Marriage started shifting from arranged to love-based marriages in the 18th Century.

 ust when the clamor over "traditional" marriage couldn’t get any louder, along comes this groundbreaking book to ask, "What tradition?" In Marriage, a History, historian and marriage expert Stephanie Coontz takes readers from the marital intrigues of ancient Babylon to the torments of Victorian lovers to demonstrate how recent the idea of marrying for love is—

0 comments:

VIJANA WANAAMBUKIZANA UKIMWI KWA KUKOSA ELIMU

Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni - UNESCO limesema zaidi vijana 50 waliofikia umri wa kubalehe katika nchi za Kusini na Afrika Mashariki wanaambukizwa virusi vya ukimwi kila siku
Hali hiyo inatokana na wao kukosa elimu ya uzazi. Kutokana na hatua hiyo, UNESCO imeanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya kutoa msukumo kwa nchi kuhaksha kwamba mitaala ya elimu inakidhi viwango vya elimu ya uzazi itayowasaidia vijana hao kufanya maamuzi pindi watapojihusisha na masula ya mapenzi. Hayo yamebainika nchini Tanzania wakati shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilipozindua ripoti mpya kuhusu vijana na balehe yenye kauli mbiu isemayo “Vijana wa Leo-Muda wa kuchukua hatua sasa”
Katika utafiti wake uliofanya katika mataifa 21, yaliyoko Kusini na Mashariki mwa Afrika, UNESCO ilibaini kasoro kadhaa ikiwemo kukosekana kwa mitaala maalumu inayoangazia afya za uzazi kwa vijana. Hali hiyo ndiyo iliyotajwa kuwa imechangia kwa kiwango kikubwa kwa vijana hao kutokuwa na maamuzi sahahi pindi wanapoanza kujishughulisha na masuala ya kipamapenzi.
Utafiti huo pia ambao umewajumuisha wataalamu kutoka taasisi za umma, mashirika ya kiraia nay ale ya Umoja wa Matifa ikiwemo UNICEF na WHO, inanoyesha kuwa, kukosekana kwa elimu ya afya ya uzazi kwa makundi ya vijana kumesabisha mamia ya wanafunzi wa kike kuacha shule kila siku kutokana na kupata mimba.
Ukosefu wa elimu ya uzazi pia kumesababisha wanafunzi wa kike kuwacha shule kila siku kutokana na uja uzitoVIJA Ukosefu wa elimu ya uzazi pia kumesababisha wanafunzi wa kike kuwacha shule kila siku kutokana na uja uzito
Akizungumzia matokeo ya utafiti huo, Mtaalamu wa UNESCO Mathias Faustini alisema kkuwa pamoja na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa ili kukabiliana na tatizo la mimba shulenni na upunguzwaji maambukizi ya virusi vya HIV kwa vijana, lakini ozeefu umeonyesha kuwa juhudi hizo zimekosa mikakati ya kisanyansi.
Hata hivyo ili kukabiliana na hali hiyo UNESCO kushirikiana na nchi zilizoko katika Jumuiya ya Maendeleo Kusin mwa Afrika(Sadc) na zile zilizoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimekubaliana kuteleza mpango wa pamoja ambao uhakikisha elimu kwa vijana inaboreshwa.
Tayari mkakati wa awali umeandaliwa ambao utajadiliwa katika kikao kinachotazamiwa kufanyika mwanzoni mwezi Disemba nchini Afrika Kusin, kikiwa husisha mawaziri Wizara za Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Elimu na Masuala ya ufundi kutoka katika nchi zote wanachama.
Baadhi ya makundi ya wanafunzi pamoja na watetezi wa maslahi ya vijana yameanza kupaza sauti yakitoa mwito kwa mamlaka za kidola kuanz akumulika utendaji wake wa mambo.
Kuanzishwa kwa mkakati huo wa upitiaji mitaala ya elimu ya afya ya uzazi kwa vijana kunatajwa na wengi pengine kunaweza kusaidia kupunguza matatizo yanayowaandama vijana wananza kubalehe.
Mwandishi: George Njogopa
Mhariri: Josephat Charo

0 comments:

ZIWA TANGANYIKA LAKABILIWA NA VITISHO SITA

Watu waliozaliwa na kukulia katika maeneo ya pembezoni mwa Ziwa Tanganyika wana wakati mgumu, kwani ziwa hilo linakabiliwa vitisho sita vinavyoliathiri na ambavyo vinayagusa moja kwa moja maisha ya watu hao.
Wakimbizi wa Kikongo wakivuuka Ziwa Tanganyika. Wakimbizi wa Kikongo wakivuuka Ziwa Tanganyika.
Ziwa Tanganyika lenye kina cha ujazo wa mita 1,470, urefu wa kilomita 673 na upana wa kilomita 50 ni la pili kwa ukubwa barani Afrika na la pili pia kwa wingi wa ujazo wake wa maji duniani na kina kirefu baada ya Baikal la Saiberia. Lakini sasa, bonde la ziwa hilo limeanza kupoteza uhai.
Sudi Mnette anaangazia maisha ya watu waliomo kwenye bonde hilo, ambalo linazihusisha nchi za Tanzania, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi.
Kusikiliza makala haya, tafadhali bonyeza alama ya spika za

0 comments:

ZAIDI YA WAANDISHI WA HABARI 100 WAUAWA MWAKA 2013

Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa Habari-IFJ, leo (31.12.2013) limetoa ripoti yake ya mwaka huu wa 2013, likionyesha idadi ya waandishi wa habari waliouawa wakiwa kazini katika maeneo mbalimbali duniani.
Waandishi wa habari wa Misri wakiwa katika mgomo mjini Cairo Waandishi wa habari wa Misri wakiwa katika mgomo mjini Cairo
Kwa mujibu wa Shirikisho hilo kiasi waandishi wa habari 108 wameuawa kwa mwaka huu, huku waandishi wengi wakiwa wameuawa kutokana na mzozo wa Syria na kufuatiwa na mauaji ya Iraq.
Idadi hiyo imepungua kwa asilimia 10 ikilinganishwa na waandishi wa habari waliouawa mwaka uliopita wa 2012, lakini Shirikisho hilo la kimataifa la waandishi habari mesema serikali zinahitaji kuongeza juhudi za kumaliza mauaji hayo.
Ripoti hiyo ya IFJ iliyotolewa leo Jumanne (31.12.2013), imeeleza kuwa viwango vya mizozo bado havikubaliki na kuna haja ya haraka kwa serikali kuwalinda waandishi wa habari pamoja na kutekeleza haki zao za msingi.
IFJ yatoa wito kwa serikali
Shirikisho hilo limetoa wito kwa serikali ulimwenguni kote kukomesha uonevu na unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wote wa kwenye vyombo vya habari. IFJ imeiorodhesha Syria kama nchi hatari zaidi ambapo waandishi wa habari 15 wameuawa nchini humo, ikifuatiwa na Iraq ambako waandishi wa habari 13 waliuawa.
Nchi nyingine zinazofuatia ni Pakistan, Ufilipino na India ambako waandishi 10 waliuawa, Somalia wameuawa waandishi saba na waandishi wa habari sita wameuawa nchini Misri.
Shirikisho hilo ambalo linawawakilisha zaidi ya waandishi wa habari 600,000 katika nchi 134 duniani, limesema kuwa waandishi wa habari wa kike wamekuwa wakikabiliwa zaidi na kuongezeka kwa ghasia.
Katibu Mkuu wa IFJ, Eden White Katibu Mkuu wa IFJ, Eden White
Waandishi wa habari sita wameuawa mwaka huu wa 2013 na wengine wengi wamekuwa waathirika wa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na vitisho.
Ripoti za mashirika mengine ya vyombo vya habari
Mwanzoni mwa mwezi huu, shirika la kimataifa la kutetea haki za vyombo vya habari linalojulikana kama "Waandishi wa Habari wasio na mipaka", lilisema kuwa waandishi wa habari 71 waliuawa kwa mwaka huu, lakini utekaji nyara uliongezeka kwa kasi.
Nayo Taasisi ya Kimataifa ya Waandishi wa Habari-IPI, yenye makao yake mjini Vienna, imesema waandishi wa habari waliouawa kwa mwaka huu hadi sasa ni 117 na kuufanya mwaka huu wa 2013 kuwa mwaka wa pili mbaya zaidi tangu ianze kurekodi mauaji ya waandishi wa habari duniani mwaka 1997.
Kwa mujibu wa IPI, mwaka 2012 ulikuwa mbaya zaidi ambapo waandishi wa habari 132 waliuawa, huku 39 wakiwa wameuawa nchini Syria.
Ama kwa upande wake Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari-CPJ yenye makao yake mjini New York imesema waandishi wa habari waliouawa kwa mwaka huu ni 70, wakiwemo wanane waliouawa mwezi huu wa Desemba.
CPJ imesema Syria ndiyo inaongoza kwa vifo hivyo, ambapo waandishi wa habari 28 waliuawa. Utafiti wa Shirikisho hilo la Kimataifa la Waandishi wa Habari-IFJ, uliwahusisha wafanyakazi wa vyombo vya habari kama vile wapiga picha na watangazaji.
Mwandishi: Grace Patricia Kabogo/AFPE
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

0 comments:

MAKAMPUNI MAKUBWA YAHIMIZAWA KUPAMBANA NA BIASHARA YA KUUZA WA0TU

Washikadau wametoa wito kwa makampuni makubwa 15 nchini Marekani kuhakikisha kuwa kampuni zake zilizo nje ya nchi hazisaidi katika uvunjifu wa haki za binaadamu hasa kazi ngumu na bishara ya ngono.
Menschenhandel, Moderne Sklaverei Wanafunzi wakiromania wakitoa hamasa ya hatari ya biashara ya kuuza watu na ile ya ngono.
Katika kampeni itakayodumu mwezi mzima wa Januari, taasisi ya ICCR inayowakilisha mashirika ya washika dao 300 yanayoendesha mali ya takriban dola bilioni 100 inatoa umuhimu kwa sekta mbili kwa ujumla, ukarimu na kilimo cha chakula.
Sekta hizi zinajumuisha mahoteli, mashirika ya ndege, mikawaha, makampuni makubwa na makambuni yanayojishughulisha na kilimo yanayoonekana sana kuwa katika hatari ya kuvunjwa kwa haki za binaadamu.
Amol Mehra mkurugenzi wa shirika moja la kimataifa aliliambia shirika la habari la IPS kwamba katika kupambana na dhuluma kama biashara ya kuuza watu isiokubalika, kila mtu ana jukumu la kutekeleza na bishara inapaswa kuwa moja ya njia ya suluhu kuweka katika vitendo heshima ya haki za binaadamu na kuhakikisha wateja wake, maajenti, wafanyabiashara wenzao na hata wanaowauzia mali kuwa wanafuata mkondo mmoja.
Jemen afrikanische Migranten in Harad Madhara ya biashara ya kuuza watu isiokubalika
ICCR sasa imetoa wito kwa makampuni makubwa 15 nchini Marekani kuchukua hatua katika suala hili. Makampuni haya ni kama ADM, ConAgra, Costco, Kroger, Target Walmart, mashirika ya ndege kama Delta, US Airways na Southwest pamoja na mahoteli kama Hyatt, Starwood, Choice na kadhalika.
Wanachama wa makundi haya hivi karibuni wametoa mikakati mipya itakayoongoza makampuni kuhakikisha kuwa wale wote walio na mkataba na kampuni hizo wanakubali kuafikia makubaliano ya kimataifa ikiwemo ule wa Umoja wa Mataifa juu ya Bishara na haki za binaadamu uliopitishwa mwaka wa 2011 yanayonuia kupiga vita aina yoyote ya biashara ya kuuza watu isiokubalika.
Makampuni pia yanatiliwa mkazo kuweka katika maandishi habari za mara kwa mara za namna wanavyokabiliana na suala hili na pia kuchambua hatari yake.
Njia zaidi za kupambana na kadhia hiyo zatolewa
Lauren Compere mwanachama wa ICCR amesema mahali ambapo makampuni yanakosa kuwepo katika viwango vinavyohitajiwa ni wakati panapokuja suala la ufichuzi, hasa katika sekta ya ukaribu kama vile hoteli, kufichua hatari ya kuwepo kwa hali ya dhuluma mbali mbali kunahitaji zaidi mfumo wa hadhi ya juu katika kuripoti.
Laureen amesema kwa sasa habari wanazozipata hazijachapishwa mahala popote au zinaosa ushahidi. Amesema kampuni nyengine zinaendelea vizuri kufichua visa vya uvunjifu wa haki za binaadamu na wala sio biashara ya kuuza watu isiokubalika.
Zwangsprostitution Prostitution Menschenhandel Deutschlandm Miguu ya msichana aliyekatika biashara ya Ngono
Kulingana na shirika la kimataifa la wafanyakazi mwaka wa 2012 takriban watu milioni 14.2 wanafikiriwa kuhusishwa katika aina ya kazi za kulazimishwa huku wengine milioni 4.5 wamekuwa wakiingizwa katika biashara ya ngono.
“Mahoteli mikahawa na sekta nyengine za burudani, sana huonekna kukumbwa na biashara za ngono na tumeona kuwa iwapo watu wanaofaya biashara kama hizi watafungua mach yao basi hueda wakapata visa vingi vikienhdeea humo ndani,” Alisema Karen Stauss, mkurugenzi wa mpango wa kuachia watumwa.
Karen Stauss amesema kuwa katika sekta ya kilimo mambo ni tofauti kwa kuwa katika eneo hilo ndiko unakopata watu wanaopata mapato madogo sana na wanaotokea mashambani wakiwa na kiwango kidogo cha eliu na kutojua haki zao.
Sasa Stauss amesema hakuna njia yoyote ambapo wanaweza kusuluhisa sula la biashra ya kuuza watu isiokubalika hadi pale akapuni makubwa yatakapoungana pamoja na kujhusisha na kampeni ya kuupiga vita.
Mwandishi:Amina Abubakar/IPS
Mhariri:Sekione Kitojo

0 comments:

WANAJESHI WA UMOJA WAMATAIFA KUPELEKWA BANGUI

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limependekeza kuwepo idadi ya wanajeshi zaidi ya elfu kumi katika Jamhuri ya afrika ya Kati kwa ajili ya kulinda amani.
Vikosi vya Umoja wa Ulaya kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati Vikosi vya Umoja wa Ulaya kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati
Tayari kikosi cha umoja wa Ulaya kimepewa ruhusa na Umoja wa mataifa ya kwenda Jamhuri ya Afrika Kati ili kuwalinda raia.Kwenye azimio lililopitishwa kwa kauli moja na wanamemba 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa ni kwamba viongozi wa makundi yaliohusika na ukiukaji wa haki za binaadamu wataekewa vikwazo na Umoja huo.Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo . Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Salehe Mwanamilongo

Mhariri: Mohamed Abdulrahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

0 comments:

MAPAMBANO DHIDI YA WAASI BADO YANAENDELEA SUDAN YA KUSINI

Wanajeshi wa serikali ya Sudan Kusini na waasi bado wanaendelea na mapigano licha ya makubaliano ya wiki iliyopita ya kuweka chini silaha, huku kila upande ukitafuta kuchukua udhibiti wa miji mikuu nchini humo
Umoja wa Mataifa umesema idadi ya raia wanaotafuta hifadhi katika kambi zake nchini humo inazidi kupanda. Naibu wa msemaji wa umoja wa Mataifa Fahran Haq amewaambia waandishi wa habari kuwa kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Mataifa kilichoko Sudan Kusini, UNMISS, kimeripoti kuzorota kwa hali ya usalama katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Unity ambako kuna viwanda muhimu vya mafuta na mapigano ya mara kwa mara yameripotiwa kati ya wanajeshi na waasi wanaomuunga mkono aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar. Haq amesema idadi ya watu waliopewa hifadhi katika kambi za Umoja wa Mataifa kote nchini humo imeongezeka na kufikia watu 79,000 kutoka idadi ya awali ya 76,000. Nusu ya idadi hiyo iko kazika kambi mbili za Umoja wa Mataifa mjini Juba.
Raia wengi wa Sudan Kusini wanaendelea kutoroka nchini humo kutokana na hofu kwamba makubaliano ya kusitisha vita huenda yasitekelezwe. Huyu hapa ni mmoja wa raia wanaoishi katika kambi ya wakimbizi nchini Uganda. "Bado kuna dalili za kuendelea mapigano, licha ya muafaka wa kusitisha mapigano. Serikali haitaki kuwapa waasi nafasi yoyote, nao waasi wanataka madaraka, na watajaribu wawezavyo kujipanga upya na kushambulia. Kwa hivyo kuna hofu mapigano yanaweza kuanza tena"
Konflikt im Südsudan Flüchtlinge 17.01.2014 Maelfu ya Wasudan Kusini wamepewa hifadhi katika kambi ya wakimbizi ya Adjumani Kaskazini mwa Uganda
Takribani watu 47,000 wamepewa hifadhi nchini Uganda na msemaji wa Shirika la Kuwashughulikia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa nchini Uganda Lucy Beck anasema hali ni mbaya katika kambi hizo."Kufikia jana walikuwa karibu 197, lakini wale wanaowasili ni wanyonge baada ya kusafiri kwa muda mrefu bila pesa za kutosha. duru nchini Sudan Kusini zinasema kuna watu wengi ambao hawajafanikiwa kufika Uganda, au wangali njiani".
Mkuu wa shirika la misaada ya kibinadaaamu wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos ambaye hapo jana alizuru mji wa Malakal amesema uhalifu wa kivita umefanyika Sudan Kusini na kuongeza kuwa watu aliozungumza nao wamepoteza kabisa imani na wanataka kuhamishwa hadi maeneo mengine nchini humo au hata katika nchi nyingine. Mashirika ya kutoa misaada nchini humo yamesema kiasi ya watu 10,000 wameuawa katika mzozo huo ulioanza tarehe 15 mwezi uliopita.
Na wakati hali ikiendelea kuwa tete nchini humo, Waziri wa sheria wa Sudan Kusini Paulino Wanawilla Unago amesema kuwa kiongozi wa waasi Riek Machar na wenzake sita wanastahili kushtakiwa kwa makosa ya uhaini kuhusiana na jukumu lao katika umwagaji damu uliofanywa nchini humo. Waziri huyo amesema wanasiasa wengine saba waliokamatwa baada ya vurugu kuzuka, wataachiliwa huru, ikiwa ni mojawapo ya masharti ya waasi katika meza ya mazungumzo.
Miongoni mwa wale waliowekwa kizuizini ni Pagan Amum, ambaye alikuwa katibu mkuu wa chama tawala, aliyekuwa waziri wa usalama wa taifa Oyai Deng Ajak, balozi wa zamani nchini Marekani Ezekiel Lol Gatkuoth na aliyekuwa naibu waziri wa ulinzi Majak D'Agoot.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

0 comments:

ARSENAL YAPUGUZWA KASI,STURRIDGE AIONGOZA LIVERPOOL KUIFUNGA EVERTON MABAO 4-0 HUKU JUAN MATA AKIIONGOZA MAN UTD KUPATA USHINDI.


Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge alifunga mabao mawili huku akikosa mkwaju wa penati lakini nahodha Steven Gerrard alikuwa nyota wa mchezo kwenye mechi ya 222 baina ya mahasimu hawa wa kitongoji cha Merseyside,kwenye mchezo Gerrard na Luis Suarez walifunga bao moja moja na kuiongoza Liverpool kuifunga Everton mabao 4-0.
 


Arsenal ilishindwa kujikita kileleni baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Southampton ugenini kwenye uwanja wa St Mary’s.



Mchezaji ghali kwenye historia ya klabu ya Man Utd Juan Mata alivaa jezi yake namba 8 ya Man Utd kwa kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cardiff City.
Kwenye mchezo huo mabao ya Man U yalifungwa na Robin Van Persie pamoja na Ashley Young.

0 comments:

LEVERKUSEN, DORTMUND ZAONA VIMULIMULI

Ilikuwa ni wikendi yenye kisirani kwa mahasimu wa viongozi wa ligi Ujerumani Bundesliga, baada ya Bayer Leverkusen na Borussia Dortmund kushindwa kupunguza pengo baina yao na viongozi Bayern
Bayern Jumamosi walijiweka imara kileleni kwa kuendeleza walikowachia katika duru ya kwanza ya msimu, walipowanyamazisha Borussia Moenchengladbach kwa kuwafunga magoli mawili kwa sifuri. Vigogo hao sasa wanashikilia usukani wakiwa na pointi 47 baada ya kutoshindwa mchuano mmoja kati ya mechi zao 42 mfululizo, na hivyo kuweka pengo la pointi 10 dhidi ya nambari mbili Leverkusen walioshindwa mabao matatu kwa mawili na Freiburg.
Mchezaji wa Dormtund Jakub Blaszczykowski atakuwa nje katika kipindi kilichosalia cha msimu kutokana na jeraha Mchezaji wa Dormtund Jakub Blaszczykowski atakuwa nje katika kipindi kilichosalia cha msimu kutokana na jeraha
Na pengo hilo huenda likapanuka hata zaidi mwishoni mwa siku ya Jumatano wiki hii, wakati Bayern itakaposhuka dimbani kucheza mchuano uliopangwa upya dhidi ya Stuttgart, ambao hawakucheza wakati wlaipokuwa nchini Morocco kucheza katika dimba la kombe la Klabu bingwa duniani, ambalo walikuja nalo mjini Munich. Thomas Müller ndiye aliyefunga goli la pili kupitia mkwaju wa penalty "Tayari tulifahamu kwamba Gladbach hawangeweza kuudhibiti mpira kwa zaidi ya dakika 90 kwa sababu sisi tunawazidi na tunautafuta mpira kwa haraka. Kulikuwa na tukio la mchezaji kuunawa mpira, tukajikinga vyema, kipa wetu Manuel Neuer akawa mzuri na hata wakawa na bahati mbaya kwamba mpira uligonga mwamba. Kwa jumla tulikuwa timu bora, lakini Gladbach wameonyesha kuwa wanaweza kupambana".
Mlinda lango wa Gladbach Marc-André ter Stegen alikiri kuwa wapinzani wao Bayern walikuwa moto wa kuotea mbali. "Ni wazi Bayern ilikuwa timu bora kutuliko, lazima ukubali. Walifunga goli mapema na hivyo ikawa vigumu kwetu. Wakati Bayern wanaongoza moja bila, inakuwa vigumu. Tulijaribu kwa muda mrefu kuyaweka mambo sawa lakini hilo halikuwezakan, lakini nadhani kwetu sisi hatuhitaji kushindana na Bayern Munich. Kuna mechi nyingi sana ambazo ni muhimu kwetu".
Mshambuliaji wa Schalke Klaas-Jan Huntelaar alirejea kwa kishindo baada ya kupona jeraha Mshambuliaji wa Schalke Klaas-Jan Huntelaar alirejea kwa kishindo baada ya kupona jeraha
Borussia Dortmund ilishindwa kuizuia Augsburg katika mechi iliyoishia sare ya kufungana magoli mawili kwa mawili na hivyo vijana hao wanjano wakasalia katika nafasi ya tatu na pointi 33 , ikiwa ni nne nyuma ya nambari mbili Leverkusen.
Schalke 04 ilisonga hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 31 huku Klaas-Jan Huntelaar akitikisa wavu katika mechi hiyo iliyokuwa yake ya kwanza baada ya kurejea kutoka mkekani kw amiezi mitano na kuwasaidia vijana hao wa samawati kuwabwaga Hamburg mabao matatu kwa sifuri. Huyu hapa Huntelaar akizungumza baada ya kuulizwa kama anaridhika na hali yake baada ya kupona jeraha. "Ndiyo nimeridhika. Nimeweza kucheza kwa dakika 75 baada ya kuugua jeraha wka muda mrefu. Nimekuwa nikisubiri sana kurejea tena katika hali hii. Kwa hivyo nikafanya mazoezi na kwa kuanza na ushindi ni vizuri kabisa bila shaka".
Werder Bremen ilitekwa kwa sare ya sifuri kwa sifuri na washika mkia Eintracht Braunschweig. Katika mechi nyingine za Jumamosi, Nuremberg iliifunga Hoffenheim magoli manne kwa sifuri ikiwa ndio ushindi wao wa kwanza kabisa msimu huu, wakati nayo Hannover ikiicharaza Wolfsburg magoli matatu kwa moja. Mainz ilisajili ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Stuttgart. Na Eintracht Frankfurt ikaizaba Hertha Berlin bao moja kwa sifuri.
Mwadishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

0 comments:

CRISTIANO RONALDO ATUNIKIWA BALLON D' OR.

Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa mwaka Ballon d'Or. Ujerumani ilinyakua tuzo tatu, wakati Jupp Heynckes na Silvia Neid wakishinda tuzo ya makocha bora
Preisverleihung Weltfußballer 2013 Cristiano Ronaldo
Nadine Angerer akiibuka mchezaji bora mwanamke. Katika sherehe za kila mwaka za Ballon d'Or mjini Zurich, Shirikisho la Soka Ulimwenguni - FIFA lilimtaja Cristiano Ronaldo kama mchezaji bora ulimwenguni katika msimu wa mwaka wa 2012/2013. Mreno huyo alipigiwa kura na kumpiku nyota wa Barcelona Muargentina Lionel Messi na Mfaransa Frank Ribery wa Bayern Munich. Kama Messi angeshinda, tuzo hiyo ingekuwa yake ya tano mfululizo.
“Namshukuru kila mmoja, wachezaji wenzangu, timu ya taifa na familia yangu, kila mtu hapa” alisema Ronaldo aliyebubujikwa machozi.
“Sina maneno mengine ya kuielezea hali hii” aliongeza. CR7 alishinda tuzo hiyo ya FIFA ya mchezaji bora ulimwenguni mara ya mwisho katika mwaka wa 2008.
Jupp Heynckes aliwabwaga Jurgen Klopp na Alex Ferguson kwa kunyakua tuzo ya kocha bora wa mwaka Jupp Heynckes aliwabwaga Jurgen Klopp na Alex Ferguson kwa kunyakua tuzo ya kocha bora wa mwaka
Mfaransa Franck Ribery alipigiwa upatu kushinda tuzo hiyo, kufuatia jukumu lake alilotekeleza katika klabu yake ya Bayern Munich, kushinda taji la Bundesliga, DFB Pokal na Champions League katika msimu wa 2012/2013. Pia alinyakua tuzo ya Shirikisho la Soka Ulaya – UEFA, mchezaji bora wa msimu wa 2012/2013.
Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi pia alikuwa kwenye orodha hiyo. Nyota huyo wa Barca alishinda mataji ya Ballon d'Or kwa miaka mitano mfululizo.
Ujerumani yashinda mataji matatu
Jupp Heynckes, kocha wa Bayern Munich katika msimu uliotangulia, alinyakua tuzo ya FIFA ya Kocha Bora wa Mwaka baada ya kuiongoza timu yake katika kutwaa mataji matatu.
Kocha mwenzake Mjerumani ambaye anaiongoza timu ya taifa ya wanawake Silvia Neid, alishinda tuzo hiyo kwa mara ya pili kwa upande wa wanawake. Aliishukuru FIFA kwa “kuitambua kandanda ya wanawake”.
Uwanjani katika soka la wanawake, mlinda lango wa Ujerumani na nahodha wa timu ya taifa Nadine Angerer, ambaye ni mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya, alimpiku Mbrazil Marta na Abby Wambach wa timu ya taifa ya Marekani.
Mwandishi: Bruce Amani/DW/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef

0 comments:

DIMBA NA CHAN ZAINGIA NUSU FAINALI

Katika dimba la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa timu za nyumbani, CHAN, Ghana, Libya, Nigeria na Zimbabwe zimeingia katika awamu ya nusu fainali mwishoni mwa wiki.
Ghana ilifunga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo goli moja kwa sifuri katika mechi ya mwisho ya robo fainali, na hivyo kujikatia tikiti ya kucheza mechi ya utani wa jadi dhidi ya mahasimu wake Nigeria katika nusu fainali. Kwabina Adusei alisukuma wavuni mkwaju wa penalty katika dakika ya 67.
Mapema jana jioni Libya iliipiku Gabon kwa mikwaju ya penalty katika mpambano mkali kabisa ambao ulikamilika kwa sare ya goli moja kwa moja katika muda wa kawaida na wa ziada. Sasa Libya itatiana kifua na Zimbabwe katika nusu fainali.
Siku ya Jumamosi, Nigeria ilinusia kichapo lakini ikapata ushindi wa magoli manne kwa matatu baada ya mechi kuingia muda wa ziada dhidi ya Morocco. Zimbabwe nayo iliwashangaza waliopigiwa upatu Mali kwa kuwafunga mabao mawili kwa moja. Mechi zote za nusu fainali zitachezwa Jumatano wiki hii.
Mwadishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

0 comments:

OBAMA AAPA KUIZUNGUKA CONGRESS

Rais wa Marekani Barack Obama ameapa kulizunguka bunge na kuchukua hatua kivyake ili kuwaimarisha watu wa tabaka la kati, akionyesha kukatishwa kwake tamaa na kasi ndogo ya kutunga sheria kwa upande wa bunge hilo.
Rais Obama akitoa hotuba yake kuhusu hali ya taifa. Rais Obama akitoa hotuba yake kuhusu hali ya taifa.
Katika ujumbe wake kwa bunge la Congress kupitia hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa, Obama aliahidi kuchukua hatua kukabiliana na ongezeko la ukosefu wa usawa, hata ikimbidi kufanya hivyo bila uungwaji mkono wa bunge, huku akiwataka wabunge kuweka pembeni tofauti za kisiasa na kufanya kazi kwa maslahi ya raia na kulipeleka mbele taifa hilo.
Rais Obama alisema nchi hiyo laazima iondokane na mawazo ya kupigana vita mara kwa mara ili kutoa fursa kwa diplomasia kutatua matatizo sugu ya ulimwengu, kama vile mgogoro wa nyukilia wa Iran. Obama pia alitoa wito wa kuchukuliwa hatua za dhati kuufufua uchumi wa Marekani, na kukabiliana na ukosefu wa usawa na kupanua fursa kwa raia wote wa taifa hilo.
Hadhira ikimsikiliza Obama katika ukumbi wa bunge la Congress. Hadhira ikimsikiliza Obama katika ukumbi wa bunge la Congress.
Mwaka wa kuchukuwa hatua
"Tuufanye mwaka huu kuwa mwaka wa kuchukuwa hatua. Hilo ndilo Wamarekani wengi wanalolitaka. Kwetu sote katika jumba hili, kuyajali maisha, matumaini na matarajio yao, na ninachoamini kinawaunganisha watu wa taifa hili bila kujali rangi, dini au chama wanakotoka, wadogo kwa wakubwa, matajiri na maskini, ni imani yao ya juu katika fursa kwa wote," alisema rais Obama aliekuwa akishangiliwa mara kwa mara na hadhira yake.
Hotuba ya Obama ilijikita hasa juu ya uchumi, mabadiliko ya tabianchi, mageuzi katika sera ya uhamiaji, Afghanistan na gereza la Guantanamo, Iran na kima cha chini cha mshahara. Hatua za Obama, ingawa zilionekana za kawaida, kwa pamoja ziliashiria kukatishwa tamaa kutokana na kasi ndogo ya kutunga sheria katika baraza la wawakilishi "Congress" linalodhibitiwa na chama cha Republicans, walio na uwezo wa kupunguza kasi ya ajenda ya rais.
"Fedheha" ya tofauti ya malipo
Alilitaka bunge kupandisha kima cha chini cha mshahara kutoka kiwango cha sasa cha dola 7.25 kwa saa hadi dola 10.10, huku akiyatolea wito makampuni pia kupandisha viwango vya mishahara na kuwalipa wanawake zaidi ya centi 77 wanazolipwa sasa kwa kila dola moja anayopata mwanaume, jambo aliloliita "fedheha."
Baadhi ya amri alizotangaza Obama katika hotuba hiyo ni pamoja na kupandisha kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wapya wa mikataba wa serikali ya shirikisho, na kuanzisha kwa akaunti za akiba kuwasaidia mamilioni ya watu kujiwekea akiba kwa ajili ya kustafu kwao, na mipango ya kuanzisha viwango vipya vya ufanisi wa mafuta kwa magari makubwa.
Alilitolea wito bunge kuruhusu majadiliano ya biashara kupitia kile kinachojulikana kama sheria ya kuharakisha, akisema ushirikiano mpya wa kibiashara kati ya Ulaya na Asia utasaidia kuunda nafasi zaidi za ajira. Obama alisema mageuzi katika sheria ya uhamiaji ni muhimu kwa uchumi, na kuongeza kuwa mageuzi hayo yanaweza kusaidia bajeti kwa kupunguza matumizi na kuongeza mapato yatokanayo na kodi.
Akisaini makaratasi ya mashabiki baada ya kutoa hotuba yake. Akisaini makaratasi ya mashabiki baada ya kutoa hotuba yake.
Fursa kwa diplomasia
Alisema pamoja na ukweli kwamba Marekani inaendelea kukabiliana na mitandao ya kigaidi kupita juhudi zinazolenga shabaha makhsusi na kujenga uwezo wa mataifa washirika, taifa hilo halipaswi kufikiria mara zote katika vita. Obama alizungumzia mafanikio ya kidiplomasia ya hivi karibuni chini ya waziri wa mambo ya nchi za kigeni, John Kerry, kuiondolea Syria silaha za kemikali, na kuanzisha tena mazungumzo kati ya Israel na Wapalestina.
Atetea mazungumzo na Iran
Aliwataka wabunge kutoiwekea vikwazo zaidi Iran, ili kutoa muda kwa mazungumzo kati ya taifa hilo la Kiislamu na mataifa makubwa sita. Akijibu ukosoaji wa wabunge juu ya kuzungumza na Iran, Obama alisema Marekani iko makini, na kwamba makubaliano yoyote hayatajengwa kwa misingi ya kuaminiana tu, bali kwa hatua zinazothibitika kwamba Iran hailengi kutengeneza bomu la nyuklia.
Syria, Afghanistan na Guantanamo
Rais huyo alizungumzia kwa muhtasari hali nchini Syria, na kusema utawala wake utaendelea kufanyia kazi mustakabali wanaostahiki watu wa Syria, usio na udikteta, vitisho wala hofu. Alisema wakati vita vya Afghanistan vikikaribia mwisho, huu unapaswa kuwa mwaka wa kuondoa vikwazo vilivyosalia kuhusu uhamishaji wa wafungwa, na kulifunga gereza la Marekani la Guantanamo lililoko katika ardhi ya Cuba.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/afpe,dpae,rtre.
Mhariri: Josephat Nyiro Charo

0 comments:

MAFUNDISHO YA MUNGU NA MTUMISHI WA MUNGU JOSEPHAT .E. MWINGIRA

Photo: Naibariki Jumatano yangu...
DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

(Darasa linaendelea lilipoishia jana...)
Ndivyo ilivyo katika maisha ya mtu, Mafanikio yake na Baraka zake; zina “Parasites” wadudu wanaokula hayo maisha yake. Sasa mdudu mkubwa anayekula maisha ya mtu ni laana, maana ndiye mdudu wa kwanza MUNGU alimtangaza. Tangazo la kwanza mdudu wa kuharibu maisha ya mtu ni laana, akasema maadamu umefanya kosa hili, nchi imelaaniwa.

Mnafahamu nchi ni udongo hivyo ardhi ikilaaniwa na ufahamu asili ya mwanadamu ni udongo. Sasa kimelaaniwa kile ambacho ni asili yako mwanadamu. Mti ukikata mizizi unanyauka na kukauka; tangazo la kwanza la kujua mateso ya mwanadamu tunajua kwamba asili yake imetokana na udongo kwa hiyo ardhi ambayo kwayo tumetoka. Na asili ya Baraka zote tunazoziona zinatokana na ardhi, fedha zinatoka kwenye ardhi, magari, miti, chakula, afya yako, nguo, wanyama, n.k. Sasa kipi ambacho hakikulaaniwa? Maana asili ya kile kitu ndicho kilicholaaniwa; hivyo hapa tunachotakiwa kuangalia kinachokutesa ni kuangalia laana gani inakutafuna wewe, maana laana ndiyo iliyotangazwa kwanza baada ya mwanadamu kukosa.

0 comments:

JUMUIYA YA UMOJA WA VIJANA CCM- UVCCM WAMSHAMBULIA LOWASA

 Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM, Paul Makonda

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), imemvaa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ikimtuhumu kuwa anafadhili mikakati ya kupingana na juhudi za sekretarieti ya chama hicho.
UVCCM imesema imeunga mkono kazi zinazofanywa na sekretarieti chini ya Katibu Mkuu, Abdulrahaman Kinana na wasaidizi wake akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda, alisema Lowassa anawatumia watu kusema hovyo kupitia vyombo vya habari juu ya kazi na juhudi zinazofanywa na sekretarieti.
“Lowassa amekuwa akiwatumia watu kusema ovyo, kwanza mwenyewe hana sifa ya kuwa rais wala kuwa amiri jeshi mkuu wa nchi, na kama wapo vijana hapa mjini wanaotaka fedha kwa haraka wamtafute,” alisema.
Makonda aliongeza kuwa UVCCM wanatambua na kuthamini juhudi za katibu mkuu na sekretarieti yake katika kukijenga chama kwa kusimamia barabara misingi na shabaha ya kuundwa kwake.
Alisema kuwa inapofika wakati wasimamizi wa chama wanaanza kupigwa vita juu ya kusimamia kanuni za chama hiyo si sahihi.
“Haiwezekani matajiri na watu wenye uchu wa madaraka watake kukihodhi chama na waratibu mikakati ya kukihujumu kwa fedha zao huku sisi vijana tukitazama. Tunasema kutakilinda chama chetu na tutawalinda viongozi wetu waadilifu,” alisisitiza.
Hata hivyo, Makonda alisema kuwa wanaobezwa leo kuwa wanaharibu chama ndio wameweza kurudisha imani ya wananchi kwa chama.
Kwamba imani na matumaini ambayo tayari yalishaanza kupotea na chama kuonekana si tena cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi wa nchi hii vimerejea.
Alifafanua kuwa mtu anayebeza ziara zilizofanyika na kuwaita viongozi waliozifanya kuwa ni waropokaji na wahuni, anapaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.
“Mhuni ni mtu mjinga, mtu wa hovyo, hana maadili, asiyependa chama. Mhuni ni mzandiki anayepaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine,” alisema Makonda.

0 comments:

CHADEMA WASHIKA NCHI WAFANYA MIKUTANI 87 MIKOANI NDANI YA WIKI MOJA

CHADEMA yafanya mikutano ya hadhara 87 mikoani ndani ya wiki mojaCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeshika nchi kwa kufanya mikutano ya hadhara zaidi ya 87 mikoani ndani ya wiki moja na kufanikiwa kupenyeza ajenda zake kwa wananchi kupitia operesheni yake ya M4C Pamoja Daima.


Operesheni hiyo ilianza Januari 22 mwaka huu, ikiwa na lengo la kuwafikisha viongozi hao katika mikoa yote ya Tanzania Bara, kupeleka ujumbe kwa umma kupitia ajenda tisa zilizopendekezwa na Kamati Kuu katika kikao chake kilichofanyika mwanzoni mwa mwezi huu.
Hii ni operesheni ambayo wadadisi wa masuala ya siasa wanasema itaisadia CHADEMA kujiimarisha na kuwapa wananchi fursa ya kujadili masuala muhimu yanayogubika taifa mwanzoni mwa mwaka 2014 baada ya misukosuko ya usaliti iliyokuwa imejitokeza.
Ajenda hizo zinazosambazwa na CHADEMA mikoani, ni mchakato wa katiba mpya katika hatua ya Bunge la Katiba, hususani suala la muundo wa serikali tatu ambalo CCM inataka kulipotosha ili liondolewe na kubakia na mfumo wa serikali mbili ambao umekuwa na kero.
Ajenda nyingine ni kura ya maoni; daftari la kudumu la wapiga kura ambapo wanakusanya orodha ya majina ya wananchi ambao wametimiza vigezo vya kujiandikisha, lakini hawajapatiwa haki hiyo ili kuishinikiza serikali iliboreshe kabla ya kura ya maoni.
Upo pia uchaguzi wa madiwani katika kata 27 ambao kampeni zake zinaendelea pamoja na ule wa jimbo la uwakilishi la Kiembe Samaki visiwani Zanzibar.
CHADEMA pia imejikita katika ujenzi wa chama ngazi za chini; uchaguzi ndani ya chama; uchaguzi serikali za mitaa na kuandaa umma kwa uchaguzi mkuu 2015.
Chama hicho ambacho kimejigawa katika vikosi sita vinavyotumia usafiri wa magari na helikopta, kimeweza kufika katika maeneo mengi nchi nzima kwa muda mfupi ikilinganishwa na ziara ya CCM mwishoni mwa mwaka jana ambapo walitumia wiki tatu katika mikoa mitatu ya Nyanda za Juu Kusini.
Ofisa habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, aliiambia Tanzania Daima Jumatano kuwa usafiri wa helikopta ni nafua na wa haraka ambao unawapa fursa ya kufanya mikutano kati ya mitano hadi saba katika mkoa mmoja kwa siku.
“Kama tungekuwa tunatumia magari kwa muda wa wiki hii moja tungekuwa tumeweza kufika katika mkoa mmoja, na hivyo mkakati wetu wa kutembea nchi nzima ndani ya wiki mbili usingefanikiwa.
“Na operesheni hizi zinagharamiwa kwa asilimia kubwa na michango ya wanachama na wafadhili wetu, ruzuku ya chama pekee haitoshi, watu wanajitolea kwa hali na mali,” alisema Makene.
Katika kuanza wiki ya pili na ya mwisho ya lala salama ya operesheni hiyo, vikosi vya CHADEMA vimebadilishana maeneo jana, ambapo Mwenyekiti, Freeman Mbowe baada ya kumaliza mikoa ya Geita na Kagera ameelekea Iringa.
Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa aliyekuwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini alisafiri kuelekea mkoani Geita huku timu ya Mwanasheria wa chama, Tundu Lissu ikiendelea kufunika anga mikoa ya Kanda ya Kati.
Mkurugenzi wa habari na mawasiliano, John Mnyika na timu yake, jana waliingia mkoani Shinyanga ambako wataunganisha hadi Simiyu.
Mbowe Geita
Janet Josiah anaripoti kutoka Geita kuwa juzi Mbowe alihutubia mkutano mkubwa wa hadhara na kusema kuwa serikali haina budi kuwawajibisha na kuwafikisha mahakamani maofisa wake wanaotuhumiwa kwa ufisadi.
Mbowe ambaye aliungana na Mnyika katika mkutano huo akitokea Kagera, aliwahimiza wananchi kuwaibua na kuwaweka hadharani baadhi ya maofisa wanaotumia ofisi zao kwa masilahi binafsi.
Akiwa Ngara, Bukoba mjini, Biharamulo kisha Geita, Mbowe alisema CHADEMA haiko tayari kuivumilia serikali ikiendelea kuwaacha viongozi hao pasipo kuwachukulia hatua.
Mkoani Geita, Mbowe alipokelewa kwa mabango ya kumponda aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto.
Mabango hayo yalikuwa na ujumbe mbalimbali ukiwemo ule uliosomeka “Katiba mpya ni lazima” na “CHADEMA kwanza Zitto baadaye”.
Mbowe alifafanua kuwa endapo wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba hawatasimamia hoja za Watanzania walizozitoa katika rasimu ya pili ya katiba, CHADEMA itazunguka tena nchi nzima kuwaambia waikatae katiba katika kura za maoni.
Alisema kuwa CHADEMA itawamahasisha Watanzania wasipige kura endapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi haitalifanyia maboresho daftari la kudumu la wapiga kura ili kuondoa watu waliokufa na kuwaongeza waliotimiza sifa za kuandikishwa.
Mnyika alisema kuwa anashangazwa kuwaona baadhi ya mafisadi wakiendelea kula maisha mitaani badala ya serikali kuwafungulia mashtaka.
Aliyataja baadhi ya makampuni hewa ambayo yametuhumiwa na maofisa wa serikali kujinufaisha kwa kutumia mikataba mibovu kuwa ni Richmond, IPTL, Net Group, Dowans, Songas na Symbion.
Lema Bukoba
Kutoka mjini Bukoba mkoani Kagera, Ashura Jumapili anaripoti kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, amewashauri wananchi kutokubali kuyumbishwa kwa dhana ya udini na ukabila.
Lema ambaye pia ni mbunge wa Arusha mjini, alisema kitendo hicho kitajenga makundi miongoni mwa jamii na hakitawaletea mabadiliko ya kimaendeleo.
Mbunge huyo alitoa ushauri huo juzi wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Bukoba ambao ulihudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.
Alisema kuwa CCM inawachanganya na kuwayumbisha wananchi kwa itikadi za udini na kabila ili wagawanyike katika makundi iendelee kuwatawala.
Kwa mujibu wa Lema, chama chochote hakiwezi kuongoza nchi bila kupata ushirikiano wa dini zote.
Alisema chama cha siasa ni taasisi, mmoja akitoka wengine wanaendeleza taasisi hiyo kwa mujibu wa kanuni na taratibu zilizowekwa.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Zanzibar), Said Issa Mohamed, alisema chama hicho hakina ubaguzi wa udini, ukabila wala umri.
Katika kudhihirisha hilo, aliwataja viongozi wa chama hicho ambao ni mwenyekiti Mbowe ambaye ni Mkristu Mlutheri, Dk. Slaa Mkristo Mkatoliki na yeye ambaye ni Muislamu wa dhehebu la Suni.
Lissu Dodoma
Danson Kaijage kutoka Dodoma, anaripoti kuwa Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu, amewatahadharisha viongozi wa dini kuwa makini na wanasiasa ambao wanatumia fedha zao kutangaza siasa makanisani au misikitini.
Alisema kuwa wanasiasa hao wanajipenyeza katika makanisa na misikiti kwa kujifanya watoaji wazuri wa misaada wakati ni sawa na mapepo na majini yanayosambaza virusi vya udini.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini hapa juzi, Lissu alisema baadhi ya viongozi wa CCM wanajipitisha makanisani na misikitini kuomba kura, jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa kasi ya kukua kwa dhambi ya udini.
“Wapo CCM (Waislamu) wanaozungukazunguka misikitini kueneza na kuchochea virusi vya udini, ukabila na ukanda, na wapo CCM (Wakristo) wanaojikomba makanisani kueneza hayo hayo, hao si waumini wa kweli, ni majini na mapepo,” alisema na kuongeza kuwa dawa yake ni kuwafukuza kwa sababu wanaweza kusababisha dhambi ya vita ya udini.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa (BAVICHA), John Heche, alitoa siri ya chama kurusha helikopta tatu na vikosi vitatu ardhini, akisema ni kuhakikisha Watanzania wanazinduliwa wasiuzwe kama nchi ilivyouzwa kwa wageni.
“Kuna watu wanasema tunatumia fedha vibaya kurusha helikopta tatu, nauliza, tumezichukua CCM? Hapana. Tumezichukua serikalini? Hapana. Tumetoa maisha yetu, tumefanya hivyo ili tuwahi kabla Watanzania hawajauzwa kama nchi ilivyouzwa kwa wageni,” alisema.
Heche pia aligusia hatua ya Serikali ya CCM kujaribu kufanya mipango ya kutaka kukwamisha urekebishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
“Kama CCM itakuwa kichwa ngumu isiboreshe daftari hilo, tutarusha helikopta kumi angani kuzunguka nchi nzima kila kata ili kuhakikisha tunatoa elimu kwa wananchi wapige kura za kukataa mchakato wa katiba mpya,”alisema Heche.

0 comments:

MWANAMKE ALIYETAPELI KWA AIRTEL MONEY ATUPWA JELA MIEZI SITA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu mkazi wa hapa kwenda jela miezi sita, kwa kosa la utapeli wa fedha kwa njia ya mtandao wa Airtel Money kwa mawakala mbalimbali wilayani humo.
Akitoa hukumu hiyo, Hakim Mkazi Mfawidhi, Joseph Ngomelo, alisema mshitakiwa Helena Alexandria, atakwenda jela miezi sita baada ya kukiri kufanya utapeli huo.
Mshitakiwa huyo alikiri kutapeli mawakala mbalimbali wa Airtel Money waliopo Nzega mjini kwa njia ya mtandao na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.
Alisema kifungo cha mama huyo kitakuwa fundisho kwa wanawake wangine wenye tamaa, kwani makosa kama hayo yakiachiwa yanaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii.
Awali Mwendesha Mashitaka wa Polisi Mkaguzi Msaidizi, Melito Ukongoji, aliiambia Mahakama hiyo kuwa Januari mosi mwaka 2014, mshitakiwa ambaye ni mkazi wa Nzega mjini, aliiba kwa kutumia mtandao wa Kampuni ya Airtel Money.
Alidai kuwa Hellena alikuwa akitumia ujumbe mfupi wa maneno wenye muamala wa kutoa pesa Sh 40,000 Airtel Money na kujipatia Sh 40,000 kwa kila wakala kwa nyakati tofauti.
 court-hammer
Akijitetea, mshitakiwa alikiri kuhusika na tuhuma hizo kwa nyakati tofauti na kuongeza kuwa lengo lilikuwa ni kutafuta fedha za kujikimu kimaisha kutokana ugumu wa maisha.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo Mwendesha Mashitaka aliiomba Mahakama hiyo itoe adhabu kwa mshitakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo za wizi wa utapeli kwa njia ya mtandao.

0 comments:

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ATOA SULUHU MZOZO KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI WILAYANI KITETO

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewataka wakazi wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wanaolima kwenye Hifadhi ya Jamii ya Emboley Murtangos, waridhie amri iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa ya kuwataka waondoke kwenye eneo hilo wakati Serikali ikitafuta ufumbuzi wa suala la wapi watakwenda.
 Pinda
“Wakazi walioko kwenye hifadhi ni lazima watii amri halali ya Mahakama ya Rufaa na waondoke katika eneo husika. Wakati mko nje, ramani iangaliwe upya na kubainisha wapi mipaka ipo na walio nje ya mipaka wasibughudhiwe,” alisema.
Waziri Mkuu ambaye aliwasili mjini Kiteto jana asubuhi akitokea Dodoma, alipokea taarifa fupi ya mapigano baina ya wakulima na wafugaji wilayani hapa, kisha akaenda kukagua eneo husika kabla ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kibaya.
Akitumia helikopta ya Polisi, Waziri Mkuu alikagua eneo husika na kuteremka kwenye vitongoji vya Mtanzania na Laitimi, ambako aliwapa pole wananchi waliokuwepo na kusikiliza risala katika kitongoji cha Mtanzania. Katika kitongoji hicho, watu sita waliuawa na katika kitongoji cha Laitimi, watu watatu waliuawa na kundi la wafugaji wapatao 40 -50.
“Vitendo vilivyofanyika ni uhalifu mkubwa, nimepata taabu na kujiuliza ni hasira za namna gani za watu kuamua kuua wakitoka kitongoji kimoja kwenda kingine? Hii hasira inatoka wapi? Na Kwa kosa lipi hasa,” alihoji Waziri Mkuu.
“Inaonekana ni kundi la watu ambao wameandaliwa na kujipanga, wanatoka eneo moja wanakwenda eneo jingine huku wamebeba silaha. Hapana! Hali hii haivumiliki. Mkuu wa Mkoa watu hawa ni lazima watafutwe haraka, na kila mbinu zitumike hadi wapatikane,” alisisitiza.
Aliwaeleza mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo kwamba kuna masuala mengi yanazunguka suala zima la Hifadhi ya Embuley Murtangos, yakiwemo ya kuchelewesha usajili wa eneo husika, uamuzi wa kutengwa kwa hifadhi hiyo na kutotambulika kwa mamlaka ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999. Aliutaka uongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na vijiji husika ikae na kupanga upya matumizi ya ardhi.
“Lazima mkoa na wilaya mfuatilie mihutasari ya vijiji saba iliyopitisha uamuzi huo iko wapi ili kujiridhisha kama maamuzi yaliyofanyika yalishirikisha wananchi wote,” alisema huku akishangiliwa kwa nguvu na wakazi hao.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alitumia fursa kuwaeleza wakazi hao kwamba hapa nchini hakuna ardhi ambayo haina mwenyewe.
Aliutaka Uongozi wa Mkoa kushirikiana na makamishna wa Polisi waliofika wilayani humo kuhakikisha wananchi wa eneo hilo wanakuwa salama.
kiteto
“Nisingependa kusikia kuna tukio jingine wakati uchunguzi ukiendelea,” alisema.
Mapema, katika taarifa yake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwillo alisema hadi kufikia Januari 13, mwaka huu watu 10 walikuwa wamepoteza maisha.
Pia alisema vibanda 60 vilichomwa moto, pikipiki sita na baiskeli 53 navyo pia vilichomwa moto.

0 comments:

LOVENESS DIVA ATANGAZA NIA YAKE YA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA 2015

Na hichi ndicho alichokiandika mtangazaji huyo
 
Natangaza nia ya kugombea ubunge mwaka 2015 na kuingia kwenye siasa rasmi 2015, kama kijana nina mengi ya kul isaidiataifa na jamii inayotuzunguka yenye vijana wengi, i want to inspire, motivate and my voice to be heard i want to speak up and there is no turning back GOD IS GOOD i need all strength and i got a big sopport in this from my close friend Solidarity madaraka kwa umma huo ndo ujumbe alioandika Diva ingawa bado hajaweka wazi ni jimbo gani atakalogombania. Ikiwa mtangazaji huyo atafanikiwa kuingia bungeni atakua ni mmoja kati ya watangazi walioingia katika siasa wakiwa na umri mdogo

0 comments:

TWASIRA ZA KIKAO CHA KISOMWA KWA RIPOTI ZA CAG ZILIZOPELEKEA MEYA WA BUKOBA KUJIUZULU

Kutoka kushoto: Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh wakiingia ukumbini leo mjini Bukoba.
Viongozi hao wakifungua kikao hicho cha kusomwa ripoti ya ukaguzi maalum ya CAG.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila akifungua kikao.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe akimkaribisha mgeni rasmi leo kwenye kikao hicho cha kukamilisha Ukaguzi Maalum " Exit Meeting" cha CAG.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh akisoma ripoti ya ukaguzi maalum leo Bukoba.
Baadhi ya waliohudhuria kikao hicho.
Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani (kulia) pamoja na Madiwani wa Manispaa ya Bukoba katika kikao hicho. Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (kulia) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh (kushoto) wakiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Bw. Fabian Massawe (kati) katika meza kuu.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (katikati) akimsikiliza kwa makini Bw. Ludovick Utouh. Viongozi meza kuu wote walikuwa makini  kusikiliza taarifa hiyo ya Ukaguzi. Taswira ya kikao hicho katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa.Madiwani wa Manispaa ya Bukoba pamoja na Mstahiki Meya Anatory Amani ambaye madiwani wa manispaa wanamtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.
 **
MEYA wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani amejiuzulu wakati Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Khamis Kaputa na wakuu wa idara tatu ambao ni Mhandisi Nimzihilwa, Ofisa Ugavi Baraka Marwa na Mweka Hazina Ulomi wakivuliwa uongozi baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh iliyosomwa leo katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera kutatua mgogoro uliokuwepo katika manispaa hiyo.

0 comments:

ARUSHA PROFFESION MOVIE SASA YAAMUA KUFANYA KWELI KATIKA TASINIA YA FILAMU NCHINI

0 comments: