TANESCO; MATRILIONI KUMALIZA MGAWO WA UMEME NCHINI

Wananchi kwa muda mrefu wamekuwa wakiteseka na wakati mwingine kupata hasira kutokana na kutopata umeme wa uhakika tangu miaka ya 1980. Wakati mwingine wanapata hasira baada ya vyombo vyao kuungua kwa mfano, friji, redio na televisheni kutokana na umeme kukatika na kurejea kwa kasi .
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) sasa, halipendi tena wateja wake wateseke kwa kuingia gizani kwa muda wa siku tatu, saa mbili mpaka saa 12, na pia hawataki tena kuwapo kwa ahadi hewa, bali sasa wanataka mapinduzi ya umeme wa uhakika kuanzia mijini mpaka vijini.
Kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme kila siku nchini na kuwapo kwa umeme mdogo, sasa Tanesco inaboresha miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam, kufunga mfumo mpya wa umeme katika Kanda ya Kaskazini Mashariki kutoka Dar es Salaam, Chalinze, Segera Tanga, Kilimanjaro mpaka Arusha.
“Mradi huu utakuwa ni wa kilometa 682 ambao utakamilika mwaka 2016 baada ya kugharimu Sh616 bilioni, tunataka wananchi wapate umeme wa uhakika,” anasema Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Felchesmi Mramba.
Tanesco vilevile inatarajia kuunganisha umeme kutoka Nairobi nchini Kenya, kupitia Arusha, mpaka Mbeya, mradi ambao utagharimu Sh433 bilioni.
Katika mchakato wa mradi huu, Tanzania ipo tayari kuanza, lakini upande wa Kenya inasita kuanza kwa mradi kutokana na sababu mbalimbali.
Pia Tanesco inakusudia kutekeleza mradi mwingine mkubwa katika Kanda ya Kaskazini Magharibi, inayojumuisha Mkoa wa Mbeya, Sumbawanga, hadi Kigoma kwenye eneo la Nyakanali na kuunganisha njia za umeme ambazo zinatokea Kahama.
Mramba anasema gharama za umeme kwenye kanda hiyo ni Sh960 bilioni na unatarajiwa kukamilika mwaka 2017 katika umbali wa kilometa 660. Mradi mwingine utaunganisha njia za umeme kutoka Geita mpaka Nyakanazi, mkoani Kigoma ambao utagharimu Sh35 bilioni.
Pia Tanesco imejipanga kufunga nyaya za umeme kutoka jijini Dar es Salaam mpaka mkoani Mtwara, lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kunakuwapo umeme wa uhakika endapo mradi wa umeme wa gesi utakuwa na hitilafu.
“Tutakuwa na mradi mwingine wa umeme wa kilometa 650 kutoka mkoani Mtwara mpaka Songea. Mradi huo utagharimu Sh640 bilioni, utakuwa kilometa 650 na utakamilika mwaka 2015,” anabainisha mkurugenzi huyo.
Uboreshaji mkubwa Dar es Salaam
Katika Jiji la Dar es Salaam moja ya miradi mikubwa ya kukabiliana na mgao wa umeme ni kufunga nyaya za umeme, kukarabati vituo 13 vya umeme kati ya 20 na kujenga vituo zaidi ya saba vipya vidogo vya vyenye uwezo wa 33kv mpaka 11kv. Vituo vipya vitajengwa Mwananyamala, Jangwani Beach, Kigogo, Tegeta, Muhimbili, Luguruni, na Mikocheni. Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, miradi hiyo tayari imeanza kutekelezwa.

0 comments:

HII NDIYO RAHA YA KUSOMESHA MTOTO WA KIKE

Mzazi na mkazi wa Ubungo, Juma Mkopi anatamani angejaaliwa kupata watoto wa kike pekee.
Tofauti na baadhi ya wazazi wanaofikiri mtoto wa kike hana thamani mbele ya mtoto wa kiume, yeye anatamani angekuwa na watoto wa kike ili aidhihirishie jamii kuwa mtoto wa kike anaweza na hata kuwa msaada mkubwa kwa familia yake na jamii kwa jumla.
Mkopi ana kisa kinachovutia kuhusu maisha yake, kama anavyokisimulia japo kwa ufupi: “Sisi kwetu tulizaliwa wawili; dada yangu na mimi. Niliishia kusoma A level (elimu ya sekondari kwa ngazi ya kidato cha tano na sita), lakini dada aliendelea na kufanikiwa kufika chuo kikuu.
“…mama yetu alikuwa muuguzi serikalini, tofauti na baba yetu, mama alikuwa mstari wa mbele kutusimamia kuhusu elimu. Kweli hakuwa na mchezo na elimu hasa kwa dada yangu.
Wakati mimi alikuwa ananiruhusu kwenda kucheza mara moja moja,dada yangu ama alazimishwe kulala au awe mezani anajisomea, niliyaona kama maisha magumu kwake, lakini leo nashuhudia matunda yake. Hata yeye nadhani anaiona faida ya udhibiti wa mama akiwa msichana.
“Dada amenizidi kila kitu katika maisha haya, nitakueleza kwa nini…Unaiona hii nyumba ninayokaa? (ananyoosha kidole kuelekea darini), siyo yangu kaniachia na familia yangu. Unadhani imegharimu kiasi gani? Ana mengi anayofanya kwangu, kwa ndugu na jamaa...’’
Kwa nini Mkopi anatamani angejaaliwa watoto wa kike pekee? Anasema: “Nimejifunza kwa dada yangu namna alivyo msaada kwa familia yetu. Uwezo wake wa fedha na hata imani ya kuwasaidia wengine, vitu ninavyoweza kusema vimetokana na kusoma kwake, kumemwezesha kusomesha watoto wengi katika ukoo wetu.’’
Anaongeza kusema: “Nina watoto watatu, wote wa kiume, sitarajii kuongeza lakini ninatamani Mungu angenipatia japo mtoto mmoja wa kike nimtengeneze kama alivyo dada yangu.’’
Ushuhuda halisi
Kisa hiki ni kielelezo madhubuti cha ukweli usio na chembe ya shaka kuwa mwanamke ni nguzo ya jamii, ni chachu ya maendeleo ya familia na jamii kama alivyo dada yake Mkopi. Chambilecho msemo…ukimsomesha mwanamke, umeelimisha jamii.
Hata hivyo, ni wazazi wangapi nchini wanaotambua ukweli huu? Kwa nini baadhi ya wazazi hawataki kuamini kuwa mtoto wa kike akiwezeshwa anaweza kuwa kiongozi bora wa familia na jamii, au hata kuwa msitiri wa wazazi wenyewe?
Dunia hasa ile ya kwanza inatambua nafasi na hadhi ya mtoto wa kike, iweje sisi wa dunia ya tatu tuendelee kumdunisha mtoto wa kike hadi kufikia hatua ya kumnyima elimu? Bado kuna mila na desturi potofu, achilia mbali mitazamo tenge ya baadhi ya wazazi wasioona umuhimu wa kusomesha watoto wa kike.

0 comments:

HUU NDIO UKUBWA WA TATIZO LA KUKOSA CHOO

Waswahili wanao usemi maarufu kuwa, raha ya nyumba ni choo.Kwa hakika, hawakukosea kwani chakula chochote kinapoliwa lazima kitumike mwilini na mabaki yake kutolewa kwa njia ya haja kubwa.
Hata hivyo, binadamu wa  jinsi zote, umri au rika baadhi yao wanakabiliwa na tatizo la kukosa choo, ambalo linawasumbua kweli. Tatizo hilo ambalo huzaa au kuambatana na tatizo jingine la kupata choo kigumu linatesa.
Kwa kawaida, mtu anapopata tatizo hili hutumia muda wake mwingi chooni akijaribu kusukuma haja kubwa wakati mwingine bila mafanikio.
Ni dakika chache zinazohitajika kumaliza haja inapotoka kwa urahisi, lakini kwa wenye tatizo hilo, dakika hizo hazitoshi kwao kumaliza haja.
Ugumu wa kuitoa haja hiyo huwasababishia maumivu makali na pengine kuzalisha maradhi mengine.
Kwa mtu anayeishi kwenye nyumba ya kupanga na yenye wapangaji  wengi wanaotegemea chumba kimoja cha choo zikiwamo zile za mijini, mmoja wao anapokuwa na tatizo hili la kupata choo kigumu  inaweza kuwa kero kwa wenzake.
Kwa ufupi,  mtu anapoingia chooni kujisaidia, wenzake hukaa nje wakisubiri kwa muda zamu zao za kuingia…hakika huwa ni mateso kwake na kero kwa wapangaji wenzake.
Tatizo la kukosa choo (constipation)
Kukosa choo kwa siku moja kitaalamu,  siyo tatizo, isipokuwa mtu anaweza kutajwa kuwa na tatizo hilo iwapo atakosa choo kwa angalau zaidi ya saa 72, yaani siku tatu.
Akizungumzia tatizo hili,  Mtaalamu wa Viungo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) , Dk Raymond Mwonekano anasema kwa kawaida kila mtu anatakiwa apate choo angalau mara tatu kwa wiki. “Kama mtu atakosa choo kwa siku tatu mfululizo, atahesabika kuwa na tatizo, lakini lazima awe amekula chakula kwa siku zote hizo.
Mtu ambaye hajala hawezi kuhesabika kuwa na ugonjwa huo bali atakuwa na tatizo jingine,” anasema.
Anaongeza kuwa tatizo hilo linatokana na haja kubwa kwenda taratibu na hivyo kuchelewa kutoka kwa wakati mwafaka.

0 comments:

MAMBO MUHIMU MATANO YANAYOIWEKA CCM PABAYA

Wiki mbili zilizopita Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliadhimisha sherehe za kutimiza miaka 37 tangua kuanzishwa, huku kikiwa na mambo matano yanayokikaba koo.

Pamoja na CCM kuendelea kuongoza nchi, ni dhahiri chama hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi zinazoweza kusababisha kusambaratika au kung’olewa madarakani katika uchaguzi ujao wa 2015.
Dalili za kusambaratika zinatokana na mgawanyiko wa makundi, yakiwemo yale yanayonyoosheana vidole kwa ufisadi, harakati za urais 2015, hali inayoendelea ya kuumbuana hadharani huku kashfa na tuhuma za rushwa na ufisadi ndani ya chama na katika Serikali yake ziliendelea kutamalaki, mambo ambayo yanaipa picha mbaya CCM mbele ya Watanzania.
Jambo jingine ni suala la kutetea Serikali mbili ndani ya Katiba Mpya. Iwapo CCM itashindwa kutetea mfumo wa sasa wa Serikali mbili, huenda ikawa ni mwanzo wa kuonekana kuwa imeshindwa kudumisha yale yaliyoasisiwa na waasisi wa Taifa hili; Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati, Abeid Karume.
Waasisi hao walipounganisha Zanzibar na Tanganyika na kuzaa Tanzania, waliona Serikali mbili ndizo zinazofaa kujenga mshikamano wa taifa moja, wakiamini kuwa Serikali tatu zingepanua wigo ule wa umoja.
Hata hivyo, Pius Msekwa ni mmoja wa viongozi wazoefu wastaafu ambao wametumikia chama hicho tangu mwaka 1960, anapingana na mambo hayo, akiamini kwamna CCM bado ni imara na inaendela kuungwa mkono na Watanzania walio wengi.
Kuumbuana ndani ya CCM
Pamoja na athari za wazi zinazoonekana, Msekwa anasema kauli za kuumbuana na kupakana matope zinazoendelea kujitokeza ndani ya chama hicho kuhusu urais 2015 hazina athari zozote kwa chama wala Serikali.
“Si jukumu la chama kuwanyamazisha watu, ila wasikilizaji wa kauli hizo watachambua mchele na pumba,” anasema Msekwa na kuongeza kuwa vitendo vya viongozi ndani ya CCM kunyoosheana vidole, kushutumiana na hata kudharauliana hadharani vinaashiria uhuru wa demokrasia ya maoni ndani ya chama.
Hivi karibuni Mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda alitoa msimamo ukimtuhumu Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuanza kampeni za urais 2015 na kumwelezea kuwa hafai na wala hana sifa za kuwa rais.
Kauli za Makonda ziliungwa mkono na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, John Malecela ambaye pia alimshutumu Lowassa akidai tayari ameanza kampeni za urais kwa kusambaza fulana zinazohamasisha mtandao wa marafiki zake.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kpamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nnape Nnauye, katika miezi ya karibuni waliibua suala la mawaziri saba mizigo na kuwatangaza hadharani wakimtaka Rais Jakaya Kikwete awachukulie hatua.

0 comments:

UTAWALA WA SYRIA ULIVUNJA MAKAZI KUADHIBU WAPINZANI WAKE

Serikali ya Syria imeyaharibu kabisa maelfu ya makazi kama adhabu jumla dhidi ya jamii ambazo ziliuunga mkono upinzani katika mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus na katika mkoa wa Hama.
Syrische Soldaten in Damaskus
Katika ripoti yake iliyochapishwa hapo jana shirika la Human Rights Watch, limeishutumu serikali ya Syria kwa kuviangamiza kabisa vitongoji vizima kutoka kwenye ramani kwa kutumia matingatinga na vilipuzi. "Operesheni hii ya kuvunjavunja makazi ya watu ni tukio la hivi karibuni linaloongezea orodha ya uhalifu uliofanywa na serikali ya Syria," amesema Ole Solvang, mtafiti wa masuala ya dharura wa shirika hilo.
Shirika la Human Rights Watch limeorodhesha visa kadhaa vya uvunjaji mkubwa wa makazi kati ya mwezi Julai mwaka 2012 na Julai mwaka 2013, visa viwili vikifanyika katikati mwa mkoa wa Hama na vitano katika mji mkuu, Damascus na viunga vyake. Kwa kutumia picha za setilaiti, shirika hilo limesema lilikadiria eneo la jumla ya hekta 140, ikiwa ni sawa na viwanja karibu 200 vya mpira wa miguu, liliharibiwa kabisa. Limedokeza kwamba majengo mengi yaliyobomolewa yalikuwa na ghorofa kadhaa na maelfu ya watu walipoteza makazi yao.
Picha za kabla ya operesheni hiyo katika kitongoji cha Wadi al-Joz katika mkoa wa Hama zinaonyesha majengo kati ya barabara mbili kuu mwezi Aprili mwaka jana, lakini picha zilizochukuliwa baadaye zinaonyesha maeneo meupe sehemu ambazo awali majumba yalikuwa yamesimama mnamo mwezi Mei mwaka jana.
"Baada ya uvunjaji huo jeshi likikuja katika kitongoji chetu likisema kutumia vipaza sauti kwamba lingekiharibu kama lilivyoviangamiza vitongoji vya Wadi al-Joz na Masha al Arbeen, iwapo risasi moja tu ingefyetuliwa kutoka hapa," alisema mwanamke mmoja kutoka kitongoji jirani wakati alihojiwa na shirika la Human Rights Watch.
Ngome za upinzani zililengwa
Shirika hilo limesema maeneo yaliyoathirika yanaonekana kuwa ngome za upinzani na hakuna ushahidi kuunga mkono madai ya serikali kwamba operesheni hiyo ilikuwa sehemu ya jitihada za kupanga maeneo ya miji. "Harakati hizo zilisimamiwa na vikosi vya jeshi na mara kwa mara zilifuatiwa na mapigano katika maeneo hayo kati ya vikosi vya serikali na vya upinzani," limeongeza kusema shirika hilo.
Shirika la Human Rights Watch aidha limesema limefaulu kubaini kwamba hakujakuwa na operesheni kama hizo za kuyavunja makazi katika maeneo ambayo kwa ujumla yanaiunga mkono serikali. Wakaazi wameliambia shirika hilo kwamba walionywa kwa muda mfupi na hata wakati mwingine hawakuonywa kabisa kabla operesheni hizo kuanza na hawakulipwa fidia yoyote.
Anschlag auf Bushaltestelle in Damaskus, Syrien Shambulizi katika mji wa Damascus
Mmiliki mmoja wa mgahawa katika kitongoji cha Qabun kaskazini mashariki mwa Damascus ameliambia shirika hilo kwamba alilazimishwa kuondoka eneo la uvunjaji wa makazi na kutishwa angetiwa mbaroni. "Kazi ya familia yangu iliharibiwa kwa sekunde moja mbele yangu nikiwa naangalia," aliliambia shirika hilo.
Mjini Damascus operesheni hiyo ilifanywa katika maeneo yanayoyazunguka maeneo yenye umuhimu kwa serikali, ukiwemo uwanja wa ndege.
Operesheni ni kinyume na sheria ya vita
Lakini shirika la Human Rights Watch limesema uharibifu huo ulikiuka sheria ya vita kwa sababu haukuwa na maana yoyote kijeshi na unaonekana ulinuia kuwaadhibu raia au kwa kuwa ulisababisha machungu yasiyo na mithili kwa raia. Ripoti hiyo imesema "wale wote waliohusika na uharibifu huo wa mali ya umma au kuweka adhabu jumla wamefanya uhalifu wa kivita na wanapaswa wachunguzwe na kuwajibishwa."
Ole Solvang, mtafiti wa shirika la Human Rights Watch amesema baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitia agizo la mahakama ya kimatafa ya uhalifu, ICC, linatakiwa kutuma ujumbe wa wazi kwamba kuufunika ukweli na uhalifu unaofanywa na serikali bila hofu ya kuadhibiwa hautakwamisha kupatikana haki kwa wahanga.
Der syrische Präsident Bashar al-Assad während eines Interviews für AFP Rais wa Syria, Bashar al Assad
Katika taarifa yake upinzani wa Syria umesema kuwatesa raia ili waachane na miito ya kutaka uhuru ni mkakati wa serikali. Umerudia mwito wa kumtaka rais wa nchi hiyo, Bashar al Assad, ang'atuke na utawala wake ukabiliwe na mashitaka katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC mjini The Hague, Uholanzi.
Zaidi ya watu 130,000 wameuwawa tangu kuanza mzozo wa Syria Machi 2011, huku mamilioni wengine wakilazimika kuwa wakimbizi nchini mwao au kuvuka mipaka na kuwa wakimbizi katika nchi jirani.
Mwandishi: Josephat Charo/AFPE

0 comments:

KANISA LA KATOLIKI LALAANIWA NA UMOJA WA MATAIFA

Kamati ya kutetea haki za binadaamu ya Umoja wa Mataifa imelikosowa kanisa Katoliki kwa kushindwa kukomesha visa vya udhalilishaji watoto kingono vinavyofanywa na makasisi
Kamati hiyo ya umoja wa Mataifa imesema maelfu ya watoto kote duniani wamedhalilishwa kingono kwa miaka mingi ndani ya kanisa katoliki.Katika ripoti inayolishutumu vikali kanisa hilo,kamati hiyo imesema kanisa katoliki limeshindwa kwa kiasi kikubwa mno kutekeleza ahadi yake ya kukomesha visa vya unyanyasaji kingono dhidi ya watoto vinavyofanywa na makasisi na wafanyakazi wa kanisa hilo ndani ya makanisa na shule zinazosimamiwa na kanisa hilo.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa inatiwa wasiwasi mkubwa na hatuwa ya makao makuu ya kanisa katoliki Vatican ya kutokubali ukubwa wa uhalifu uliofanywa na haijachukua hatua muafaka za kukabilana na unyanyasaji wa watoto ili kuwalinda na badala yake imeanzisha sera ambazo zimesababisha kuendelea kwa udhalilishaji huo bila ya kutojali.
Watuhumiwa wanalindwa na kanisa
Umoja wa Mataifa umeshutumu hatua ya kanisa hilo kuwahamisha makasisi wanaotuhumiwa kutoka parokia moja hadi nyingine ndani ya nchi na hata wakati mwingine kuhamishiwa nchi nyingine katika juhudi za kufunika maovu hayo na kuwakwepesha kukabiliwa na mkono wa sheria.
Mwanakamati wa kamati ya kutetea haki za binadamu ya umoja wa Mataifa Kirsten Sandberg Mwanakamati wa kamati ya kutetea haki za binadamu ya umoja wa Mataifa Kirsten Sandberg
Makao makuu ya kanisa hilo yametoa taarifa baada ya ripoti hiyo ya umoja wa Mataifa na kusema imesikitishwa na kile ilichokiita hatua za kuingiliwa kwa mafunzo ya kanisa hilo kuhusu uavyaji mimba na matumzi ya mpango wa uzazi.
Vatican imesema inaendelea kuwajibika katika kutetea na kulinda haki za watoto lakini imesikitishwa na jaribio la kamati hiyo kuingilia mafunzo ya kanisa katoliki kuhusu hadhi ya maisha ya mwanadamu na uhuru wa kuabudu.
Ripoti hiyo pia imependekeza kanisa hilo libadilishe sheria zake kuhusu utoaji mimba na mafunzo ya namna ya kuishi baada ya vijana kubalehe katika shule za kikatoliki ili kuhakikisha haki za watoto na upatikanaji wa huduma za afya zinahakikishwa.
Vatican ambayo ni mwanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa wa kulinda haki za watoto uliofikiwa mwaka 1989 ulikubali kuchunguzwa na jopo hilo la wataalam.
Usiri mkubwa umefunika maovu ya muda mrefu
Tangu mwaka 2001,visa hivyo vya unyanyasaji watoto kingono vilivyoripotiwa kutoka maeneo mbalimbali duniani vimekuwa vikishughulikiwa na kanisa hilo kupitia idara yake ya sheria.
Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis
Papa aliyestaafu mwaka jana Benedict wa kumi na sita, alikuwa kiongozi wa kwanza wa kanisa katoliki kuwaomba msamaha wathiriwa wa unyanyasaji huo na kutaka kutovumiliwa kwa maouvu hayo.
Mrithi wake Papa Francis mwezi Desemba alisema kanisa hilo linapaswa kuaibika kwa kuhusika katika udhalilishaji kingono kwa watoto na kuunda jopo maalum la kuchunguza uhalifu huo,kuzuia kuendelea kwake na kuwashughulikia waathiriwa.
Kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa ilisifu hatua hiyo ya Papa Francis lakini ilisema hiyo haitoshi kwani ni wakati uongozi wa kanisa uanzishe mfumo huru wa kushughulikia masuala ya haki za binadaamu kuangazia maovu hayo.
Shirika la kutetea haki za waathiriwa walionyanyaswa kingono na makasisi SNAP limetaka hatua za kisheria sasa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa baada ya kutolewa kwa ripoti hiyo.
Mwandishi:Caro Robi/dpa/afp/Reuters

0 comments:

SCHALKE YAINGIA TENA KATIKA MSITU WA SIMBA NI BAADA YA KUGARAGAZWA NA REAL MADRID

Schalke 04 baada ya kugaragazwa na Real Madrid katikati ya wiki katika mpambano wa Champions League sasa inakabiliwa na kibarua kigumu tena, ambapo inapambana na mshindi asiyeshindika msimu huu Bayern Munich.
Fans in der Bundesliga Schalke 04 Mashabiki wa Schalke uwanjani
Na katika ligi zingine Chelsea ya Uingereza inamatumaini ya kujiimarisha zaidi kileleni mwa ligi ya Uingereza , wakati Ronaldo anarejea katika ligi ya Uhispania, La Liga baada ya kutumikia adhabu ya kutocheza michezo mitano.
Wakiwa bado wanauguza vidonda baada ya kubugizwa mabao 6-1 na Real Madrid ya Uhispania , Schalke 04 inaingia katika mtihani mwingine mgumu jioni ya leo wakati watakapokuwa wageni wa Bayern Munich ambayo haijapoteza mchezo msimu huu.
Bundesliga Schalke Leverkusen Julian Draxler Julian Draxler
Hakuna cha kuhofia
Hatuna uchaguzi , ila kuachana na hisia za mchezo huo, amesema mchezaji wa kati wa Schalke Julian Draxler baada ya kimbunga kilichowakuta dhidi ya Real Madrid.
Tunapaswa kuondoa kichwani mwetu mchezo huo na kujitayarisha dhidi ya Bayern.
Fußball DFB-Pokal Viertelfinale Eintracht Frankfurt - Borussia Dortmund Wachezaji wa Borussia Dortmund
Schalke inakabiliwa na mlima mwingine mkubwa na changamoto kubwa zaidi dhidi ya Bayern , timu ambayo imeshinda michezo yake yote 14 na wameweka rekodi sasa ya kushinda michezo 47 bila kufungwa.
Bayern ni wazuri zaidi ya Real Madrid, lakini hatuendi kwao kupunguza madhara, amesema mkurugenzi wa spoti wa Schalke Horst Heldt.
Ushindi wa mabao wa 4-0 wa Bayern dhidi ya Hannover 96 wiki iliyopita umekiweka kikosi hicho cha Pep Guardiola mabingwa wa Ulaya points 19 mbele katika msimamo wa ligi ya Ujerumani Bundesliga .
Nyota wa Bayern Bastian Schweinsteiger anatarajiwa kuwamo tena katika kikosi cha kwanza kwa mara ya pili baada ya kurejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Borussia Dortmund ambayo inashikilia nafasi ya tatu katika Bundesliga inaikaribisha Nuremburg leo jioni bila hakika ya kuwa na mlinzi wao Socrates ambaye ni majeruhi.
DFB Joachim Löw Trainer Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew
Bayer Leverkusen inayoshikilia nafasi ya pili , inaikaribisha Mainz 05 , huku ikikabiliwa pia na kuporomoka katika kujiamini baada ya vipigo vya kutisha hivi karibuni mara saba katika michezo tisa.
Michezo mingine jioni ya leo(01.03.2024) ni kati ya Werder Bremen ikipambana nyumbani dhidi ya Hamburg SV, Augsburg inaikaribisha Hannover 96, na Eintracht Braunschweig ina miadi na Borussia Moenchengladbach.
Naye kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew amemteua mchezaji wa kati Bastian Schweinsteiger kurejea katika kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Chile siku ya jumatano wiki ijayo baada ya kupona kifundo cha mguu, ambapo pia kocha huyo amewaita kikosini wachezaji wengine wanne wapya.
Schweinsteiger , ambaye alicheza mchezo wake wa 100 dhidi ya Sweden Oktoba mwaka jana anaungana pia na mchezaji wa kati wa Borussia Dortmund Kevin Grosskreuz, ambaye aliwahi kuwamo kundini Februari mwaka 2011.
Wachezaji chipukizi walioteuliwa ni pamoja na Matthias Ginter wa Freiburg na Shkodran Mustafi wa Sampdoria pamoja na mshambuliaji wa Hamburg SV Pierre-Michel Lasogga na mchezaji wa kati wa Augsburg Andre Hahn.
Premier League
Katika ligi ya Uingereza, Premier League mlinzi wa Chelsea Gary Cahill amekiri kuwa timu hiyo ina fursa ya kuchukua hatua moja zaidi kuelekea katika ubingwa wa ligi hiyo wakati itakapokumbana na Fulham leo jioni.
Champions League - FC Schalke 04 gegen Chelsea Mlinzi wa Chelsea Ivanovic akishangiria bao
Wakati huo huo Brendan Rodgers anaamini kuwa Liverpool itakuwa mpizani tofauti kabisa na timu iliyoshindwa na Southampton mapema katika msimu huu wakati kikosi hicho kikijitayarisha kwa ziara muhimu katika uwanja wa St Mary leo jioni kupambana na Southampton.
Katika michezo mingine Arsenal London wako ugenini kupambana na Stoke City , Everton iko nyumbani ikiisubiri West Ham United , na Hull City ina miadi na Newcastle.
Real Madrid inaingia uwanjani kuumana katika mchezo wa nne wa watani wa jadi msimu huu dhidi ya Atletico Madrid kesho Jumapili na kikosi hicho kitaongezewa nguvu na kurejea kwa Cristiano Ronaldo ambaye amemaliza adhabu yake ya kutocheza michezo mitano.
Barcelona itajitupa dimbani pia kesho Jumapili (02.03.2014) ikiikaribisha nyumbani Almeria.
Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre

0 comments:

MWANARIADHA MO FARAH AENDELEA NA MAZOEZI KENYA

Bingwa mara mbili wa dhahabu katika Olimpiki, na ambaye pia ni bingwa wa ulimwengu katika mbio za mita 10,000 na 5,000 Muingereza Mo Farah yuko nchini Kenya lakini siyo kwa mapumziko au kujivinjari tu…hapana.
Mo Farah atakuwa nchini humo kwa kipindi cha wiki nne, ili kufanya mazoezi makali katika maeneo ya nyanda za juu ya Bonde la Ufa kabla ya mbio za marathon za jijini London mnamo mwezi Aprili, ambazo zitakuwa zake za kwanza kabisa katika taaluma yake ya riadha.
Mwanariadha huyo mzaliwa wa Somalia, atafanya mazoezi yake katika eneo la Iten, ambako amejiunga na wanariadha wengine sita wa Uingereza ambao waliwasili nchini humo mapema mwezi huu kujiandaa kwa Michezo ya Jumuiya ya Madola itakayoandaliwa mjini Glasgow mwezi Agosti. Wanariadha hao wanaishi katika kambi ya mazoezi ya nyanda za juu inayomilikiwa na mzaliwa wa Kenya aliyewahi kuweka rekodi ya ulimwengu ya mbio za half marathon, Lorna Kiplagat. Mji wa Iten ni nyumbani kwa wanariadha maarufu wa marathon nchini Kenya ikiwa ni pamoja na Wilson Kipsang, ambaye ndiye anayeshikilia rekodi ya sasa ulimwenguni kwa upande wa wanaume.
Na wakati Farah na wenzake wakiendelea kuipasha misuli moto, naye gwiji wa Ethiopia Kenenisa Bekele tayari ana rekodi mbili za ulimwengu, lakini anasema anaimezea mate rekodi nyingine ya tatu: ambayo mara hii ni ya mbio za marathon.
Bekele atazitimka mbio za marathon za mjini Paris mnamo Aprili 6, ikiwa ni wiki moja tu, kabla ya hasimu wake wa uwanjani Mo Farah wa Uingereua kujitosa barabarani kwa mara ya kwanza katika mbio za marathon. Wote wawili watalenga kufuata nyayo za Mfalme wa Ethiopia Haile Gebreselassie na wengine waliofanikiwa kujipa changamoto ya kushiriki mbio za marathon
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA

0 comments:

KERRY, STEINMEIER WAZUNGUMZIA WA FARAGHA

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ametumia ziara yake ya kwanza nchini Marekani tangu kufichuliwa kwa udukuzi wa Marekani nchini Ujerumani, kujadili ulinzi wa faragha na mwenzake John Kerry.
Mawaziri Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani na John Kerry wa Marekani katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Washington. Mawaziri Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani na John Kerry wa Marekani katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Washington.
Wasiwasi uliibuka kati ya washirika hao mwaka uliopita baada ya nyaraka zilizovujishwa na wakala wa ujasusi wa Marekani Edward Snowden, kuonyesha kuwa shirika la usalama wa taifa la Marekani NSA, lilikusanya taarifa kuhusu raia wa Ujerumani na lilidukuwa mawasiliano ya simu ya mkononi ya Kansela Merkel na wanasiasa wengine wa Ujerumani. Waziri Kerry alisema baada ya chakula cha mchana na Steinmeier jana Alhamisi, kuwa mazungumzo baina yao yalikuwa ya tija. Steinmeier anatarajiwa kufanya mikutano zaidi kuhusu faragha na ujasusi leo mjini Washington.
Waziri Kerry alisema mataifa yao ni marafiki wa zamani na ni marafiki wa karibu, na kwamba wana uwezo wa kuzungumza kwa uwazi na kutafuta njia ya kushirikiana pamoja kuhusu masuala muhimu yanayowahusu wote. Yeye na Steinmeier walijadili hatua zaidi za kuimarisha ushirikiano wa kijasusi baina ya Marekani na Ujerumani, na kuongeza kuwa wataendeleza mazungumzo katika miezi ijayo.
Ufichuzi wa Edward Snowden uliathiri pakubwa uhusiano kati ya Marekani na Ujerumani. Ufichuzi wa Edward Snowden uliathiri pakubwa uhusiano kati ya Marekani na Ujerumani.
Walizungumza kwa kirefu juu ya uhusiano baina ya Washington na Berlin, ikiwemo namna ya kuweka urari kati ya usalama wa raia wao na faragha za raia hao. Ujerumani inataka kuwepo na mkataba wa kutochunguzana baina yake na Marekani lakini wito huo bado haujajibiwa mpaka sasa. Steinmeier anasema makubaliano kama hayo yangeboresha kwa kiasi kikubwa uhusiano kati ya Ujerumani na Marekani, liliripoti jarida la habari la Ujerumani la Der Spiegel.
Ukraine yachomoza katika mazungumzo
Kerry alisema hali nchini Ukraine, ambako serikali mpya iko katika mchakato wa kuundwa baada ya miezi kadhaa ya machafuko, ilikuwa ya kipaumbele kwao, na ilichukuwa sehemu kubwa ya mjadala baina yake na Steinmeier wakati wa chakula cha mchana. Alimshukuru waziri Steinmeier kwa uongozi wake, akibainisha kuwa waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani alisafiri kwenda mjini Kiev na kusaidia kufikiwa makubaliano ya wiki iliyopita.
Hali nchini Ukraine ilikuwa miongoni mwa masuala yaliyozungumziwa na mawaziri Kerry na Steinmeier. Hali nchini Ukraine ilikuwa miongoni mwa masuala yaliyozungumziwa na mawaziri Kerry na Steinmeier.
Ziara hii ya siku mbili ndiyo ya kwanza nchini Marekani tangu Steinmeier alipoteuliwa kuwa waziri wa mambo ya kigeni miezi miwili iliyopita. Alihudumu kama waziri wa mambo ya kigeni katika baraza la kwanza la Kansela Angela Merkel kuanzia mwaka 2005 hadi 2009.
Amekutana kwa mara kadhaa na waziri Kerry, ambaye alifanya ziara fupi mjini Berlin mwaka huu na kuhudhuria mkutano wa ulinzi na usalama mjini Munich. Akiwa mjini Washinton, Steinmeier anatarajiwa kukutana na John Podesta, mshauri wa juu wa rais Barack Obama, na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa, Susan Rice.
Steinmeier amepangiwa kuzungumzia hali ya ushirikiano kati ya mataifa ya Ulaya na Marekani katika taasisi ya Brookings, katika hotuba inayotarajiwa kugusia mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine na vita vya Syria. Kandoni mwa hayo, Steinmeier atakutana na mkuu wa shirika la fedha duniani, IMF, Christine Lagarde, kujadili hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili Ukraine.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/dpae

0 comments:

UFARANSA YAPANIA KUZUIA KUGAWANYIKA KWA TAIFA LA CAR

Rais wa Ufaransa ameiambia Jamhuri ya Afrika ya Kati, wanajeshi wa Ufaransa walioko huko watafanyakazi kuiepusha nchi hiyo isigawike, na kuwapokonya silaha wanamgambo na makundi ya wahalifu wanaowapiga vita Waislamu.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande Rais wa Ufaransa Francois Hollande
Akiwasili mjini Bangui kutoka Nigeria, alikohudhuria sherehe ya miaka 100 ya muungano wa nchi hiyo, Rais Hollande alikutana na rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya kati Catherine Samba-Panza na pia kuwahutubia wanajeshi wa Ufaransa. Hii ni ziara ya pili ya Francois Hollande tangu mwezi Desemba mwaka jana na inakuja wakati kukiwa na ongezeko la wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Siku ya Jumanne bunge la Ufaransa lilipiga kura kurefusha muda wa wanajeshi wa Ufaransa nchini humo, licha ya Wafaransa wenyewe kutounga mkono ushirikishwaji wa wanajeshi wao katika koloni lake hilo la zamani.
Baadhi ya wanajeshi walioko Jamhuri ya Afrika ya Kati Baadhi ya wanajeshi walioko Jamhuri ya Afrika ya Kati
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema watu milioni moja wameikimbia nchi hiyo tangu kuanza kwa ghasia za kimadhehebu mwaka uliopita na kwamba watu wapatao milioni 1.3 wanahitaji msaada wa haraka wa chakula katika nchi hiyo ya Afrika.
Miezi minne iliopita, Ufaransa ilituma wanajeshi wake ambao kwa sasa wamefikia takriban 2000 katika nchi hiyo ilio na idadi kubwa ya Wakristo, na waasi wa Kiislamu wa kundi la Seleka walichukua madaraka baada ya mapinduzi waliyofanya mwezi Machi mwaka Jana, na wamekuwa wakisukumwa nyuma na wanamgambo wa kundi la "anti-balaka."
Kando na kuwepo kwa wanajeshi wa Ufaransa, Wanajeshi 6000 wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika (MISCA) pia wapo nchini humo huku takriban wanajeshi 1000 wa Umoja wa Ulaya wakiwa bado wanatarajiwa kuwasili Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Samba Panza atoa wito wa kuundwa kikosi cha kulinda amani cha U.N
Hata hivyo akizungumza mjini Geneva, baada ya miezi miwili ya kusimamia shirika la Umoja wa Mataifa la ulinzi wa Raia mjini Bangui, Philippe Leclerc, amesema bado nchi hiyo haina wanajeshi wa kutosha wa kulinda amani.
Rais wa mpito Samba Panza Rais wa mpito Samba Panza
Ulinzi mdogo ulililazimisha shirika hilo la Umoja wa Mataifa kuwahamisha baadhi ya raia.
Rais wa mpito Samba-Panza mara kwa mara amekuwa akitoa wito wa kuundwa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini mwake. Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki-moon anatarajiwa kutoa ripoti wiki ijayo, ya kuangalia uwezekano wa kukibadilisha kikosi cha MISCA kuwa kikosi cha Umoja wa Mataifa. Netsanet Belay, Mkurugenzi wa utafiti na utetezi wa shirika la Amnesty International, amelitaka baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuridhia hatua hiyo mara moja.
Kwa upande mwengine madaktari wasio kuwa na mipaka (MSF) wamesema zaidi ya wakimbizi 8000 waliwasili kusini mwa nchi jirani ya Chad tangu mwishoni mwa mwezi wa January.
Hata hivyo kundi la antibalaka linasemekana linawafuata Waislamu kule wanakokwenda na kujaribu kuwashambulia wakati wakijaribu kukimbia ghasia.
Mwandishi: Amina Abubakar/Reuters

0 comments:

OBAMA AELEZA WASI WASI YAKE KUHUSU UKRAINE

Marekani imeonya Ijumaa (28.02.2014) kuwa rais Barack Obama pamoja na viongozi wengine wa Ulaya wataususia mkutano wa kundi la mataifa ya G8 mjini Sochi iwapo wataona kuwa Urusi inaingilia uhuru wa Ukraine.
Obama zur Lage auf der Krim Rais Barack Obama akizungumzia kuhusu hali nchini Ukraine
Obama ameeleza wasi wasi wake mkubwa kuhusiana na ripoti kuwa majeshi ya Urusi yameingia mjini Crimea, kufuatia madai yaliyotolewa na afisa wa serikali mjini Kiev kuwa uvamizi umeanza.
Maafisa waandamizi wamesema rais ameamua kujitokeza katika ikulu ya Marekani ya White House na kutoa maelezo baada ya nchi hiyo kuamua kuwa kulikuwa na ushahidi kwamba majeshi ya Urusi ni kweli yako ndani ya Ukraine.
Soldaten auf der Krim Wanajeshi waliovamia majengo ya serikali huko Crimea
Vikosi vyenye silaha nzito na katika sare ambazo hazina nembo ya taifa vimeonekana kuzunguka majengo ya serikali na katika uwanja wa ndege katika mji wa Crimea wa Simferopol , wakati maafisa wa Ukraine wakiishutumu Urusi kwa kile walichokiita uvamizi wa wazi.
Majeshi ya Urusi
Mzozo huo ulianzia katika mzozo wa kisiasa na kiuchumi kufuatia kuondolewa kwa serikali inayoelemea upande wa Urusi mjini Kiev na kuingia katika mpambano wa kieneo baada ya madai ya maafisa wa Ukraine kuwa kiasi ya wanajeshi 2,000 wa Urusi wamewasili mjini Crimea.
Krim Flughafen Paramilitär 28.2.2014 Wanajeshi wakilinda doria
"Tuna wasi wasi mkubwa sasa kuhusiana na ripoti za harakati za kijeshi zinazochukuliwa na shirikisho la Urusi ndani ya Ukraine," Obama amesema.
Afisa wa jeshi ameliambia shirika la habari la AFP baada ya taarifa ya rais kwam,ba " inaonekana kama wameingiza wanajeshi kadha nchini humo."
Afisa huyo amesema kuwa Urusi haijatoa tahadhari yoyote kabla kuhusu harakati hizo. Obama anatambua kuwa Urusi imekuwa na maslahi yake pamoja na uhusiano wa kiutamjaduni na kiuchumi na Ukraine, na imekuwa na maeneo ya kijeshi katika eneo la Crimea, eneo ambalo liliunganishwa na jamhuri ya zamani ya Kisoviet ya Ukraine katika umoja wa Kisoviet mwaka 1954.
Obama aonya
Lakini amesema ukiukaji wowote wa uhuru wa Ukraine pamoja na ardhi ya nchi hiyo utaiyumbisha kwa kiasi kikubwa Ukraine. "Marekani itasimama pamoja na jumuiya ya kimataifa katika kusisitiza kuwa kutakuwa na gharama katika uvamizi wowote wa kijeshi nchini Ukraine," alisema rais Obama.
Afisa mwingine mwandamizi baadaye amedokeza kuwa gharama hizo zinaweza kujumuisha uamuzi wa Obama na viongozi wengine wa ngazi ya juu wa Ulaya kususia mkutano wa nchi zenye utajiri mkubwa wa viwanda za G8 mkutano utakaofanyika katika mji wa kitalii uliofanyika michezo ya Olimpiki wa Sochi mwezi Juni.
Simferopol Flughafen Militär Wanajeshi wanaodhaniwa kuwa ni wa Urusi katika uwanja wa ndege wa Simferopol
Uwezekano mwingine wa kibiashara na kiuchumi ambao Urusi ilikuwa inataka hadi wiki hii huenda ukaingia katika hali shaka , afisa huyo amesema.
Urusi pia itavuruga nafasi yake ya kuonekana kuwa na mvuto duniani baada ya michezo ya majira ya baridi, ambayo ilimalizika mwishoni mwa juma lililopita, ameeleza afisa wa Marekani.
Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

0 comments:

BURUNDI YASHTAKIWA MAHAKAMA YA AFRICA NI BAADA YA KUKIUKA HAKIZA BINADAMU

SERIKALI ya Burundi imeburuzwa kwenye korti ya Afrika Mashariki (EACJ), kwa madai ya kukiuka haki za binadamu na utawala wa sheria.
Isidore Rufyikiri
Inadaiwa kumnyang’anya pasi ya kusafiria Rais wa Chama cha Wanasheria Burundi (BBA), Isidore Rufyikiri, baada ya kufanya kikao na waandishi wa habari akizungumzia masuala ya utawala wa sheria, demokrasia na katiba ya nchi hiyo.
Katika shauri hilo lililofunguliwa na Chama cha Wanasheia wa Afrika Mashariki, (EALS), wanamtaka Katibu Mkuu wa EAC kwenda nchini humo kujionea hali halisi ikibidi nchi hiyo isimamishwe uanachama kabisa au kwa muda kutokana na kukiuka vipengele vya mkataba wa jumuiya hiyo.

0 comments:

TUTAANDAMANA KIKWETE AKISAINI NYONGEZA BUNGE LA KATIBA

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), limeazimia kuongoza maandamano kote nchini, kama Rais Jakaya Kikwete ataridhia nyongeza ya posho kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.
Viongozi wa Tucta mkoani Dodoma walisema kitendo cha wajumbe hao kulilia nyongeza ya posho kimewagusa mno na kimelifanya shirikisho hilo kutokuwa na imani na wajumbe hao.
Hadi sasa hakujawa na majibu ya moja kwa moja kuhusu msuguano unaotokana na madai hayo.
Mwenyekiti wa Tucta wa Mkoa wa Dodoma, Dk Hamoud Ndenge, alisema shirikisho halitakubali kuona mambo yasiyofaa yanaridhiwa.
“Rais akisaini nyongeza ya posho kwa wajumbe, lazima tutaandamana ili kudai madai ya wafanyakazi ambayo tulinyamazia baada ya kuona fedha nyingi zimeelekezwa katika jambo hili muhimu (Bunge),” alisema Ndenge.
Kiongozi huyo alitofautiana na mawazo ya wengi kwamba maisha katika mji wa Dodoma ni magumu na kwamba Sh 300,000 wanazolipwa sasa ni ndogo.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, maisha katika mji huu bado ni rahisi na kwa msingi huo hakuna sababu ya kuwaongezea posho.
Alisema maisha ya Dodoma hata kama wangelipwa kiasi cha chini ya kiwango wanacholipwa, wangeweza kumudu.
Kwa upande wake, Katibu wa Tucta mkoani humo, Ramadhan Mwendwa, alisema kiwango wanachodai wajumbe hao ni kikubwa zaidi ikilinganishwa na umuhimu wa kitu kinachofanyika.
Mwendwa aliwataka wajumbe kutambua kwamba wametumwa na watu ambao baadhi yao hawana uwezo wa kupata hata mlo mmoja kwa siku.

0 comments:

"NACHEZA POPOTE PALE UWANJANI" MRISHO NGASA

  Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa amesema yuko tayari kucheza kokote atakapopangwa na kocha wake Hans Pluijm.
Kauli hiyo ya Ngassa imekuja siku chache baada ya Mdachi huyo kumchezesha namba 8 wakati wa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting iliyomalizika kwa Yanga kushinda mabao 7-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
.
Akizungumza na gazeti hili, Ngassa alisema kuwa nafasi asiyoweza kuicheza ndani ni ya kipa pekee ambayo ni ngumu na hajawahi kuicheza tangu aanze kucheza soka la ushindani katika mechi mbalimbali.
Ngassa alisema, hachagui nafasi ya kucheza ndani ya uwanja atakayopangwa na kocha wake kutokana na uwezo wake wa kumudu kucheza nafasi zote akiwa uwanjani.
Aliongeza kuwa, yupo tayari kuendelea kucheza nafasi hiyo namba 8 katika kikosi hicho na kuondolewa namba 7, 9, 10 na 11 ambazo zimezoeleka ndiyo anazozimudu kuzicheza.
“Mimi nina uwezo wa kucheza nafasi zote ndani ya uwanja, nafasi nisiyoweza kuicheza ni kipa pekee, sijawahi kuicheza tangu nianze kujiingiza kwenye soka la ushindani.
“Lakini hizo namba nyingine zote nimezicheza na ndiyo maana kwenye mechi dhidi ya Ruvu Shooting nilicheza kwa kiwangocha juu kwa kufunga mabao na kutengeneza pasi nyingi zilizozaa mabao,”alisema Ngassa.

0 comments:

BUNGE LA KATIBA LAPINGWA KUENDESHA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA



Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Mwalimu Nyerere Idealogy Conservation Society ya jijini Tanga, imefungua Kesi Mahakama Kuu ikitaka kuzuia mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.
Taasisi hiyo inapinga mchakato huo wa Katiba kwa kile inachodai kuwa ni kasoro zilizojitokeza, ikiwamo wananchi kukosa uwakilishi uliotokana na ridhaa yao, posho kubwa wanayolipwa wajumbe na gharama kubwa zilizotumika katika maandalizi ya Bunge hilo.
Kesi hiyo ya madai namba 02/2014, ilifunguliwa Februari 17, mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Tanga na mwenyekiti wa taasisi hiyo, Dk. Muzzammil Mussa Kalokola.
Washtakiwa katika kesi hiyo iliyofunguliwa kwa stakabadhi ya malipo ya Serikali namba 49803745, ni Waziri wa Sheria na Katiba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), (kwa sasa ni Frederick Werema) na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo Mwenyekiti wake ni Jaji Mstaafu, Joseph Warioba.
Hata hivyo Jaji Werema na Jaji Warioba wamesema hawana taarifa za kesi hiyo.
Dk. Kalokola alisema katika hati yake ya madai kuwa anataka mchakato huo wa Katiba usitishwe kwa kuwa umevunja Katiba iliyopo.
Amesema Katiba ya sasa imekiukwa katika Muundo wa Bunge la Katiba na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika utekelezaji wa majukumu na wajibu wake wa kukusanya maoni na kutengeneza Rasimu ya Madadiliko ya Katiba ibara ya 98.
“Vilevile imeshindwa kuzingatia hadidu za rejea kama zilivyoainishwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83,” alisema Dk Kalokola.
Dk. Kalokola alifafanua kuwa Katiba ya sasa imeweka masharti kadhaa, ikiwamo utaratibu wa namna ya kuibadilisha na sheria nyingine ambazo zimeanishwa katika ibara ya 98 na Sheria ya mwaka 1984 Na.15 ib.14.
“Ibara ya 98 (1) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii kwa kufuata kanuni zifuatazo,” alisema huku akiinukuu ibara hiyo na kuendelea:
“Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii (isipokuwa yale yanayohusika na aya ya (b) ya ibara hii ndogo) au masharti yoyote ya sheria yoyote iliyotajwa katika orodha ya Kwanza kwenye Nyongeza ya Pili utaungwa mkono kwa kura za wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya wabunge wote.
“Muswada wa sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii au masharti yoyote ya sheria yoyote yanayohusika na jambo lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika Orodha ya Pili kwenye Nyongeza ya Pili iliyoko mwishoni mwa Katiba hii, utapitishwa tu iwapo utaungwa mkono kwa kura za wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Tanzania Zanzibar.”

0 comments:

DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat

Photo: Naibariki Jumamosi yangu... (Darasa linaendelea lilipoishia jana,... Pata UFAHAMU ili UWE HURU na MSHINDI).
Tatizo ambalo MUNGU Aliruhusu mwenyewe ni:- .
Ahabu alipotakiwa afe kwa sababu njia zake hazikumpendeza MUNGU, MUNGU Aliitisha kikao, MUNGU Akasababisha laana itokee hata kwa wale makuhani. Akauliza nani anaweza kumdanganya Ahabu ili akafe, vita ikaanzishwa ambayo haikuwepo ili tu Ahabu akafe.

N.B. Siyo kila vita inayoanzishwa unaruhusiwa uende ukapigane, tambua imetoka wapi kwanza. Ahabu alijiandaa kwenda kupigana, manabii wakaja na shetani naye akajitokeza kwa MUNGU.
(Kwa kutaka kuijua zaidi habari hii soma 1Falme 22:)

MUNGU Anapoamua kuleta mabaya mahali anamruhusu shetani mzoefu wa maovu. Kama MUNGU Akiona njia zako hazijanyooka na unapoelekezwa hutaki kuelewa, una masikio ya utafiti; MUNGU Anairuhusu roho ya upotevu ikufuate. Manabii wa uongo wanajitokeza.

(Darasa litaendelea wiki ijayo, USIKOSE Mwana wa MUNGU Wewe uliyedhamiria kuwa HURU, kuwa HURU KWELI KWELI, Ubarikiwe.)
(Darasa linaendelea lilipoishia jana,... Pata UFAHAMU ili UWE HURU na MSHINDI).

0 comments: