
Hata hivyo ripoti hiyo imetofautisha walimu wa sasa na wale wa miaka iliyopita. Linasema kuwa walimu wa zamani walikuwa na haiba, uzalendo na kujitolea kufanya kazi na pia walithaminiwa sana na jamii lakini leo kazi ya ualimu imekuwa kazi ya ilimradi
Baadhi ya mikoa nchini Tanzania imebuni mbinu zinazoweza kuwavutia walimu ili wafanye kazi katika maeneo yao kutokana na maeneo hayo kukosa walimu kwa miaka mingi mfululizo kutokana na mazingira duni ya kazi

0 comments:

VYETI BANDIA VYA UKIMWI VYAUZWA

 
Idhaa ya BBC kitengo cha Afrika kimebaini kuna watu wanaonunua matokeo bandia ya vipimo vya virusi vya HIV yakionyesha hawana virusi hivyo nchini Uganda.
Picha za Filamu zilizonaswa kisiri zinaonyesha namna ilivyo rahisi kutoa hongo kwa wahudumu wa afya ili kupata vyeti hivyo bandia.
Baadhi ya watu wanaonunua vyeti hivyo visivyokubalika kisheria wanasema wamefanya hivyo ili kupata kazi, kusafiri kwenda ng'ambo ama kwa ajili ya kupata wapenzi wa ngono.
Mwandishi wa BBC wa Kampala Catherine Byaruhanga alilitembelea kliniki 15 bila ya kujitambulisha.
Kumi na mbili kati ya kiliniki hizo zilikuwa tayari kumpa vyeti bandia vya kuthibitisha kuwa hawana virusi vinavyosababisha ukimwi vya HIV.
Wanaosimamia kliniki hizo walitaka hongo kati ya Dola 10 na 20 kwa kila cheti.
Picha za video tulizopiga kisiri katika maduka ya kupiga chapa katika maeneo mengi ya mji mkuu wa Uganda, Kampala zinathibitisha kuwa mtu anaweza kuigiza cheti pia kwa urahisi sana.
BBC ilipomkabdihi Waziri wa Afya, Ruhakana Rugunda, ushahidi huo, alikubali kuwa hiyo ni changamoto kubwa lakini akasisitiza kuwa Serikali itafanya kila juhudi kuwakamata na kuwashitaki wanaohusika katika ufisadi huo.
Serikali ya Marekani hutoa kiwango kikubwa cha peza za miradi inayotumiwa kupambana na ukimwi nchini Uganda.
Balozi wa Marekani alitoa wito kwa viongozi wa taifa hilo kufanya bidii zaidi kupambana na kashfa hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa hana uhakika kuwa Dola za Marekani hazijatumiwa katika kliniki hizo zinazotoa vyeti bandia.

0 comments:

TETEMEKO LA PILI LATOKEA NCHINI CHILE

 


Tetemeko la pili kubwa la ardhi limetokea Kaskazini mwa Chile saa 24 baada ya tetemeko la kwanza kubwa kutokea Jumatano na kuwaua watu sita huku likiharibu nyumba 2,600 huku likisababisha watu kuhamishwa kutoka maeneo ya Pwani.
Tetemeko hilo lenye vipimo vya 7.8 lilimlazimisha Rais Michelle Bachelet kuondoka pwani ya eneo hilo na kuelekea sehemu salama maeneo ya juu.

Maafisa wa huduma za dharura wameamuru kuondoshwa kwa watu kutoka maeneo yaliyo karibu na pwani ya nchi hiyo.
Hii ni baada ya Rais Bachelet alipokuwa kukagua uharibifu uliosababishwa na tetemeko la kwanza Jumatano.
Mawimbi ya kwanza ya Tsunami yamepiga katika fukwe ya bahari na hapajakuwa na taarifa za uharibifu wa aina yoyote.
Serikali za Chile na Peru zililazimika kutoa tahadhari ya tisho la Tsunami kwa mara nyingine ingawa tahadhari hiyo iliondolewa baada ya mawimbi makali kupiga maeneo ya Pwani.
Tetemeko hilo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ingawa hakuna taarifa zozote za uharibifu zaidi zimeripotiwa.

0 comments:

MAPOLISI WA EASTELIIGH WADAIWA KUWA PIGA WANAINCHI KIGAIDI

Majeruhi wa shambulizi la kigaidi mtaani Eastleigh


Wakazi wa mtaa wa Eastleigh ambako watu sita waliuawa katika shambulizi la kigaidi siku ya Jumatatu, wanalalamika kuwa polisi wanatumia nguvu kuwahangaisha huku wakiendelea kufanya msako wa kudhibiti usalama katika mtaa huo.
Wakazi wengi ambao ni wasomali wanasema kuwa polisi wanawachapa na kuwakamata kiholela huku operesheni hiyo ya usalama ikeindelea kwa siku ya tatu.
Baadhi waliohojiwa wanasema kuwa wanalazimika kuwahonga polisi kwa sababu hawana hatia na hawataki kukamatwa.
Polisi wamewakamata watu 1,000 mtaani Eastleigh na viunga vyake katika msako huo.
Kwa mujibu wa waziri wa usalama Joseph Ole Lenku operesheni hiyo itaendelea hadi pale washukiwa wa ugaidi na wale ambao wanaeneza itikadi kali za dini ya kiisilamu watakapokamatwa.
Mnamo siku ya Jumatatu, magaidi walishambulia mkahawa mmoja mtaani Easteligh na kuwaua watu 6 huku wengine 30 wakijeruhiwa.
Siku iliyofuata muhubiri tatanishi muisilamu, Sheikh Makababri akapigwa risasi na kuuawa nje ya mahakama ya Shanzu mjini Mombasa.
Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara tangu wanajeshi wake kuingia nchini Somalia kwa vita dhidi ya wanamgambo wa kisomali wa Al Shabaab.
Wapiganaji hao wameahidi kufanya mashambulizi Kenya hadi wanajeshi hao watakapoondoka Somalia.
Lakini serikali ya Kenya imesema kuwa kamwe haitaondoa wanajeshi wake Somalia kwani kwa sasa ijulikane kwamba wako vitani na kundi hilo la kigaidi.

0 comments:

KAZI BADO NZITO LIGI KUU YA ENGLAND MSIMU HUU NANI KUTWAA TAJI HILO



Ligi kuu ya England sasa imekuwa ni kitendawali nani kutwaa taji hilo katika msimu huu mgumu. Ligi hiyo yenye mashabiki wengi Duniani kutokana na umaarufu wa tumu zinazoshiri ligi hiyo imekuwa yenye kitendawili kikubwa baada ya mfumo mzima wa ushindi kubadilika.
Ligi hyo imekuwa ngumu kwa mashabiki kutabiri kutokana na ushindani mkubwa unaoonyeshwa na timu hizo pinzani.haya ni maelezo tu kuhusu timu hizo je we unaisi nani anafaa kutwa taji hilo la Ligi kuu ya England msimu huu?

0 comments:

MAFUNDISHO YA MUNGU NA MTUMISHI WA MUNGU JOSEPHAT .E. MWINGIRA



DARASA/CHUMBA CHA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Efatha Ministry.
(Darasa linaendelea lilipoishia....)

"Katika kila msuguano kuna kisababisho ambacho kina mzizi na huo mzizi ukijulikana utang’olewa na uking’olewa ndipo kipindi cha burudiko kitakujulia. Kipindi hiki kitakujilia pale tu huo mzizi utakuwa umeondolewa.

Zaburi 139: 23 -24 “Ee MUNGU unichunguze uujue moyo wangu, unijaribu uyajue mawazo yangu, uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu; ukaniongoze katika njia ya milele”, HAYA NDIO MAOMBI ya mtu anayetaka kupona na kufunguliwa katika vifungo vilivyopo ndani yake; anayetafuta WEMA WA BWANA utokee kwake; ANAYETESEKA anatafuta kiini cha mateso yake; aliye na taabu anayemlilia BWANA apate kumjulisha kiini cha tabu yake; mama aliye na TATIZO la NDOA anayemlilia BWANA apate kumkumbuka."

(USIKOSE Darasa ni NEEMA yako hii ya USHINDI, YESU Anakupenda)

0 comments:

OKWI AINGIA MITINI KAMBI YANGA



Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi ameanza vituko Yanga baada ya kuondoka kikosini na kushindwa kuambatana na wenzake walioingia kambini jana Bagamoyo, Pwani.
Wachezaji 20  wa Yanga  waliingia kambini kujiandaa na mechi ya Jumapili  Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Ruvu,  itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Van Der Pluijm aliliambia gazeti hili jana kuwa hakuambatana na Okwi kwa vile hakuwapo kambini wakati timu yake inajiandaa na safari ya Bagamoyo.
“Okwi hayupo kambini na hakuna anayejua sababu za kutokuwapo kwake, lakini niseme kwamba ni makosa, ingawa hilo naliacha kwa uongozi utajua nini cha kufanya,” alisema Pluijm.
Mdachi huyo amekuwa akiwalalamikia washambuliaji wakiongozwa na Okwi, Hamis Kiiza, Didier Kavumbagu na Jerry Tegete kwa kiasi kikubwa kuwa wamekuwa chanzo cha timu hiyo kufanya vibaya kwa sababu ya kushindwa kutumia nafasi nyingi wanazopata kufunga mabao katika baadhi ya mechi.
“Katika eneo ambalo linaumiza kichwa ni la ushambuliaji, nina washambuliaji wengi wazuri  pengine kuliko timu yoyote kwenye ligi, lakini hawafanyi ambacho wanatakiwa kufanya, wanapata nafasi nyingi lakini hawazitumii na hivyo kuikosesha timu ushindi.
Akizungumzia madai hayo, Kavumbagu amesisitiza kuwa wachezaji wenzake na wapenzi wa klabu hiyo, waache kutafutana uchawi na badala yake wapambane kwa ajili ya kutetea taji kwa sababu bado nafasi ipo.
Mshambuliaji huyo alisema: “Wanaosema tunacheza chini ya kiwango siyo kweli kama mechi yetu na Mgambo JKT aliyekuwapo alishuhudia  jinsi tulivyojitolea, lakini mazingira ya mchezo yalikuwa magumu na hali ya uwanja haikuwa nzuri.”
Mbali ya Okwi, Pluijm aliwataja wachezaji wengine ambao hawakuingia kambini jana kuwa ni viungo Haruna Niyonzima na Athumani Idd ‘Chuji’.
Kocha huyo alisema wachezaji hao hakuwajumuisha kwa sababu ni wagonjwa, hivyo amewapa muda wa kupumzika.
Katika hatua nyingine, uongozi wa Yanga, umepinga madai ya kuwa unawachunguza nyota wake, Juma Kaseja na Kelvin Yondani kwa madai  ya kuhujumu mechi yao dhidi ya Mgambo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Benno Njovu alisema hakuna ukweli kuhusu yanayosemwa kuhusu mchezo huo na yaliyotokea ni sehemu ya makosa ya kawaida ya mchezo.

0 comments:

SHIRIKISHO LA SOKA ULAYA (UEFA) YAIPIGA 'STOP' BARCELONA KUSAJILI


Nyon, Uswisi. Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) limeizuia klabu ya soka ya Barcelona kusajili wachezaji wapya kwa miezi 12.
Adhabu hiyo ambayo inakwenda sanjari na faini ya Euro 306,000 inatokana na Barcelona kukiuka kanuni kwa kusajili makinda wenye umri chini ya miaka 18 kutoka sehemu mbalimbali nje ya Hispania na kuwaweka katika shule yake ya soka, La Masia.
Pia, Shirikisho la Soka la Hispania limetozwa Euro 340,000 kwa kosa hilo, Fifa imeeleza jana.
Fifa imesema Barcelona imekuwa ikishawishi vijana wenye umri wa kwenda shule na kuwasajili kupitia mfumo wake wa kukuza vipaji.
Adhabu hiyo kubwa imewahi kuikumba Chelsea msimu wa 2009 baada ya kumsajili kinda wa klabu a Lens ya Ufaransa, Gael Kakuta.
Hata hivyo, adhabu hiyo ilifutwa baada ya klabu hiyo kukubaliana na Lens na kulipa Euro 3 milioni.
Shirikisho hilo la soka limeeleza kuwa kwa muda mrefu Barcelona imekuwa ikirubuni makinda hao, jambo ambalo halikubaliki.
Kanuni za Fifa zinataka sheria za kimataifa za uhamisho wa wachezaji zifuatwe na kuzingatiwa kwa wachezaji wenye miaka 18, isipokuwa kwa matukio maalumu na kwa ruhusa ya Kamati ya Hadhi ya Wachezaji.
Kamati ya Nidhamu ya Fifa imesisitiza haja ya kuwalinda wachezaji chipukizi na kuzingatiwa kwa kanuni za usajili na uhamisho wa wachezaji kimataifa.

0 comments: